Smiley face

Jumatano, 11 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza)


Ukamilifu wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova bado hakuwa amepanga hatua ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; hatua ya pili ya kazi, ile ya neema; au hatua ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kutokana na hili Angeweza kuushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi Yake yote ilifanywa bila kupangwa. Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima ya usimamizi wa miaka elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, Hakuwa ameandika mpango kama huo kama Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Binadamu kabla ya kuumba ulimwengu. Katika kazi ya Mungu, Anaonyesha moja kwa moja kile Alicho; Hapigi bongo kuunda mpango. Bila shaka, manabii wengi wameongea unabii mwingi, lakini bado haiwezi kusemekana kwamba kazi ya Mungu siku zote imekuwa ya upangaji mpango dhahiri; unabii ulitolewa kulingana na kazi halisi ya Mungu. Kazi Zake zote ni kazi halisi zaidi. Hutekeleza kazi Yake kulingana na maendeleo ya nyakati, na Anatekeleza kazi Yake nyingi zaidi halisi kulingana na mabadiliko ya mambo. Kwake Yeye, kutekeleza kazi ni sawa na kutoa dawa kwa ugonjwa; Anaangalia wakati akifanya kazi Yake; Anafanya kazi kulingana na kuangalia Kwake. Katika kila hatua ya kazi Yake, Anaweza kuonyesha hekima Yake ya kutosha na kuelezea uwezo Wake wa kutosha; Anafichua hekima Yake ya kutosha na mamlaka Yake ya kutosha kulingana na kazi ya enzi hiyo husika na kuruhusu yeyote kati ya watu waliorudishwa na Yeye wakati wa enzi hizo kuweza kuiona tabia Yake nzima. Anawaruzuku watu na kutekeleza kazi Anayofaa kufanya kulingana na kazi ambayo lazima ifanywe katika kila enzi; Anawaruzuku watu kulingana na kiwango ambacho Shetani amewapotosha. Ilikuwa namna hii wakati Yehova aliwaumba Adamu na Hawa mwanzoni ili kuwaruhusu kumdhihirisha Mungu katika dunia na kuwa na mashahidi wa Mungu miongoni mwa uumbaji, lakini Hawa alitenda dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka; Adamu alifanya vivyo hivyo, na kwa pamoja wakiwa kwenye bustani wakalila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na hivyo basi, Yehova alikuwa na kazi ya ziada ya kutenda miongoni mwao. Aliuona uchi wao na kuifunika mili yao kwa nguo ziliyotengenezwa kutoka kwa ngozi za wanyama. Kufuatia haya, Alimwambia Adamu “Kwa sababu umesikiliza sauti ya mkeo, na umekula kutoka kwa mti ule, ambao Nilikuamuru, nikisema, usile kutoka kwa mti huo: udongo umelaaniwa kwa sababu yako … mpaka urudi udongoni, kwani ulitolewa hapo: kwa kuwa wewe ni mavumbi, na utarudi mavumbini.” Kwa mwanamke Akasema, “Nitazidisha sana sikitiko lako na kupata kwako watoto; utazaa watoto kwa sikitiko; na ashiki yako itakuwa kwa mume wako, na atatawala juu yako.” Kuanzia hapo kuendelea aliwafukuza kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuwafanya waishi nje ya bustani, kama vile binadamu wa kisasa afanyavyo duniani. Mungu alipomwumba mwanadamu mwanzoni kabisa, Hakupanga kumfanya binadamu ajaribiwe na nyoka baada ya kuumbwa na kisha kuwalaani binadamu na nyoka. Kwa hakika hakuwa na mpango wa aina hii; ilikuwa tu maendeleo ya mambo yaliyompa kazi hii mpya miongoni mwa uumbaji Wake. Baada ya Yehova kutekeleza kazi Yake miongoni mwa Adamu na Hawa kwenye ardhi, binadamu waliendelea kuimarika kwa miaka elfu kadhaa mpaka “Yehova aliona kwamba uovu wa mwanadamu ulikuwa mkubwa ulimwenguni, na kuwa kila wazo la fikira za moyo wake lilikuwa ovu tu daima. Na Yehova akajuta kwamba alikuwa amemwumba mwanadamu ulimwenguni, na akawa na huzuni moyoni mwake. ... Lakini Nuhu alipata neema katika macho ya Yehova.” Wakati huu Yehova alikuwa na kazi mpya zaidi, kwa ajili binadamu Aliowaumba walikuwa wamezidisha dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka. Kwa mujibu wa hali hizi, Yehova aliichagua familia ya Nuhu kutoka miongoni mwa watu hawa na kuwanusuru, na kutekeleza kazi Yake ya kuuangamiza ulimwengu kwa gharika. Binadamu wameendelea kukua kwa njia hii mpaka siku ya leo, wakiendelea kupotoka kwa kukithiri, na wakati maendeleo ya binadamu yafikapo kilele, utakuwa ndio mwisho wa binadamu. Kuanzia mwanzo kabisa hadi mwisho wa ulimwengu, ukweli wa ndani wa kazi Yake siku zote umekuwa hivi. Ni sawa na namna ambavyo binadamu atakavyoainishwa kulingana na aina yake; mbali na kila mtu anayeamuliwa kabla kwa kikundi kinachomfaa mwanzoni kabisa, watu wanaainishwa kwa polepole baada ya kupitia mchakato wa maendeleo. Mwishowe, yeyote ambaye hawezi kuokolewa kwa ukamilifu atarudishwa kwa mababu zake. Hamna kati ya kazi za Mungu miongoni mwa binadamu iliyokuwa tayari imetayarishwa wakati wa uumbaji wa ulimwengu; badala yake, ilikuwa ni maendeleo ya mambo yaliyomruhusu Mungu kutekeleza kazi Yake hatua kwa hatua kwa uhalisia zaidi na kwa kimatendo zaidi miongoni mwa binadamu. Hivi ni kama ambavyo Yehova Mungu hakumwumba nyoka ili kumjaribu mwanamke. Haukuwa mpango Wake mahususi, wala halikuwa jambo ambalo Alikuwa ameliamua kimakusudi kabla; mtu anaweza kusema kwamba hili halikutarajiwa. Hivyo basi ilikuwa ni kwa sababu ya hili ndiyo Yehova aliwatimua Adamu na Hawa kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuapa kutowahi kumwumba binadamu tena. Lakini hekima ya Mungu inagunduliwa tu na watu kwenye msingi huu, kama tu ile hoja Niliyotaja awali: “Hekima Yangu hutumika kutokana na njama za Shetani.” Haikujalisha ni vipi ambavyo binadamu walizidi kupotoka au vipi nyoka alivyowajaribu, Yehova bado alikuwa na hekima Yake; kwa hivyo, Amekuwa Akijihusisha katika kazi mpya tangu Alipouumba ulimwengu, na hamna hatua zozote za kazi hii zimewahi kurudiwa. Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; binadamu wamekuwa wakipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa. Baada ya binadamu kupotoshwa na Shetani, Aliendelea siku zote kufanya kazi miongoni mwa watu ili kumshinda adui Wake anayewapotosha binadamu. Vita hivi vitaendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajaruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu waovu na kuwatuza wema. Amepambana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo mbali na kufanya tu kila kitu mbinguni kitii mamlaka Yake; pia Hufanya kila kitu duniani kipumzike chini ya kigonda Chake, na pia Huwafanya wale watenda maovu wanaoshambulia na kunyanyasa binadamu wajipate katika kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake. Alikuwa hajawahi kufichua hekima Yake kabla ya uwepo wa binadamu, kwani Hakuwa na maadui kule mbinguni, juu ya dunia, au kwenye ulimwengu kwa ujumla, na hakukuwa na nguvu za giza zilizoshambulia chochote katika maumbile. Baada ya malaika mkuu kumsaliti, Aliwaumba binadamu kwenye dunia, na ilikuwa ni kwa sababu ya binadamu ndiyo Alianza rasmi vita Vyake vya milenia nzima dhidi ya Shetani, malaika mkuu, vita ambavyo vilizidi kushamiri kwa kila hatua iliyopigwa. Uweza Wake na hekima vinapatikana katika kila mojawapo ya awamu hizi. Ni katika muda huu tu ndipo kila kitu kule mbinguni na duniani huweza kushuhudia hekima ya Mungu, uweza Wake, na hasa uhalisi wa Mungu. Angali anatekeleza kazi Yake kwa njia ile ya kihalisi leo; aidha, Anapoendelea kutekeleza kazi Yake anafichua pia uweza Wake na hekima Yake; Anawaruhusu kuona ule ukweli wa ndani katika kila hatua ya kazi, kuona hasa ni vipi mnaweza kuelezea uweza wa Mungu na hasa ni vipi mnavyoweza kuelezea uhalisia wa Mungu.

Je, watu hawaamini kwamba ilitabiriwa awali kabla ya uumbaji kwamba Yuda angemwuza Yesu? Kwa hakika, Roho Mtakatifu alikuwa amepanga haya kulingana na uhalisi wakati huo. Ilitukia tu kwamba kulikuwepo mtu kwa jina la Yuda ambaye siku zote angebadhiri fedha. Hivyo basi alichaguliwa kutekeleza wajibu huu na kuwa mwenye huduma katika njia hii. Huu ni mfano halisi wa kutumia rasilimali za mahali palepale. Yesu hakujua hili kwanza; Alilijua hili tu Yuda alipolifichuliwa baadaye. Kama mtu mwingine angeweza kutekeleza wajibu huu, basi mtu mwingine angeweza kufanya hivi badala ya Yuda. Kile ambacho kiliamuliwa awali kiliweza hasa kufanywa wakati mmoja na Roho Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu siku zote inafanywa kwa hiari; wakati wowote Anapopanga kazi Yake, Roho Mtakatifu ataitekeleza. Kwa nini sikuzote Nasema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni ya uhalisi? Kwamba siku zote ni mpya na haijawahi kuwa zee, na siku zote inakuwa na uhai zaidi? Kazi ya Mungu bado haikuwa imepangwa wakati ulimwengu ulipoumbwa; hivi sivyo kamwe ilivyofanyika! Kila hatua ya kazi hufikia athari yake bora kwa wakati wake mwafaka, nazo haziingiliani kati. Kunao wakati mwingi ambapo mipango katika akili zako hazilingani kamwe na kazi ya hivi punde ya Roho Mtakatifu. Kazi Yake si rahisi kama wanavyofikiria watu, wala si ngumu kama watu wengi wanavyofikiria; inajumuisha kuwaruzuku watu wakati wowote na mahali popote kulingana na mahitaji yao ya sasa. Hakuna aliye wazi zaidi kuhusu kiini halisi cha watu kama Yeye, na ni kwa sababu hii mahususi ndiposa hakuna kinachoweza kufaa mahitaji ya kihalisi ya watu kama vile ambavyo kazi Yake inavyofanya. Hivyo basi, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kazi Yake ilipangiwa milenia kadha mbele. Anavyofanya kazi miongoni mwenu sasa, kulingana na hali yenu, Yeye pia Anafanya kazi na kuongea wakati wowote na mahali popote. Wakati watu wako katika hali fulani, Yeye huongea maneno hayo ambayo hasa ndiyo wanayohitaji ndani yao. Ni kama hatua ya kwanza ya kazi Yake ya nyakati za kuadibu. Baada ya nyakati za kuadibu, watu walionyesha tabia fulani, walikuwa na mienendo ya kuasi katika njia fulani, hali fulani nzuri ziliibuka, hali fulani hasi pia ziliibuka, na mipaka ya juu ya uhasi huu ikafikia kiwango fulani. Mungu alifanya kazi Yake kwa msingi wa mambo haya yote, na hivyo basi Alichukua haya yote ili kuweza kutimiza athari bora zaidi kwa ajili ya kazi Yake. Anatekeleza tu kazi Yake ya kuruzuku miongoni mwa watu kulingana na hali zao za sasa. Yeye Hutekeleza kila hatua ya kazi Yake kulingana na hali halisi za watu. Viumbe wote wamo mikononi Mwake; Angekosa kuujua? Kwa mujibu wa hali za watu, Mungu hutekeleza hatua inayofuata ya kazi inayofaa kufanywa, wakati na mahali popote. Kazi hii haikupangwa maelfu ya miaka kabla; hii ni dhana ya kibinadamu tu! Yeye hufanya kazi huku akiangalia athari za kazi Yake, na kazi Yake inaendelea kuwa ya kina na kukua; Anapoendelea kuangalia matokeo ya kazi Yake, Anatekeleza hatua inayofuata ya kazi Yake. Yeye hutumia mambo mengi ili kuingia kwenye mpito hatua kwa hatua na kufanya kazi Yake mpya kuonekana na watu baada ya muda. Aina hii ya kazi inaweza kuruzuku mahitaji ya watu, kwani Mungu anawajua watu vizuri mno. Hivi ndivyo Anavyotekeleza kazi Yake kutoka mbinguni. Vilevile, Mungu mwenye mwili anafanya kazi Yake kwa njia iyo hiyo, Akipangilia kulingana na uhalisi na kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Hakuna yoyote kati ya kazi Zake iliyopangwa kabla ya ulimwengu kuumbwa, wala kupangwa kwa umakinifu kabla ya wakati. Miaka 2,000 baada ya ulimwengu kuumbwa, Yehova aliona binadamu walikuwa wamepotoka sana kiasi cha kwamba Alikitumia kinywa cha nabii Isaya kutabiri kwamba baada ya Enzi ya Sheria kukamilika, Angetekeleza kazi Yake ya kukomboa binadamu katika Enzi ya Neema. Huu ulikuwa mpango wa Yehova, bila shaka, lakini mpango huu pia kufanywa kulingana na hali ambazo Aliangalia wakati huo; bila shaka Yeye hakuufikiria mara moja baada ya kumwumba Adamu. Isaya alitabiri tu, lakini Yehova hakufanya matayarisho mara moja wakati wa Enzi ya Sheria; badala yake, Alianza kazi hii katika mwanzo wa Enzi ya Neema, wakati mjumbe alipojitokeza katika ndoto ya Yusufu na kumpa yeye nuru, akimwambia kwamba Mungu angekuwa mwili, na hivyo kazi Yake ya kupata mwili ikaanza. Kama watu wanavyofikiria Mungu hakujitayarishia kazi Yake ya kuwa mwili baada ya kuumba ulimwengu; jambo hili liliamuliwa tu kulingana na kiwango cha maendeleo ya binadamu na hadhi ya vita Vyake na Shetani.

Mungu anapokuwa mwili, Roho Wake anamshukia binadamu; kwa maneno mengine, Roho wa Mungu anauvaa mwili. Anafanya kazi Yake duniani, na badala ya kuleta naye hatua mbalimbali zilizozuiliwa, kazi hii haina mipaka kamwe. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya katika mwili bado inaamuliwa na athari ya kazi Yake, na Yeye hutumia mambo haya kuamua urefu wa muda ambao Atafanya kazi akiwa katika mwili. Roho Mtakatifu hufichua moja kwa moja kila hatua ya kazi Yake; Yeye huchunguza kazi Yake anapozidi kuendelea; si jambo la kimwujiza kiasi cha kupanua ile mipaka ya kufikiriwa na binadamu. Hii ni kama kazi ya Yehova katika kuumba mbingu na nchi na vitu vyote; Aliweza kupanga na kufanya kazi wakati huo huo. Alitenga nuru kutoka kwenye giza, na asubuhi pamoja na jioni vyote vikawepo—hii ilichukua siku moja. Siku ya pili Aliumba mbingu, ambayo pia ilichukua siku moja na kisha Akaiumba nchi, bahari na viumbe vilivyojaa ndani, pia ikichukua siku nyingine moja. Hili liliendelea hivyo hadi siku ya sita, wakati Mungu alipomwumba binadamu na kumwacha asimamie viumbe hivi vyote juu ya nchi, mpaka siku ya saba, Alipokuwa amemaliza kuumba viumbe vyote, na akapumzika. Mungu alibariki siku ya saba na kuitenga kuwa siku takatifu. Aliiamulia siku hii takatifu baada ya kuviumba viumbe vyote, na wala si kabla ya kuviumba. Kazi hii pia ilitekelezwa kwa hiari; kabla ya kuviumba viumbe vyote, Hakuamua kuumba ulimwengu kwa siku sita na kupumzika siku ya saba; ukweli hauko hivi hata kidogo. Hakusema hili, wala Hakupanga hili. Kwa vyovyote vile Hakusema kwamba uumbaji wa viumbe vyote ungekamilishwa katika siku ya sita na kwamba Angepumzika katika siku ya saba; badala yake, Aliumba kulingana na kile kilichokuwa kikionekana kizuri Kwake. Punde Alipomaliza kuumba kila kitu, tayari ilikuwa ni siku ya sita. Kama ingekuwa ni siku ya tano Alipomaliza kuumba kila kitu, Angepangilia basi siku ya sita kuwa siku takatifu; hata hivyo, Alimaliza kuumba kila kitu katika siku ya sita, na hivyo basi siku ya saba ikawa siku takatifu, ambayo imeenezwa hadi siku ya leo. Hivyo basi, kazi Yake ya sasa inatekelezwa kwa njia ii hii. Yeye huongea na kuwaruzuku kulingana na hali zenu. Yaani, Roho huongea na kufanya kazi kulingana na hali za watu; Roho huangalia kila kitu na kufanya kazi wakati wowote na mahali popote. Kile Ninachofanya, kwa mfano, kuwawekea na kuwapa bila kiwazo ni kile mnachohitaji. Ndiyo maana Nasema kwamba hakuna kazi Yangu iliyo tofauti na uhalisi; yote ni halisi, kwani nyinyi nyote mnajua ya kwamba “Roho wa Mungu hulinda vyote.” Kama haya yote yalikuwa yameamuliwa kabla ya wakati, huoni kwamba mambo yangekuwa yamekwisha amuliwa? Unafikiri kwamba Mungu alifanya kazi kwa milenia sita nzima na kisha kuamulia kabla binadamu kama waasi, wapingaji, waongo na wadanganyifu, kama kuwa na mwili, tabia za kishetani zilizopotoka, ashiki za macho na kujihusisha kwao kwa mambo yasiyofaa. Haya yote hayakupangwa kabla, lakini yalitokana na upotoshaji wa Shetani. Baadhi watasema, “Shetani naye hakuwa ndani ya mfumbato wa Mungu? Mungu alikuwa amepanga awali kwamba Shetani angepotosha binadamu kwa njia hii, na baada ya hapo Akatekeleza kazi Yake miongoni mwa binadamu.” Je, Mungu kwa kweli angepanga awali Shetani kuwapotosha binadamu? Anayo hamu mno ya kuwaruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida na kibinadamu; Angenyanyasa maisha ya binadamu? Basi kumshinda Shetani na kuokoa binadamu si kungekuwa jitihada za bure bilashi? Je, uasi wa binadamu ungeamuliwaje kabla? Ulitokana na kunyanyaswa na Shetani kwa hali halisi; ungepangwa vipi awali na Mungu? Shetani aliye ndani ya mfumbato wa Mungu ambaye mnamwelewa na Shetani ndani ya mfumbato wa Mungu ambaye Ninamzungumzia ni tofauti sana. Kulingana na kauli zenu kwamba “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake,” Shetani asingemsaliti Yeye. Je, wewe hujasema kwamba Mungu ni mwenyezi? Maarifa yenu ni ya kidhahania mno na hayaambatani na uhalisi; hayaeleweki wala hayana urazini na hayafanyi kazi! Mungu ni mwenyezi; huu si uwongo kamwe. Malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa sababu Mungu alimpa sehemu ya mamlaka awali. Bila shaka, tukio hili halikutarajiwa, kama vile Hawa kushindwa na jaribio la nyoka. Hata hivyo, bila kujali ni vipi ambavyo Shetani hutekeleza usaliti wake, tofauti na Mungu, yeye si mwenyezi. Kama vile mlivyosema, Shetani ni mwenye nguvu; haijalishi ni nini atakachofanya, mamlaka ya Mungu humshinda siku zote. Hii ndiyo maana ya kweli katika ule msemo “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake.” Hivyo basi, vita Vyake na Shetani lazima vitekelezwe hatua moja baada ya nyingine; aidha, Yeye hupanga kazi Yake katika kuitikia ujanja wa Shetani. Hivi ni kusema, kulingana na enzi, Anawaokoa watu na kufichua hekima na uweza Wake. Vilevile, kazi katika siku za mwisho haikuamuliwa awali kabla ya Enzi ya Neema; haikuamuliwa awali katika mpangilio unaofuatana kama huu: Kwanza, kuifanya tabia ya nje ya binadamu ibadilike; pili, kumfanya binadamu apokee kuadibu na majaribio yake; tatu, kumfanya binadamu apitie kifo; nne, kumfana binadamu apitie nyakati za kumpenda Mungu na aonyeshe uamuzi wa kiumbe kilichoumbwa; tano, kumfanya binadamu ayaone mapenzi ya Mungu na kumjua Mungu kabisa, kisha kumkamilisha binadamu. Hakupanga mambo haya yote wakati wa Enzi ya Neema; badala yake, Alianza kuyapanga katika enzi ya sasa. Shetani yumo kazini, kama vile alivyo Mungu. Shetani huonyesha tabia yake potovu, huku naye Mungu huongea moja kwa moja na kufichua baadhi ya mambo muhimu. Hii ndiyo kazi inayofanywa leo, na kanuni ii hii ya kufanya kazi ilitumika zamani, baada ya ulimwengu kuumbwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni