Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu(Sehemu ya Kwanza)
Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo, na mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kufanya mipango yako mwenyewe, na huna uwezo wa kujitawala mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinadhibitiwa na mikono Yake.
Kama kazi ya Mungu ilimkimu mwanadamu kwa kumpa hatima, hatima ya ajabu, kabla ya wakati, na kama Mungu alitumia hii kumshawishi mwanadamu na kusababisha mwanadamu kumfuata Yeye—kama Yeye alifanya mpango na mwanadamu—basi huu haungekuwa ni ushindi, wala haingekuwa kufanya kazi katika maisha ya binadamu. Kama Mungu angetumia hatima ya mambo kumtawala au kumdhibiti mwanadamu na kupata moyo wake, basi kwa hii Hangekuwa anamkamilisha mwanadamu, wala Hangeweza kumpata mwanadamu, lakini badala yake angekuwa akitumia hatima kumdhibiti. Mwanadamu anajali tu kuhusu hatima ya siku zijazo, hatima, na kama kuna ama hamna kitu kizuri cha kutumainia. Iwapo mwanadamu angepewa matumaini mazuri wakati wa kazi ya ushindi, na kama, kabla ya kushindwa kwa mwanadamu, yeye angepewa hatima ifaayo ya kufuata, basi kushindwa kwa mwanadamu kusingekosa kuwa na athari tu, bali athari za kushindwa zingeshawishika pia. Hivi ni kusema kwamba, kazi ya ushindi inafanikisha mazao yake kwa kuchukua hatima na matarajio ya mwanadamu na kuhukumu na kuadibu uasi wa tabia ya mwanadamu. Haifanikishwi kwa kufanya mpango na mwanadamu, yaani, kwa kumpa mwanadamu baraka na neema, lakini ni kwa kufichua uaminifu wa mwanadamu kwa kumnyang’anya uhuru wake na kukomesha matarajio yake. Hiki ni kiini cha kazi ya ushindi. Kama mtu angepewa matumaini mazuri hapo mwanzoni sana, na kazi ya kuadibu na hukumu zingefanywa baadaye, basi mwanadamu angekubali kuadibu huku na hukumu kwa msingi kwamba alikuwa na matarajio, na mwishowe, utiifu na ibada ya Muumba isiyo na masharti ya viumbe vyote vyake haingetimizika; kungekuwepo tu na utiifu wenye upofu na wa ujinga, au pengine mwanadamu angetoa madai yasiyo na msingi kwa Mungu, na ingekuwa ni vigumu kushinda moyo wa mwanadamu. Kwa hivyo, kazi kama hii ya ushindi haingekuwa na uwezo wa kumpata mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Viumbe kama hawa hawangeweza kutekeleza jukumu lao, na wangeweza tu kufikia makubaliano na Mungu; hii haitakuwa ushindi, lakini huruma na baraka. Tatizo kubwa mno kwa mwanadamu ni kuwa yeye hufikiria tu kuhusu hatima yake na matarajio, na kuyaabudu. Mwanadamu humfuata Mungu kwa ajili ya hatima yake na matarajio; yeye hamwabudu Mungu kwa sababu ya upendo wake kwake. Na kwa hivyo, katika ushindi kwa mwanadamu, ubinafsi wa mwanadamu, uroho na vitu ambavyo sana sana huzuia ibada yake kwa Mungu ni sharti viondolewe. Kwa kufanya hivyo, matokeo ya ushindi kwa mwanadamu yatatimizwa. Hivyo, katika ushindi wa kwanza wa mwanadamu ni muhimu kwanza kuondoa matarajio makubwa ya mwanadamu na udhaifu unaohuzunisha kabisa, na, kupitia hili, kufichua upendo wa mwanadamu kwa Mungu, na kubadilisha maarifa yake kuhusu maisha ya binadamu, mtazamo wake kwa Mungu, na maana ya kuwepo kwake. Kwa njia hii, upendo wa mwanadamu kwa Mungu unatakaswa, ambapo ni kusema, moyo wa binadamu unashindwa. Lakini katika mtazamo wake wa viumbe vyote, Mungu hashindi kwa sababu ya kushinda; badala yake, Yeye anashinda ili kumpata mtu, kwa sababu ya utukufu wake mwenyewe, na ili kuokoa ufanano wa kwanza wa awali wa mwanadamu. Kama angeshinda kwa ajili ya kushinda, basi umuhimu wa kazi ya ushindi ungepotea. Hiyo ni kusema kuwa ikiwa, baada ya kumshinda mwanadamu, Mungu alikata tamaa kwa ajili ya mwanadamu, na hakuzingatia maisha au kifo chake, basi hii haitakuwa usimamizi wa mwanadamu, wala kumshinda mwanadamu haitakuwa ni kwa ajili ya wokovu wake. Ni upato wa mwanadamu tu kufuatia ushindi kwake na ujio wake wa mwisho katika hatima ya ajabu ndiyo yaliyomo katika kiini cha kazi yote ya wokovu, na ni hii tu ndio inayoweza kufikia lengo la wokovu wa mwanadamu. Kwa maneno mengine, ni ufikaji wa mwanadamu katika hatima nzuri na kuingia kwake katika mapumziko tu ndiyo matarajio ambayo yanatakiwa yamilikiwe na viumbe vyote, na kazi ambayo lazima ifanywe na Muumba. Kama mwanadamu ndiye ambaye angefanya kazi hii, basi kazi hii ingekuwa kidogo sana. Ingemchukua mwanadamu hadi kiwango fulani, lakini haingekuwa na uwezo wa kumleta mwanadamu katika hatima ya milele. Mwanadamu hana uwezo wa kuamua hatima ya mwanadamu, wala, zaidi ya hayo, hana uwezo wa kuhakikisha matarajio na hatima ya baadaye ya binadamu. Kazi inayofanywa na Mungu, hata hivyo, ni tofauti. Tangu Yeye amuumbe mwanadamu, Yeye anamwongoza; kwa sababu Yeye humwokoa mwanadamu, atamwokoa mwanadamu kwelikweli, na atampata kikamilifu’; kwa kuwa Yeye humwongoza mwanadamu, atamleta kwenye hatima inayofaa; na kwa kuwa Yeye alimuumba mwanadamu na humsimamia mwanadamu, ni sharti Achukue jukumu la hatima ya mwanadamu na matarajio yake. Ni hii ndio kazi ambayo hufanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inatimizwa kwa kutakasa matarajio ya mwanadamu, hatimaye ni lazima mwanadamu aletwe kwenye hatima ifaayo aliyotengenezewa na Mungu kwa ajili yake. Ni kwa sababu hasa kuwa Mungu hufanya kazi katika mwanadamu ndiyo maana mwanadamu ana hatima na hatima yake ni ya uhakika. Hapa, hatima ifaayo inayoangaziwa sio matumaini na matarajio yaliyotakaswa katika nyakati za zamani, hizi mbili ni tofauti. Kitu ambacho mwanadamu hutumainia na kufuata ni tamaa za harakati ya hamu ya kimwili iliyo badhirifu, badala ya hatima ya mwanadamu anayotazamiwa. Kile ambacho Mungu amemwandalia mwanadamu, wakati huo huo, ni baraka na ahadi alizoandaliwa mwanadamu mara baada ya kutakaswa, ambayo Mungu alimtayarishia mwanadamu baada ya kuumba ulimwengu, na ambayo haitiwi doa na uchaguzi, dhana, mawazo au mwili wa mwanadamu. Hatima hii haitayarishwi kwa ajili ya mtu fulani, lakini ni mahali pa kupumzikia pa wanadamu wote. Na kwa hivyo, hii hatima ni hatima inayofaa zaidi kwa wanadamu.
Muumba anakusudia kupanga viumbe vyote. Wewe ni lazima usitupe au kutokaidi chochote ambacho Yeye anakifanya, wala usiwe na uasi kwake. Kazi ambayo Yeye hufanya hatimaye itahitimisha nia yake, na katika hii atapata utukufu. Leo, ni kwa nini haisemwi kwamba nyinyi ni wa uzao wa Moabu, au watoto wa joka kuu jekundu? Je, ni kwa nini hakuna mazungumzo ya wateule, na mazungumzo pekee ni ya viumbe? Kiumbe—hili lilikuwa jina la asili la mwanadamu, na ni hili ndilo utambulisho wake wa asili. Majina yanatofautiana tu kwa sababu nyakati na vipindi ni tofauti; kwa kweli, mwanadamu ni kiumbe wa kawaida. Viumbe wote, ikiwa ni wapotovu zaidi ama ni watakatifu sana, ni lazima watekeleze wajibu wa kiumbe. Wakati Yeye anafanya kazi ya ushindi, Mungu hakudhibiti kwa kutumia matarajio yako, majaliwa au hatima. Kwa kweli hakuna haja ya kufanya kazi kwa namna hii. Lengo la kazi ya ushindi ni kumfanya mwanadamu atekeleze wajibu wa kiumbe, kumfanya aabudu Muumba, na ni baada ya hii tu ndivyo ataweza kuingia kwenye hatima ya kustaajabisha. Majaliwa ya mwanadamu yanadhibitiwa na mikono ya Mungu. Wewe huna uwezo wa kujidhibiti mwenyewe: Licha ya mwanadamu yeye mwenyewe daima kukimbilia na kujishughulisha, anabakia bila uwezo wa kujidhibiti. Kama ungejua matarajio yako mwenyewe, kama ungeweza kudhibiti majaliwa yako mwenyewe, ingekuwa wewe bado ni kiumbe? Kwa kifupi, bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi, kazi yote yake ni kwa ajili ya mwanadamu. Chukua, kwa mfano, mbingu na nchi na vitu vyote ambavyo Mungu aliviumba ili kumhudumia mwanadamu: mwezi, jua, na nyota ambazo Yeye alimuumbia mwanadamu, wanyama na mimea, majira ya machipuko, majira ya joto, vuli na baridi, na kadhalika—yote ni kwa ajili ya kuwepo kwa mwanadamu. Na kwa hivyo, bila kujali ni jinsi gani anavyoadibu na kuhukumu mwanadamu, yote ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Japokuwa yeye humnyang’anya mwanadamu matumaini yake ya kimwili, ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, na utakaso wa mwanadamu ni kwa ajili ya kuishi kwake. Hatima ya mwanadamu iko mikononi mwa Muumba, hivyo ni jinsi gani mwanadamu anaweza kujidhibiti mwenyewe?
Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani. Nguzo ya maisha mema kama haya ni lazima iwe hivyo, hivi kwamba baada ya mwanadamu kutakaswa na kushindwa, anajiwasilisha mbele za Muumba. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu kabla ya wanadamu kuingia katika hatima ya ajabu. Maisha kama haya ni maisha ya baadaye ya mwanadamu duniani, ni maisha yanayopendeza zaidi duniani, aina ya maisha ambayo mwanadamu ametamania, aina ambayo mwanadamu hajawahi kamwe kutimiza katika historia ya ulimwengu. Ni matukio ya mwisho ya miaka 6,000 ya kazi ya usimamizi, na ndicho wanadamu wanatamani sana, na pia ni ahadi ya Mungu kwa mwanadamu. Lakini ahadi hii haiwezi timika mara moja: Mwanadamu ataingia katika hatima ya mbeleni punde tu kazi ya siku za mwisho zitakapokuwa zimemalizika na yeye amekwisha kushindwa kikamilifu, yaani, punde tu Shetani atakapokuwa ameshindwa kabisa. Mwanadamu atakuwa hana asili ya kutenda dhambi baada ya kusafishwa, kwa sababu Mungu atakuwa amemshinda Shetani, ambayo ina maana kuwa hakutakuwepo na kuvamiwa na vikosi vya uhasama, na hakuna vikosi vya uhasama ambavyo vinaweza kushambulia mwili wa mwanadamu. Na kwa hivyo mwanadamu atakuwa huru, na mtakatifu—yeye atakuwa ameingia ahera. Ni kama tu vikosi vya uhasama wa giza vitakuwa vimefungwa ndipo mwanadamu atakuwa huru kokote aendako, na bila uasi au upinzani. Shetani ni sharti awe amefungwa ili mwanadamu awe sawa; leo, hayuko sawa kwa sababu[a] Shetani bado huchochea shida kila mahali hapa duniani, na kwa sababu kazi nzima ya usimamizi wa Mungu bado haijafika mwisho wake. Punde tu Shetani anaposhindwa, mwanadamu atakuwa amekombolewa kikamilifu; wakati mwanadamu anampata Mungu na anatoka katika kumilikiwa na Shetani, atatazama jua ya haki. Maisha atakayolipwa mwanadamu wa kawaida yatarejeshwa; yote yale ambayo ni lazima yamilikiwe na mwanadamu wa kawaida—kama uwezo wa kupambanua mema na mabaya, na kufahamu jinsi ya kula na kujivisha mwenyewe, na uwezo wa kuishi kama kawaida—yote haya yatarejeshwa. Hata kama Hawa hakuwa amejaribiwa na nyoka, mwanadamu ni lazima angekuwa na maisha kama haya ambayo ni ya kawaida baada ya kuumbwa hapo mwanzo. Ni lazima angekula, angevishwa, na kuendelea na maisha ya mwanadamu wa kawaida hapa duniani. Ila baada ya mwanadamu kupotoshwa, maisha haya yakawa ndoto, na hata leo mwanadamu hathubutu kufikiri mambo kama haya. Kwa kweli, maisha haya ya kupendeza ambayo mwanadamu anatamani ni haja yake: Iwapo mwanadamu angekuwa hana hatima kama hii, basi maisha yake ya duniani yaliyopotoshwa kamwe hayangekoma, na kama hakungekuwepo na maisha yakupendeza kama haya, basi hakungekuwa na hitimisho la majaliwa ya Shetani au kwa enzi ambayo Shetani ana utawala duniani kote. Mwanadamu ni sharti awasili kwenye ufalme ambao huwezi kufikiwa na nguvu za giza, na wakati atawasili, hii itathibitisha ya kwamba Shetani amekwisha shindwa. Kwa njia hii, punde tu hakuna usumbufu wa Shetani, Mungu mwenyewe atamdhibiti mwanadamu, na Yeye ataamuru na kudhibiti maisha yote ya mwanadamu; hii tu ndiyo itahesabika kama kushindwa kwa Shetani. Maisha ya mwanadamu leo ni sanasana maisha ya uchafu, na bado ni maisha ya kuteseka na mateso. Hii haingeitwa kushindwa kwa Shetani; mwanadamu bado hajatoroka kutoka katika bahari ya mateso, bado hajatoroka kutoka katika ugumu wa maisha ya mwanadamu, ama ushawishi wa Shetani, na bado yeye ana maarifa ya Mungu lakini kidogo sana. Taabu zote za mwanadamu ziliumbwa na Shetani, ni Shetani ndiye alileta mateso katika maisha ya mwanadamu, na ni baada tu ya Shetani kufungwa ndipo mwanadamu ataweza kutoroka kikamilifu kutoka katika bahari ya mateso. Na bado utumwa wa Shetani unahitimika kupitia kushindwa na kupatwa kwa moyo wa mwanadamu, kwa kumfanya mwanadamu mabaki ya vita dhidi ya Shetani. Leo, harakati ya mwanadamu ya kukuwa mshindi na kufanywa mkamilifu ni vitu ambavyo vinafuatwa kabla yeye hajakuwa na maisha ya mtu wa kawaida duniani, na ndiyo malengo ambayo mwanadamu hutafuta kabla ya utumwa wa Shetani. Kwa kiini, harakati ya mwanadamu ya kukuwa mshindi na kufanywa kamili, au kufanywa wa kutumika vilivyo, ni kutoroka kutoka katika ushawishi wa Shetani. Harakati ya mwanadamu ni kuwa mshindi, lakini matokeo ya mwisho yatakuwa ni kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ni kwa kutoroka kutoka kwa ushawishi wa Shetani tu ndipo mwanadamu ataweza kuishi maisha ya mtu wa kawaida duniani, maisha ya kumwabudu Mungu. Leo, harakati ya mtu ya kukuwa mshindi na kufanywa kamilifu ndiyo mambo ambayo yanafuatwa kabla ya kuwa na maisha ya mtu wa kawaida duniani. Haya yanafuatwa kimsingi kwa ajili ya kutakaswa na kuweka ukweli katika vitendo, na ili kufanikisha ibada ya Muumba. Kama mwanadamu anamiliki maisha ya mtu wa kawaida duniani, maisha ambayo hayana taabu na matatizo, basi mwanadamu hawezi kushiriki katika harakati za kuwa mshindi. “Kuwa mshindi” na “kufanywa kamili” ni malengo ambayo Mungu humpa mwanadamu kufuatilia, na katika ufukuziaji wa malengo haya, Yeye husababisha mwanadamu kuweka ukweli katika vitendo na kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye umuhimu. Lengo ni kumkamilisha mtu na kumpata yeye, na harakati ya kukuwa mshindi na kufanywa kamili ni njia tu. Kama, hapo mbeleni, mwanadamu ataingia kwenye hatima ya ajabu, hakutakuwepo na kurejelea kuwa mshindi na kukamilika, kutakuwepo tu na kila kiumbe kikitekeleza wajibu wake. Leo, mwanadamu anafanywa kufuata mambo haya tu ili kufafanua upeo wa mwanadamu, ili harakati ya mwanadamu ilengwe zaidi na iwe ya utendaji zaidi. Bila hayo, harakati ya mwanadamu ya kuingia katika uzima wa milele ingekuwa sio dhahiri na ya kudhania, na kama ingekuwa hivyo, je, si mwanadamu hata angelikuwa hafifu hata zaidi? Kufuata njia hii, bila malengo au kanuni—je, hii sio kujidanganya? Hatimaye, harakati hii ingekuwa kama kawaida bila mazao; na mwishowe, mwanadamu bado angemilikiwa na Shetani na hangeweza kujinasua mwenyewe kutokana nayo. Mbona ajikabili mwenyewe kwenye harakati kama hii isiyo na sababu? Wakati mwanadamu ataingia kwenye hatima ya milele, mwanadamu atamwabudu Muumba, na kwa sababu mwanadamu amepata wokovu na kuingia ahera, mwanadamu hawezi kimbiza malengo yoyote, wala, zaidi ya hayo, yeye hatakuwa na haja ya kuhangaika kuwa atazingirwa na Shetani. Kwa wakati huu, mwanadamu atajua nafasi yake, na atatekeleza wajibu wake, na hata kama hataadibiwa au kuhukumiwa, kila mtu atatekeleza jukumu lake. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa kiumbe katika sura na hadhi pia. Hakutakuwepo tena na tofauti ya juu na chini; kila mtu atatekeleza tu kazi tofauti. Bado mwanadamu ataishi katika hatima ya wanadamu yenye utaratibu na ifaayo, mwanadamu atatekeleza wajibu wake kwa ajili ya kumwabudu Muumba, na wanadamu kama hawa ni wanadamu wa milele. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa amepata maisha yaliyoangaziwa na Mungu, maisha chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, na maisha pamoja na Mungu. Wanadamu wataishi maisha ya kawaida duniani, na wanadamu wote wataingia katika njia sahihi. Mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 utakuwa umemshinda Shetani kabisa, ambayo ina maana kuwa Mungu atakuwa amerejesha sura ya awali ya mwanadamu kufuatia kuumbwa kwake, na kwa hivyo, nia ya awali ya Mungu itakuwa imetimizwa. Hapo mwanzo, kabla mwanadamu hajapotoshwa na Shetani, mwanadamu aliishi maisha ya kawaida duniani. Baadaye, alipopotoshwa na Shetani, mwanadamu alipoteza maisha haya ya kawaida, na kwa hivyo kazi ya Mungu ya usimamizi ikaanza, na vita dhidi ya Shetani ikaanza ili kurejesha maisha ya kawaida ya mwanadamu. Ni wakati tu ambapo usimamizi wa kazi ya Mungu wa miaka 6,000 utafikia kikomo ndipo maisha ya mwanadamu yatakapoanza rasmi hapa duniani, ni wakati huo tu ndipo mwanadamu atakapokuwa na maisha mazuri, na Mungu atarejesha lengo la kumuumba mwanadamu hapo mwanzoni, na pia kufanana kwake kwa asili na mwanadamu. Na kwa hivyo, punde tu atakuwa na maisha ya kawaida ya mwanadamu duniani, mwanadamu hatafuatilia kuwa mshindi ama kuwa kamili, kwa kuwa mwanadamu atakuwa mtakatifu. Ushindi na ukamilifu uliosemwa na mwanadamu ndiyo malengo yaliyopewa mwanadamu ili kufuata wakati wa vita kati ya Mungu na Shetani, na yapo tu kwa sababu mwanadamu amepotoshwa. Ni kwa kukupa lengo, na kukufanya wewe kufuata lengo hili, ndipo Shetani atashindwa. Kukuambia uwe mshindi au ufanywe kamili ama utumike kunahitaji ya kwamba uwe na ushuhuda ili umwaibishe Shetani. Mwishowe, mwanadamu ataishi maisha ya mwanadamu wa kawaida duniani, na mwanadamu atakuwa mtakatifu, na wakati hii itatendeka, je, watatafuta kuwa washindi? Je, wote si viumbe? Kuwa mshindi na kuwa yule aliyekamilika yote mawili yanaelekezwa kwa Shetani, na uchafu wa mwanadamu. Je, hii “mshindi” si kuhusu ushindi dhidi ya Shetani na majeshi ya uhasama? Unaposema kuwa wewe umefanywa mkamilifu, nini hicho ndani yako ambacho kimekamilishwa? Je, si kuwa umevua mwenyewe tabia potovu ya kishetani, ili uweze kufaulu kupata upendo mkuu wa Mungu? Mambo kama haya yanasemekana kuhusu mambo machafu ndani ya mtu, na kuhusu Shetani; na hayasemwi kuhusu Mungu.
Leo, kama haufuatilii kuanza kuwa mshindi na kukamilishwa, basi mbeleni, wakati mwanadamu ataishi maisha ya kawaida duniani, hakutakuwa na nafasi ya harakati kama hizo. Wakati huo, hatima ya kila aina ya mtu itakuwa imefichuliwa. Wakati huo, itakuwa wazi wewe ni kitu cha aina gani, na kama unataka kuwa mshindi au unataka kukamilishwa haitawezekana. Ni hivyo tu kwa sababu ya uasi wake mwanadamu ataadhibiwa baada ya kufichuliwa. Wakati huo, harakati za mtu hazitakuwa za juu kuliko za watu wengine, kwa wengine kuwa washindi na wengine kukamilika, au kwa wengine kuwa wazaliwa wa kwanza wa Mungu na wengine kuwa wana wa Mungu; hawatafuatilia vitu hivi. Wote watakuwa viumbe vya Mungu, wote wataishi duniani, na wote wataishi duniani pamoja na Mungu. Sasa ni wakati wa vita kati ya Mungu na Shetani, ni wakati ambapo vita hivi havijahitimishwa bado, wakati mwanadamu bado hajapatwa kikamilifu, na ni kipindi cha mpito. Na kwa hivyo, mwanadamu anatakiwa afuatilie kuwa mshindi au mmoja wa watu wa Mungu. Leo kuna tofauti baina ya hadhi, lakini wakati utawadia ambapo hakutakuwepo na tofauti kama hizo: Hadhi ya wote hao ambao wamekuwa washindi itakuwa sawa, wote watakuwa wamehitimu kuwa wanadamu, na wataishi duniani kwa usawa, kwa maana kuwa wote watakuwa viumbe wenye sifa zinazostahili, na chochote watapewa kitakuwa sawa. Kwa kuwa nyakati za kazi ya Mungu ni tofauti, na madhumuni ya kazi yake ni tofauti pia, kama kazi hii inafanyika ndani yenu, nyinyi mnafaa kufanywa kamili na kuwa washindi; kama ingefanyika ng’ambo, basi wangekuwa na stahiki ya kuwa kundi la watu la kwanza kushindwa, na kundi la watu la kwanza la kufanywa kamilifu. Leo, kazi hii haifanywi kule ng’ambo, na kwa hivyo hawastahiki kufanywa wakamilifu ama kuwa washindi, na haiwezekani wao kukuwa kundi la kwanza. Kwa kuwa nia ya kazi ya Mungu ni tofauti, enzi ya kazi ya Mungu ni tofauti, na upeo wake ni tofauti, hivyo kuna kundi la kwanza, yaani, kuna washindi, na pia vile vile kutakuwa na kundi la pili ambalo ni la kufanywa kamilifu. Punde tu kunapokuwa na kundi la kwanza lililokamilishwa, kutakuwa na kiolezo na mfano, na hivyo mbeleni kutakuwa na kundi la pili na la tatu la wale wanakamilishwa, lakini ahera wote watakuwa sawa, na hakutakuwa na uainishaji wa hadhi. Wote watakuwa tu wamefanywa wakamilifu katika nyakati tofauti, na hakutakuwa na tofauti katika hadhi. Wakati utakapofika kila mtu amefanywa wakamilifu, na kazi ya ulimwengu mzima imehitimishwa, hakutakuwa na kulinganisha kwa hadhi, na wote watakuwa wa hadhi sawa. Leo, kazi hii inafanywa kati yenu ili muweze kuwa washindi. Kama ingefanyika nchini Uingereza, basi Uingereza ingekuwa kundi la kwanza, kwa njia sawa na vile mtakavyokuwa. Mimi mahsusi nakuwa tu mwenye neema ya kufanya kazi Yangu ndani yenu leo, na kama Singefanya kazi ndani yenu, basi kwa usawa mngekuwa kundi la pili, au la tatu, au la nne, au la tano. Hii ni kwa sababu tu ya utofauti katika utaratibu wa kazi; kundi la kwanza na kundi la pili haliashirii kuwa moja ni la juu au la chini kuliko lingine, inaashiria tu utaratibu ambao upo wa watu hawa kufanywa wakamilifu. Leo maneno haya yanawasiliwa kwenu, lakini mbona hamkuwa mmefahamishwa mapema? Kwa sababu, bila mchakato, watu huwa wanakaa kuenda kuzidi kiasi. Kwa mfano, wakati huo Yesu alisema kwamba: “Kama Nilivyoondoka, ndivyo Nitakavyowasili.” Leo, wengi wamepumbazwa na maneno haya, na wanataka tu kuvaa mavazi meupe wakisubiri kuchukuliwa kwenda mbinguni. Kwa hivyo, kuna maneno mengi ambayo hayawezi kusemwa mapema mno; kama yangesemwa mapema mno, mwanadamu angeenda kuzidi kiasi. Kimo cha mwanadamu ni kidogo mno, na hana uwezo wa kuona kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ukweli wa maneno haya.
Wakati mtu anafanikiwa kupata maisha ya ukweli ya mwanadamu duniani, vikosi vizima vya Shetani vitafungwa, na mwanadamu ataishi kwa urahisi katika ardhi. Mambo hayatakuwa magumu kama yalivyo sasa: Mahusiano ya binadamu, mahusiano ya kijamii, mahusiano changamani ya kifamilia…., haya ni ya kusumbua, machungu mno! Maisha ya mwanadamu hapa ni duni! Punde tu mwanadamu anaposhindwa, moyo wake na akili yake vitabadilika: atakuwa na moyo unaomcha Mungu na moyo ambao unampenda Mungu. Punde tu wote walio ulimwenguni ambao wanatafuta upendo wa Mungu wanaposhindwa, ambayo ni kusema, punde tu Shetani anaposhindwa, na punde tu Shetani—nguvu zote za giza—zimekwisha fungwa, basi maisha ya mwanadamu duniani yatakuwa yasiyotaabishwa, na ataweza kuishi huru duniani. Kama maisha ya mwanadamu hayana mahusiano ya kimwili, na hayana changamani za mwili, basi itakuwa rahisi mno. Mahusiano ya kimwili ya mwanadamu ni changamani mno, na kwa mwanadamu kuwa na mambo kama hayo ni thibitisho kuwa yeye bado hajajikomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kama ungekuwa na uhusiano sawa na ndugu na dada, kama ungekuwa na uhusiano sawa na familia yako ya kawaida, basi hungekuwa na wasiwasi, na hungekuwa na haja ya kuhofia kuhusu mtu yeyote. Hakuna kitakachoweza kuwa bora zaidi, na kwa njia hii mwanadamu atapunguziwa nusu ya mateso yake. Kuishi maisha ya kawaida ya binadamu duniani, mwanadamu atakuwa sawa na malaika; ingawa atakuwa bado na mwili, atakuwa sawa na malaika. Hii ni ahadi ya mwisho, ni ahadi ya mwisho ambayo mwanadamu amezawadiwa. Leo mwanadamu anapitia kuadibu na hukumu; Je, unafikiri matukio kama haya ya mwanadamu hayana maana? Je, kazi ya kuadibu na kuhukumu inaweza kufanywa bila sababu. Hapo awali ilisemekana kuwa kuadibu na kuhukumu mwanadamu ni kumweka katika shimo lisilo na mwisho, ambayo ina maana ya kuchukua majaliwa na matarajio. Hii ni kwa ajili ya jambo moja: utakasaji wa mwanadamu. Mwanadamu hawekwi kwenye shimo lisilo na mwisho kimakusudi, ambapo baadaye Mungu hukata tamaa juu yake. Badala yake, ni ili kushughulika na uasi ndani ya mwanadamu, ili hatimaye mambo ndani ya mwanadamu yaweze kutakasika, ili aweze kuwa na ufahamu wa kweli wa Mungu, na awe kama mtu mtakatifu. Iwapo hii itafanywa, basi yote yatakuwa yametimia. Kwa kweli, wakati mambo hayo ndani ya mwanadamu ambayo yanapaswa kushughulikiwa yameshughulikiwa, na mwanadamu anakuwa na ushuhuda wa mwangwi, Shetani pia atashindwa, na hata ingawa kunaweza kuwa na mambo machache ambayo awali ndani ya mwanadamu hayakuwa yametakasika kabisa, punde tu Shetani ameshindwa, Shetani hawezi tena kusababisha taabu, na wakati huo mwanadamu atakuwa ametakaswa kabisa. Mwanadamu hajawahi kupitia maisha kama haya, lakini wakati Shetani anashindwa, yote yatakuwa yametulizwa na mambo hayo pumbavu ndani ya mwanadamu yatatatuliwa yote; matatizo mengine yote yataisha punde tu tatizo kuu litakapokuwa limetatuliwa. Wakati wa kupata kwa mwili kwa Mungu duniani, wakati Yeye binafsi anafanya kazi miongoni mwa watu, kazi yote ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na Yeye atamshinda Shetani kupitia kumshinda mwanadamu na kuwafanya kamili. Wakati nyinyi mtakuwa na ushuhuda wa ajabu, hii, pia, itaonyesha kushindwa kwa Shetani. Kwanza mwanadamu anashindwa na hatimaye anafanywa kamili kabisa ili kumshinda Shetani. Kwa kiini, hata hivyo, pamoja na kushindwa kwa Shetani hii pia vilevile ni wokovu wa wanadamu wote kutoka kwa shimo la bahari hii ya mateso. Bila kujali kama kazi hii inatendeka katika ulimwengu mzima au katika nchi ya China, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani na kuleta wokovu kwa wanadamu wote ili mwanadamu aweze kuingia pahali pa kupumzika. Unaona, mwili wa kawaida wa Mungu mwenye mwili ni kwa usahihi kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni kuleta wokovu kwa wale wote walioko chini ya mbingu wanaompenda Mungu, ni kwa ajili ya kushinda wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, kwa ajili ya kumshinda Shetani. Msingi wa kazi yote ya Mungu ya usimamizi haitengani na kushindwa kwa Shetani ili kuleta wokovu kwa watu wote. Kwa nini, katika mengi ya kazi hii, daima inasemekana kwenu kuwa na ushuhuda? Na ushuhuda huu unaelekezewa nani? Je, si unaelekezwa kwa Shetani? Ushuhuda huu unafanyiwa Mungu, na unafanywa ili kushuhudia kuwa kazi ya Mungu imetimiza matokeo yake. Kuwa na ushuhuda inahusiana na kazi ya kumshinda Shetani; kama hakungekuwa na vita dhidi ya Shetani, basi mwanadamu hangetakiwa kuwa na ushuhuda. Ni kwa sababu kwamba Shetani lazima ashindwe, kwa wakati huo huo kama kuokoa mwanadamu, Mungu anataka kwamba mwanadamu awe na ushuhuda wake mbele ya Shetani, ambao Yeye hutumia kufanya vita na Shetani. Kwa hivyo, mwanadamu ni mlengwa wa wokovu na chombo cha kumshinda Shetani, na kwa hivyo mwanadamu yumo katika msingi wa usimamizi mzima wa Mungu, na Shetani ni mlengwa wa uharibifu, adui. Unaweza kuhisi kuwa haujafanya kitu chochote, lakini kwa sababu ya mabadiliko katika tabia yako, umekuwa na ushuhuda, na ushuhuda huu unaelekezwa kwa Shetani na haufanywi kwa mwanadamu. Mwanadamu hajafaa ili afurahie ushuhuda kama huu. Je, jinsi gani yeye ataweza kuelewa kazi inayofanywa na Mungu? Mlengwa wa vita vya Mungu ni Shetani; mwanadamu, wakati huo huo, ni mlengwa wa wokovu. Mwanadamu ana tabia potovu ya kishetani, na hana uwezo wa kuelewa kazi hii. Hii ni kwa sababu ya kupotoshwa na Shetani. Sio kwa asili ya ndani ya mtu, bali inaelekezwa na Shetani. Leo, kazi kuu ya Mungu ni kumshinda Shetani, yaani, kumshinda mwanadamu kabisa, ili kwamba mwanadamu awe na ushuhuda wa mwisho wa Mungu mbele ya Shetani. Kwa njia hii, mambo yote yatatimika. Kwa matukio mengi, kwa macho yako pekee inaonekana kwamba hakuna chochote ambacho kimefanyika, lakini kwa kweli, kazi tayari imekamilika. Mwanadamu anahitaji kwamba kazi yote iliyokamilika iwe ya kuonekana, bali bila kuifanya inayoonekana wazi kwako, Nimemaliza kazi yangu, kwa kuwa Shetani ametii, ambayo ina maana kuwa yeye ameshindwa kabisa, ya kuwa busara yote ya Mungu, nguvu na mamlaka yamemshinda Shetani. Huu ndiyo ushuhuda mahsusi ambao ni lazima mtu awe nao, na ingawa haijidhihirishi kwa uwazi katika mwanadamu, ingawa haionekani kwa macho pekee, Shetani tayari ameshindwa. Ujumla wa kazi hii lazima uelekezwe dhidi ya Shetani, na inafanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Shetani. Kwa hivyo, kuna mambo mengi ambayo mwanadamu haoni kuwa ni mafanikio, lakini ambayo, machoni pa Mungu, yalikuwa na mafanikio kwa muda mrefu uliopita. Hii ni moja ya ukweli wa ndani wa kazi yote ya Mungu.
Tanbihi:
a. Maandishi ya asilia yanasoma "leo, ni kwa sababu."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni