Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu anasema, “Katika moyo wa Bwana Yesu, Alikuwa radhi kujitoa kwa ajili ya mwanadamu, kujitoa Mwenyewe. Alikuwa radhi pia kuchukua nafasi ya sadaka ya dhambi, kusulubishwa msalabani, na Alikuwa na hamu ya kukamilisha kazi hii. Alipoona hali za kusikitisha za maisha ya binadamu, Alitaka hata zaidi kukamilisha misheni Yake haraka iwezekanavyo, bila ya kuchelewa hata dakika au sekunde moja.

