Smiley face

Jumamosi, 23 Desemba 2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)(Sehemu ya Pili)



Mwenyezi Mungu alisema, Hebu sasa tuangalie maneno na maonyesho mengine ya Shetani yanayomruhusu mwanadamu kuona uso wake wenye sura mbaya. Hebu tuendelee kusoma baadhi ya maandiko.
3. Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
(Ayu 1:6-11) Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.  Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.
(Job 2:1-5) Tena kulikuwa na siku hao wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujihudhurisha mbele za BWANA. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu. Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.
Vifungu hivi viwili ni mazungumzo kati ya Mungu na Shetani, na vinarekodi kile alichosema Mungu na kile alichosema Shetani. Je, Mungu alisema mengi sana? (La.) Hakuzungumza sana, na Aliongea kwa urahisi sana. Tunaweza kuona utakatifu wa Mungu katika maneno rahisi ya Mungu? Wengine watasema “Hii si rahisi.” Hivyo tunaweza kuona ubaya wa shetani katika majibu yake? (Ndiyo.) Basi kwanza wacha tuangalie ni aina gani ya swali ambalo Yehova Mungu alimwuliza Shetani. “Umetoka wapi wewe?” Hili ni swali linaloeleweka kwa urahisi? (Ndiyo.) Kuna maana iliyofichwa? (La.) Ni swali tu, safi, bila madhumuni mengine. Kama Ningekuuliza: “Unatoka wapi wewe?” mngejibu vipi? Ni swali gumu kujibu? Mngesema: “Natoka katika kuzunguka-zunguka, na katika kutembea huku na huku?” (La.) Hamngejibu namna hii, kwa hivyo mnahisi aje mnapomwona Shetani akijibu kwa njia hii? (Tunahisi kwamba Shetani ni mpumbavu na mjanja.) Mnahisi hivi? Unaweza kusema ni nini Ninachohisi? Kila wakati Ninapoona maneno haya Nahisi kuchukizwa. Mnahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Mbona kuchukizwa? Kwa sababu anazungumza bila kusema lolote! Alijibu swali la Mungu? (La.) Mbona? Maneno yake hayakuwa jibu, hayakuwa na matokeo yoyote, siyo? Hayakuwa jibu lililoelekezwa kwa swali la Mungu. “Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.” Niambie, unayaelewa maneno haya? Unayaelewa? Kwa hivyo Shetani ametoka wapi duniani? Mmepata jibu kuhusu wapi ametoka? (La.) Hii ndiyo “akili” ya ujanja wa Shetani, kutomwacha yeyote kujua anachosema. Baada ya kuyasikia maneno haya, bado huwezi kutambua ni nini amesema, ilhali amemaliza kujibu. Pengine anaamini kwamba amejibu vizuri sana. Basi unahisi vipi? Kuchukizwa? (Ndiyo.) Kuchukizwa, siyo? Sasa unaanza kuhisi chukizo na maneno haya, Shetani haongei moja kwa moja, kukufanya kutoweza kutambua akili yake ama chanzo cha maneno yake. Anazungumza kimakusudi, kwa ujanja, na anatawaliwa na kiini chake mwenyewe, asili yake. Shetani hakuzingatia maneno haya kwa muda mrefu; aliyaeleza kiasili. Punde tu unapomwuliza mahali ametoka, anatumia maneno haya kukujibu. “Ametoka wapi duniani? Unahisi kuchanganyikiwa, bila kujua ametoka wapi. Kuna wowote kati yenu wanaozungumza hivi? (Ndiyo.) Hii ni njia ya aina gani ya kuzungumza? (Si dhahiri na haina jibu la uhakika.) Tunapaswa kutumia aina gani ya maneno kuelezea namna hii ya kuzungumza? Ni ya kupotosha na kudanganya, siyo? Watu wengine huzungumza namna hii. Unauliza mtu: “Nilikuona jana. Ulikuwa unaelekea wapi? Hawakujibu moja kwa moja kusema mahali walienda jana. Wanasema “Jana ilikuwa siku kweli. Nimechoka sana!” Je, walijibu swali lako? Hilo si jibu ulilokuwa unataka, ni kweli? Hii ni “akili” ya ujanja wa mwanadamu. Huwezi kugundua wanachomaanisha ama kutambua chanzo ama nia nyuma ya maneno yao. Hujui mioyo yao kwa sababu ndani ya mioyo yao wanayo hadithi yao wenyewe—hii ni yenye kudhuru kwa siri. Je, ninyi pia huongea hivi mara nyingi? (Ndiyo.) Basi madhumuni yenu ni yapi? Je, huwa ni kulinda maslahi yenu wakati mwingine, kudumisha nafasi yenu wakati mwingine, taswira yenu, kuweka siri za maisha yenu ya kibinafsi, kuokoa sifa zenu binafsi? Licha ya madhumuni, hayatenganishwi na maslahi yenu, yanahusiana na maslahi yenu, sivyo? Hii ni asili ya mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo si kila mtu aliye na asili ya aina hii ni kama Shetani? Tunaweza kusema hivi, sivyo? Kuzungumza kwa ujumla, huu udhihirisho ni wenye makuruhu na wa kusinya. Mnahisi pia sasa kuchukizwa, sivyo? (Ndiyo.) Hii inawakilisha ujanja na uovu wa Shetani.
Tukiangalia tena kifungu cha kwanza, Shetani anamjibu tena Yehova, akisema: “Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?” Anaanza kushambulia tathmini ya Yehova ya Ayubu, na shambulio hili linapakwa rangi na uhasama. “Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo?” Huu ndio utambulisho na tathmini ya Shetani ya kazi ya Yehova kwa Ayubu. Shetani anaitathmini hivi, akisema: “Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.” Shetani huongea kwa utata kila mara, lakini hapa anaongea kwa uhakika. Maneno haya yaliyozungumzwa kwa uhakika ni shambulio, ni kufuru na ni upinzani kwa Yehova Mungu, kwa Mungu Mwenyewe. Mnahisi vipi mnapomsikia? Mnahisi chuki? (Ndiyo.) Mnaweza kuona nia zake? Kwanza kabisa, anakataa kabisa tathmini ya Yehova ya Ayubu—yule anayemwogopa Mungu na kuepuka maovu. Kisha anakataa kabisa kila kitu anachosema na kufanya Ayubu kwa kumcha Yehova. Je, yeye anashitaki? Shetani anashitaki, anakataa na anashuku kila anachofanya na kusema Yehova. Haamini, akisema “Ukisema mambo yako namna hii, mbona sijaiona? Umempa baraka nyingi, anawezaje kukosa kukucha?” Je, huku si kukataa kabisa kila anachofanya Mungu? Kushitaki, kukataa, kufuru—maneno yake si ya ugomvi? Ni maonyesho ya ukweli ya kile anachofikiria Shetani ndani ya moyo wake? (Ndiyo.) Haya maneno hakika si sawa na maneno tuliyoyasoma hivi sasa: “katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Ni tofauti sana na hayo. Kupitia maneno haya, Shetani anaweka wazi mtazamo wake kwa Mungu na kuchukizwa na kumcha Mungu kwa Ayubu ambako kuko katika moyo wake. Haya yakifanyika, ubaya wake na asili yake mbovu inafichuliwa kabisa. Anawachukia wale wanaomcha Mungu, anawachukia wale wanaoepukana na maovu, na hata zaidi anamchukia Yehova kwa sababu ya kumpa mwanadamu baraka. Anataka kutumia fursa hii kumwangamiza Ayubu ambaye Mungu
alimwinua na mkono Wake mwenyewe, kumtilifisha, akisema: “Unasema Ayubu anakuogopa na kuepukana na maovu. Naiona vingine.” Anatumia mbinu mbalimbali kumchochea na kumjaribu Yehova, na kutumia mbinu mbalimbali ili Yehova Mungu amkabidhi Ayubu kwa Shetani ili atawaliwe, adhuriwe na ashughulikiwe kwa ukatili. Anataka kutumia fursa hii ili kumwangamiza mtu huyu ambaye ni mwenye haki na mtimilifu katika macho ya Mungu. Yeye kuwa na moyo wa aina hii ni msukumo wa muda mfupi? La, siyo. Imekuwa ikiundwa kwa muda mrefu. Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini? Hataki Mungu awe na mtu yeyote; anataka wale wote ambao Mungu anataka, kuwamiliki, kuwatawala, kuwaelekeza ili wamwabudu, ili watende maovu pamoja naye. Je, hii siyo nia ya husuda ya Shetani? Kwa kawaida, ninyi husema mara nyingi kwamba Shetani ni mwovu sana, mbaya sana, lakini umemwona? Mnaweza kuona tu jinsi ambavyo mwanadamu ni mbaya na hamjaona kwa uhakika jinsi ambavyo Shetani ni mbaya sana. Lakini mmemwona kwa hili swala linalohusiana na Ayubu? (Ndiyo.) Swala hili limeufanya uso wenye sura mbaya wa Shetani na kiini chake kuwa wazi kabisa. Shetani ako vitani na Mungu, akifuata nyuma Yake. Lengo lake ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka Kufanya, kuwamiliki na kudhibiti wale wote ambao Mungu anawataka, kuwafisha kabisa wale ambao Mungu anataka. Kama hawajafishwa, basi wanakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake. Na Mungu anafanya nini? Mungu anasema tu sentensi rahisi katika kifungu hiki; hakuna rekodi ya chochote zaidi ambacho Mungu anafanya, lakini tunaona kwamba kuna rekodi nyingi zaidi za kile ambacho Shetani anafanya na kusema. Katika kifungu cha maandishi hapa chini, Yehova alimwuliza Shetani, “Umetoka wapi wewe?” Jibu la Shetani ni nini? (Bado ni “Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.”) Bado ni sentensi hiyo. Niambieni, imekuwaje wito wa Shetani, kazi ya Shetani ya ujuzi wa juu? Si Shetani ni wa kuchukia? Kusema sentensi hii inayochafua moyo mara moja inatosha. Kwa nini Shetani daima anarejelea Sentensi hii? Hii inadhihirisha kitu kimoja: asili ya Shetani haibadiliki. Uso wake wenye sura mbaya si kitu anachoweza kuficha kwa muda mrefu. Mungu anamwuliza swali na anajibu kwa njia kama hiyo, sembuse anavyotendea watu! Hamwogopi Mungu, hamchi Mungu, na hamtii Mungu. Hivyo anathubutu kuwa na kiburi isiyo na maadili mbele ya Mungu, kutumia haya maneno ili kujaribu kuficha kwa maswali ya Mungu, kutumia jibu hili moja kujibu swali la Mungu, kujaribu kutumia jibu hili kumshangaza Mungu—huu ndio uso usiopendeza wa Shetani. Haamini uweza wa Mungu, haamini mamlaka ya Mungu, na hakika hayuko tayari kutii kutawaliwa na Mungu. Daima anampinga Mungu, daima anashambulia yote anayofanya Mungu, akijaribu kuharibu yote anayofanya Mungu—hili ndilo lengo lake ovu.
Katika mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita, hasa katika kitabu cha Ayubu, vifungu hivi viwili ambavyo Shetani anasema na mambo ambayo Shetani anafanya yanawakilisha upinzani wake kwa Mungu. Tunaweza kusema hivi? (Ndiyo.) Huyu ni Shetani akidhihirisha alivyo kwa kweli. Umeyaona matendo ya Shetani katika maisha tunayoishi sasa? Utakapoyaona, unaweza kutoyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na Shetani, lakini badala yake kuyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na mwanadamu, siyo? Kipi kilichowakilishwa, wakati mambo kama hayo yanazungumzwa na mwanadamu? Shetani anawakilishwa? Hata kama utamtambua, bado huwezi kuona kwamba ukweli yanazungumzwa na Shetani. Lakini hapa na sasa umeona bila shaka kile ambacho Shetani mwenyewe amesema. Sasa una uelewa usio na shaka na ulio wazi kabisa wa uso wenye sura mbaya na uovu wa Shetani. Hivyo hivi vifungu viwili vilivyozungumzwa na Shetani ni vya thamani kwa watu wa leo kuweza kutambua asili ya Shetani? Hivi vifungu viwili vinastahili kukusanywa ili binadamu leo aweze kutambua uso wenye sura mbaya wa Shetani, kutambua uso wa asili na wa kweli wa Shetani? Ingawa kusema jambo hili hakuonekani kufaa sana, kulieleza kwa njia hii bado kunaweza kuchukuliwa kuwa sahihi. Naweza tu kuliweka kwa njia hii na iwapo mnalielewa, basi imetosha. Tena na tena, Shetani anayashambulia mambo ambayo Yehova anafanya, akitoa mashtaka kuhusu kumcha Yehova Mungu kwa Ayubu. Anajaribu kumchochea Yehova kwa kutumia mbinu mbalimbali, kumfanya Yehova kumkubali kumjaribu Ayubu. Maneno yake basi yanachochea sana. Basi Niambieni, baada ya Shetani kuzungumza maneno haya, Mungu anaweza kuona wazi kile ambacho Shetani anataka kufanya? (Ndiyo.) Je, Mungu anaelewa kile anataka kufanya? (Ndiyo.) Katika moyo wa Mungu, huyu mtu Ayubu ambaye Mungu anamwangalia—huyu mtumishi wa Mungu, ambaye Mungu anamchukulia kuwa mwenye haki, mtu mtimilifu—Ayubu anaweza kuyahimili majaribio ya aina hii? (Ndiyo.) Kwa nini Mungu anasema “ndiyo” kwa uhakika kama huo? Mungu huchunguza mioyo ya binadamu daima? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anaweza kuchunguza mioyo ya binadamu? (La.) Shetani hawezi. Hata kama Shetani anaweza kuona kwamba mwanadamu ana moyo unaomcha Mungu, asili yake mbovu haiwezi kuamini kwamba utakatifu ni utakatifu, ama kwamba uchafu ni uchafu. Shetani mwovu hawezi kuthamini chochote kilicho takatifu, chenye haki ama chenye kung’aa. Shetani hawezi kuepuka kuumiza kwa kutenda kupitia asili yake, uovu wake, na kupitia mbinu hizi anazotumia. Hata kwa hatari ya yeye kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu, hasiti kumpinga Mungu kwa ukaidi—huu ni uovu, hii ni asili ya Shetani. Kwa hivyo katika kifungu hiki, Shetani anasema: “Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.” Anafikiria nini? Kumcha Mungu kwa mwanadamu ni kwa sababu mwanadamu amepata manufaa mengi kutoka kwa Mungu. Mwanadamu hupata manufaa mengi kutoka kwa Mungu, kwa hivyo wanasema Mungu ni mwema. Lakini si kwa sababu Mungu ni mwema, ni kwa sababu tu mwanadamu amepata manufaa mengi na hivyo anaweza kumcha Mungu kwa njia hii: Punde unapomnyima manufaa haya, basi anaachana na wewe. Katika asili yake mbovu, Shetani haamini kwamba moyo wa mwanadamu kwa kweli unaweza kumcha Mungu. Mbona? Kwa sababu ya asili yake mbovu hajui utakatifu ni nini, na hata chini zaidi hajui heshima ya kuogopa ni nini. Hajui ni nini kumtii Mungu, ni nini kumcha Mungu. Kwa sababu yeye mwenyewe hamchi Mungu, anafikiri, “Mwanadamu pia hawezi kumcha Mungu. Haiwezekani.” Sivyo? (Ndiyo.) Niambieni, si Shetani ni mwovu? (Ndiyo!) Shetani ni mwovu. Hivyo, isipokuwa kanisa letu, yawe ni makundi na madhehebu mbalimbali, ama makundi ya kidini na ya kijamii, hawaamini uwepo wa Mungu, hawaamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi na hawaamini kwamba kuna Mungu, hivyo wanafikiri, “Kile unachoamini si Mungu pia.” Chukua mfano wa mwanamume mzinzi. Anaangalia na kuona kila mtu mwengine akiwa mzinzi, kama alivyo yeye. Mwanadamu anayedanganya kila wakati anaangalia na kuona hakuna mtu mwanimifu, anawaona wote wakidanganya. Mtu mwovu anawaona watu wote wakiwa waovu na anataka kupigana na kila mtu anayemwona. Wale watu walio na uaminifu kidogo wanawaona wote kuwa waaminifu, na hivyo daima wanalaghaiwa, wanadanganywa, na hakuna wanachoweza kufanya kuhusu hilo. Si hii ni sahihi? Nasema mifano hii michache ili kuwafanya kuwa na uhakika zaidi: asili mbovu ya Shetani si msukumo wa muda mfupi ama kitu kinachosababishwa na mazingira yake, wala si udhihirisho wa muda ulioletwa na sababu yoyote ama usuli wowote. Sivyo kabisa! Hana namna ila kuwa hivyo! Hawezi kufanya chochote chema! Hata anaposema kitu kinachofurahisha kusikia, anakushawishi tu. Kadiri maneno yake yanavyofurahisha, yenye busara zaidi, uungwana zaidi, ndivyo nia zake za husuda zinakuwa za kijicho zaidi nyuma ya maneno haya. Umeona Shetani akiwa na uso na asili ya aina gani katika vifungu hivi viwili? (Ya kudhuru kwa siri, yenye kijicho, na mbovu.) Tabia yake ya msingi ni mbovu, hasa mbovu na yenye kijicho; yenye kijicho na mbovu.
Desemba 17, 2013
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi:  Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu,  Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni