Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu.
Jumatatu, 8 Julai 2019
Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu
Jumapili, 7 Julai 2019
Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili
Mwenyezi Mungu anasema, Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani.
Ijumaa, 5 Julai 2019
Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja
Alhamisi, 4 Julai 2019
Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini
Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao. Kwa hivyo, miongoni mwa watu hakuna mtu aliyewahi kuishi katika hali halisi, na watu wote huishi maisha yasiyo na maana.
Jumatano, 3 Julai 2019
Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa
Jumanne, 2 Julai 2019
Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane
Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oh, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu? Wanawezaje, katika mwanga, kukosa kuendeleza kazi zao? Dunia si kimya na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena.







