Smiley face

Jumapili, 8 Oktoba 2017

Kuhusu Biblia (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kuhusu Biblia (1)


Biblia inapaswa kuangaliwaje kuhusiana na imani kwa Mungu? Hili ni swali muhimu sana. Kwa nini tunawasiliana swali hili? Kwa sababu wakati ujao utaeneza injili na kupanua kazi ya Enzi ya Ufalme, na haitoshi tu kuweza kuzungumza juu ya kazi ya Mungu leo. Ili kupanua kazi Yake, ni muhimu zaidi kwamba unakuwa na uwezo wa kubadilisha dhana za watu za dini ya kale na njia za kale za imani, na kuwaacha wakiwa wameshawishika kabisa—na kufikia katika hoja hiyo Biblia inahusishwa. 

Jumamosi, 7 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu  Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

 

Mwenyezi Mungu alisema: Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi.

Ijumaa, 6 Oktoba 2017

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. 

Alhamisi, 5 Oktoba 2017

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" (Video Rasmi ya Muziki)


Nitampenda Mungu Milele

Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako.
Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku.
Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana.
Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni,
na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.
Lakini Hujawahi kuniacha.

Jumatano, 4 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
 Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari


Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. 

Jumanne, 3 Oktoba 2017

Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea


Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. 

Jumatatu, 2 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. 

Jumapili, 1 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Je, Utatu Mtakatifu Upo?


Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.