Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII ” Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu
Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu.
Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.) Ya pili ilikuwa ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.) Na ya tatu? (Utakatifu wa Mungu.) Tumejadili mara ngapi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, imewacha wazo kwako? (Mara mbili.) Je kuhusu tabia ya haki ya Mungu? (Mara moja.) Idadi ya safari tulizojadili utakatifu wa Mungu pengine imeacha wazo kwako, lakini maudhui mahususi tuliyojadili kila mara yamewacha wazo kwako? Katika sehemu ya kwanza “mamlaka ya Mungu,” kitu kipi kimeacha wazo wa kina sana kwako, ni sehemu gani imekuwa na matokeo makubwa kwako? (Mungu kwanza alizungumza juu ya mamlaka na nguvu ya neno la Mungu; Mungu ni mwema kama neno Lake na neno Lake litakuwa kweli. Hiki ndicho kiini kabisa cha Mungu.) (Mamlaka ya Mungu yapo katika uumbaji Wake wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Hakuna mtu anaweza kugeuza mamlaka ya Mungu. Mungu ni Mtawala wa vitu vyote na Anadhibiti vitu vyote.) (Mungu anatumia upinde wa mvua na maagano pamoja na mwanadamu.) Haya ni maudhui mahususi. Kulikuwa na kitu kingine? (Maagizo ya Mungu kwa Shetani kwamba anaweza kumjaribu Ayubu, lakini hawezi kuchukua uhai wake. Kutokana na hili tunayaona mamlaka ya neno la Mungu.)
Tazama Video: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Tazama Video: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni