Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yehova. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yehova. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 23 Desemba 2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)(Sehemu ya Pili)



Mwenyezi Mungu alisema, Hebu sasa tuangalie maneno na maonyesho mengine ya Shetani yanayomruhusu mwanadamu kuona uso wake wenye sura mbaya. Hebu tuendelee kusoma baadhi ya maandiko.
3. Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
(Ayu 1:6-11) Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. 

Ijumaa, 1 Desemba 2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)(Sehemu ya Nne )


Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki

Mwenyezi Mungu alisema, Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni fungu jingine lililozungumziwa na Yehova Mungu, Alisema kwa Ibrahimu, “Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.” 

Jumamosi, 28 Oktoba 2017

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli


Mwenyezi Mungu alisema: Katika matendo, amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri. Kutenda ukweli na kuzishika amri sio vitendo vinavyopingana, lakini badala yake vinahusiana.

Jumatatu, 16 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Maana ya “Mwanaadamu Halisi”


Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu huenda hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho na pia huenda hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda wale walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini, adui Yangu alipoungana katika vita na Mimi, Nilikuwa Nimeshamwambia kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kufanywa watoto wake na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake.

Jumatatu, 2 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. 

Alhamisi, 28 Septemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

  <font-size>Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi.

Jumatatu, 25 Septemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi katika Enzi ya Sheria

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kazi Katika Enzi ya Sheria


Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Ijumaa, 8 Septemba 2017

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.