Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”
Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya ndani yao ni kule tu kufanya kazi na pamoja na kupanua kile ambacho tayari kimo ndani yao.
Wawe ni manabii au binadamu wanaotumiwa na Mungu kutoka kwa enzi zilizopita, hakuna yeyote anayeweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.” “Kwani kiini cha binadamu ni tofauti na kile cha Mungu. Binadamu hawezi kamwe kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, sembuse kuwa Mungu. Kile ambacho Roho Mtakatifu anamwelekeza binadamu kuishi kwa kudhihirisha ni kulingana tu na kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu.”
Tazama Video: Neno la Mungu | "Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu"
Yaliyopendekezwa: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni