Smiley face

Ijumaa, 16 Agosti 2019

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza)


1. Tangu watu waanze kukanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi cha kazi wanayopaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na udhaifu katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho. Sio tu kwamba hamna uhakika kuhusu kile ambacho mnapaswa kuingia kwacho; bali pia ninyi ni wajinga kuhusu kazi ya Mungu.  Hili ni zaidi tu ya suala la dosari ndani yenu: Ni dosari kubwa ya wote walio katika ulimwengu wa dini. Hii ndiyo sababu kuu ya watu kutomjua Mungu, na hivyo dosari hii ni kasoro ya kawaida miongoni mwa wale wote wanaomtafuta. Hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kumjua Mungu, au amewahi kuuona uso Wake halisi. Ni kwa sababu hii ndipo kazi ya Mungu inakuwa ngumu kama kazi ya kuhamisha mlima au kukausha bahari. Ni watu wangapi ambao wametoa sadaka maisha yao kwa ajili ya kazi ya Mungu; ni wangapi wametengwa kwa sababu ya kazi Yake; ni wangapi wameteswa hadi kufa kwa ajili ya kazi Yake; ni wangapi wamelia kwa ajili ya upendo wao kwa Mungu, wamekufa pasipo haki; ni wangapi wamekutana na mateso katili na ya kinyama…? Kwamba majanga haya yanapita–yote sio kwa sababu ya watu kutokuwa na maarifa juu ya Mungu? Inawezekanaje mtu ambaye hamjui Mungu awe na ujasiri wa kusimama mbele Yake? Inawezekanaje mtu anayemwamini Mungu na bado anamtesa awe na ujasiri wa kusimama mbele Yake? Hizi si dosari za wale waliopo katika ulimwengu wa kidini pekee, bali ni dosari za kawaida kwenu na kwao. Watu wanamwamini Mungu bila kumfahamu; ni kwa sababu hii pekee ndio watu hawamheshimu Mungu kutoka mioyoni mwao, na hawamchi Yeye mioyoni mwao. Hata kuna wale ambao, kwa majivuno makuu na hali, wanafanya kazi ambayo wanafikiria kichwani wenyewe katika mkondo huu, na wanaifanya kazi ya Mungu kulingana na matakwa yao wenyewe na tamaa zao za kibadhirifu. Watu wengi wanatenda ovyoovyo, hawamheshimu Mungu bali wanafuata mapenzi yao wenyewe. Je, hii si mifano mizuri ya mioyo ya watu yenye ubinafsi? Je, haya hayaonyeshi dalili nyingi zaidi za udanganyifu walio nao watu?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Kwa kweli watu wanaweza kuwa wenye akili sana, lakini inawezekanaje karama zao zichukue nafasi ya kazi ya Mungu? Kwa kweli watu wanaweza kuujali mzigo wa Mungu, lakini hawawezi kufanya mambo kwa ubinafsi sana. Je, matendo ya watu ni ya kiungu kweli? Je, mtu yeyote anaweza kuhakikishiwa vyema? Kutoa ushuhuda kuhusu Mungu kurithi utukufu Wake—huyu ni Mungu akifanya jambo la pekee na kuwainua watu; wangewezaje kustahili? Kazi ya Mungu ndio imeanza tu, maneno Yake yameanza tu kuzungumzwa. Katika hatua hii, watu wanajigamba; hii haiwezi kuwa ni kujitafutia fedheha? Wanaelewa kidogo sana. Hata mwanafalsafa mwenye karama ya juu sana, mzungumzaji mzuri kabisa, hawezi kuelezea yote kuhusu utele wa Mungu—sembuse nyinyi? Ni vyema msijione wakubwa kabisa zaidi ya mbingu, lakini badala yake jioneni kuwa watu wa chini kabisa kuliko watu razini wengine wanaotafuta kumpenda Mungu. Hii ndiyo njia ambayo kwayo mnapaswa kuingia: kujiona wadogo kuliko wengine wote kwa muda. Kwa nini mjiweke katika viwango hivyo vya juu? Kwa nini mjiweke katika heshima hiyo ya juu? Katika safari ndefu ya maisha, mmepiga hatua chache tu za kwanza. Mnachokiona ni mkono wa Mungu tu, si mwili mzima wa Mungu. Ni wajibu wenu kuiona kazi ya Mungu zaidi, kugundua zaidi juu ya kile mnachopaswa kuingia kwacho, kwa sababu mmebadilika kidogo sana.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Kwa kweli, kati ya vitu vingi katika uumbaji wa Mungu, mwanadamu ni wa kiwango cha chini sana. Ingawa ni mtawala wa vitu vyote, mwanadamu ni kiumbe pekee ambaye yuko chini ya hila za Shetani, ni kiumbe pekee ambaye anashikwa kwa namna nyingi katika uharibifu wake. Mwanadamu hajawahi kuwa na ukuu juu yake mwenyewe. Watu wengi wanaishi mahali pabaya pa Shetani, na kuumizwa na dhihaka zake; anawaudhi kwa njia hii hata hapo watakapokuwa wamelemewa kabisa, wakistahimili kila badiliko, kila ugumu katika ulimwengu wa kibinadamu. Baada ya kuwachezea, Shetani hukomesha hatima yao. Na hivyo watu wanaishi maisha yao yote wakiwa na mkanganyiko, wasiwahi kufurahia hata siku moja vitu vizuri ambavyo Mungu amewaandalia, badala yake wanajeruhiwa na Shetani na kuachwa wakiwa wameharibika kabisa. Leo wamekuwa wadhoofu na walegevu sana kiasi kwamba hawana mwelekeo wa kuzingatia kazi ya Mungu. Ikiwa watu hawana mwelekeo wa kuzingatia kazi ya Mungu, uzoefu wao utabakia kusambaratika na usiokamilika milele, na kuingia kwao kutabakia sehemu tupu milele.

kutoka katika "Kazi na Kuingia(1)" katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Katika miaka elfu kadhaa tangu Mungu alipokuja duniani, idadi yoyote ya watu wenye mawazo ya kiburi wamekuwa wakitumiwa na Mungu kufanya kazi Yake kwa miaka mingi; lakini wale wanaoijua kazi Yake ni wachache sana kiasi kwamba karibu hawapo. Kwa sababu hii, idadi kubwa ya watu isiyojulikana wanachukua jukumu la kumpinga Mungu na wakati huo huo wanapoifanya kazi Yake, kwa sababu, badala ya kufanya kazi Yake, kimsingi wanafanya kazi ya kibinadamu katika nafasi waliyopewa na Mungu. Je, hii inaweza kuitwa kazi? Wanawezaje kuingia? Wanadamu wamechukua neema ya Mungu na kuizika. Kwa sababu jambo hili, kwa karne nyingi zilizopita wale wanaofanya kazi Yake wana kuingia kwa kiwango kidogo. Hawazungumzi juu ya kuijua kazi ya Mungu kwa sababu wanafahamu kidogo kuhusu hekima ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba, ingawa kuna watu wengi wanaomtumikia Mungu, wameshindwa kuona jinsi Alivyoinuliwa, na hii ndiyo sababu watu wamejifanya wao ndio Mungu wa kuabudiwa na watu.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili 

5. Kwa miaka mingi sana Mungu amebakia sirini katika uumbaji; Ameangalia katika misimu yote ya machipuko na kipupwe nyuma ya umande ufunikao; Ametazama chini kutoka katika mbingu ya tatu kwa siku nyingi sana; Ametembea miongoni mwa wanadamu kwa miezi na miaka mingi sana. Amekaa juu ya wanadamu wote Akisubiri kwa utulivu katika vipindi vingi vya baridi. Hajawahi kujionyesha wazi kwa mtu yeyote yule, wala kutoa sauti hata kidogo, Akiondoka bila ishara na kurudi kimyakimya vilevile. Nani anaweza kuujua uso wake halisi? Hajawahi kuzungumza na mwanadamu hata mara moja, Hajawahi kuonekana kwa mwanadamu hata mara moja. Ni rahisi kiasi gani kwa watu kufanya kazi ya Mungu? Wanatambua kidogo tu kwamba kumjua Yeye ni kitu kigumu sana kuliko vitu vyote. Leo Mungu amezungumza na mwanadamu, lakini mwanadamu hajawahi kumfahamu, kwa sababu kuingia kwake katika maisha ni finyu sana na hakuna kina. Kwa mtazamo Wake, watu hawastahili kabisa kuonekana mbele za Mungu. Wana ufahamu mdogo sana wa Mungu na wamejitenga mbali naye sana. Aidha, mioyo inayomwamini Mungu ni tatanishi sana, na hawana hasa taswira ya Mungu chokomeani mwa mioyo yao. Kwa hiyo, juhudi kubwa sana za Mungu, na kazi Yake, kama vipande vya dhahabu vilivyofunikwa mchangani, haviwezi kutoa mwanga. Kwa Mungu, tabia, nia, na mitazamo ya watu hawa ni machukizo sana. Wakiwa dhaifu katika uwezo wao wa kupokea, bila hisia kiasi cha kufa ganzi, waliojidharau na kuharibika tabia, wakitumikishwa kupita kiasi, dhaifu na wasiokuwa na dhamiri, ni lazima waongozwe kama ng'ombe na farasi wanavyoongozwa. Kama ilivyo kuingia kwao katika roho, au kuingia katika kazi ya Mungu, hawachukui tahadhari yoyote, hawajizatiti hata kidogo kuteseka kwa ajili ya ukweli. Haitakuwa rahisi kwa mtu kama huyu kufanywa mkamilifu na Mungu. Hivyo ni muhimu kwamba mnapanga kuingia kwenu katika pembe hii—kwamba kupitia kazi yenu na kuingia kwenu ndipo mnakaribia kuijua kazi ya Mungu.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Kazi inapozungumziwa, mwanadamu anaamini kwamba kazi ni kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu, akihubiri kila sehemu, na kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Ingawa imani hii ni sahihi, imeegemea upande mmoja sana; kile ambacho Mungu anamwomba mwanadamu si kusafiri kwenda huku na huko tu kwa ajili ya Mungu; ni zaidi kuhusu huduma na kujitoa ndani ya roho. Ndugu na dada wengi hawajawahi kufikiria juu ya kumfanyia Mungu kazi hata baada ya miaka mingi sana ya uzoefu, maana kazi kama mwanadamu anavyoielewa haipatani na ile ambayo Mungu anaitaka. Kwa hiyo, mwanadamu havutiwi kwa namna yoyote ile na kazi ya Mungu, na hii ndiyo sababu ya kuingia kwa mwanadamu pia kunaegemea upande mmoja. Nyinyi nyote mnapaswa kuanza kuingia kwa kumfanyia Mungu kazi, ili kwamba muweze kupata uzoefu zaidi wa vipengele vyake vyote. Hiki ndicho mnapaswa kuingia kwacho. Kazi haimaanishi kutembea huku na huko kwa ajili ya Mungu; maana yake ni iwapo maisha ya mwanadamu na kile ambacho mwanadamu anaishi kwa kudhihirisha ni kwa ajili ya Mungu kufurahia. Kazi inamaanisha mwanadamu kutumia uaminifu alio nao kwa Mungu na maarifa aliyo nayo juu ya Mungu ili kumshuhudia Mungu na kumhudumia mwanadamu. Huu ndio wajibu wa mwanadamu na yote ambayo mwanadamu anapaswa kutambua. Kwa maneno mengine, kuingia kwenu ni kazi yenu; mnatafuta kuingia wakati wa kazi yenu kwa ajili ya Mungu. Kupata uzoefu wa Mungu sio tu kuweza kula na kunywa neno Lake; la muhimu zaidi, mnapaswa kuweza kumshuhudia Mungu, kumtumikia Mungu, na kumhudumia na kumkimu mwanadamu. Hii ni kazi, na pia kuingia kwenu; hiki ndicho kila mwanadamu anapaswa kukitimiza.
kutoka katika "Kazi na Kuingia (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili
   
7. Kuna watu wengi wanaotilia mkazo tu katika kusafiri huku na huko kwa ajili ya Mungu, na kuhubiri kila sehemu zote, lakini hawazingatii uzoefu wao binafsi na kupuuza kuingia kwao katika maisha ya kiroho. Hiki ndicho kinawasababisha wale wanaomtumikia Mungu kuwa watu wanaompinga Mungu. Kwa miaka mingi sana, wale wanaomtumikia Mungu na kumhudumia mwanadamu wameona kufanya kazi na kuhubiri kama kuingia, na hakuna waliochukulia uzoefu wao binafsi wa kiroho kuwa kuingia muhimu. Badala yake, wanatumia nuru ya kazi ya Roho Mtakatifu kuwafundisha wengine kwa faida yao. Wanapohubiri, wanakuwa na mzigo mkubwa sana na wanapokea kazi ya Roho Mtakatifu, na kupitia hili wanatoa sauti ya Roho Mtakatifu. Wakati huo, wale wanaofanya kazi wanahisi wenye kiburi kana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wao binafsi wa kiroho; wanahisi kana kwamba maneno yote wanayoyazungumza wakati huo ni asili zao wenyewe…. Baada ya kuhubiri kwa namna hiyo, unahisi kwamba kimo chako halisi sio kidogo kama ulivyoamini. Baada ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yako kwa namna ile ile mara kadhaa, basi unakusudia kwamba tayari una kimo na unaamini kimakosa kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuingia kwako na asili yako binafsi. Unapopitia uzoefu huu kwa mfululizo, unakuwa mzembe kuhusu kuingia kwako mwenyewe. Halafu unakuwa mvivu bila kujua, na kutozingatia kabisa kuingia kwako mwenyewe. Kwa hiyo, unapowahudumia wengine, unapaswa kutofautisha waziwazi kati ya kimo chako na kazi ya Roho Mtakatifu. Hii itasaidia zaidi kuingia kwako na kuunufaisha uzoefu wako vizuri zaidi. Mwanadamu kuichukulia kazi ya Roho Mtakatifu kuwa uzoefu wake binafsi ndio mwanzo wa upotovu. Hivyo, kazi yoyote mnayoifanya, mnapaswa kuzingatia kuingia kwenu kama somo muhimu.
kutoka katika "Kazi na Kuingia (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili

8. Mtu anafanya kazi ili kutimiza mapenzi ya Mungu, kuwaleta wale wote wanaoutafuta moyo wa Mungu mbele Yake, kumleta mwanadamu kwa Mungu, na kuitambulisha kazi ya Roho Mtakatifu na uongozi wa Mungu kwa mwanadamu, kwa kufanya hivyo atakuwa anayakamilisha matunda ya kazi ya Mungu. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kuelewa kiini cha kufanya kazi. Kama mtu anayetumiwa na Mungu, watu wote wanafaa kumfanyia Mungu kazi, yaani, wote wana fursa ya kutumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, kuna hoja moja mnayopaswa kuielewa: Mwanadamu anapofanya kazi ya Mungu, mwanadamu anakuwa na fursa ya kutumiwa na Mungu, lakini kile kinachosemwa na kujulikana na mwanadamu sio kimo cha mwanadamu kabisa. Mnaweza tu kujua vizuri kasoro zenu katika kazi yenu, na kupokea nuru kubwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, hivyo kuwawezesha kuingia kuzuri katika kazi yenu. Kama mwanadamu anachukulia uongozi wa Mungu kuwa ni kuingia kwake mwenyewe na kile kilicho ndani ya mwanadamu, hakuna uwezekano wa mwanadamu kuongezeka kimo. Roho Mtakatifu humpatia mwanadamu nuru anapokuwa katika hali ya kawaida; katika nyakati kama hizo, mara nyingi mwanadamu anadhani nuru anayopokea ni kimo chake mwenyewe katika uhalisia, maana Roho Mtakatifu huangazia kwa njia ya kawaida: kwa kutumia kile ambacho ni cha asili ndani ya mwanadamu. Mwanadamu anapofanya kazi na kuzungumza, au wakati mwanadamu anapofanya maombi katika shughuli zake za kiroho, ndipo ukweli utawekwa wazi kwake. Hata hivyo, katika uhalisia, kile ambacho mwanadamu anakiona ni nuru tu iliyoangaziwa na Roho Mtakatifu (kwa asili, hii inahusiana na ushirikiano kutoka kwa mwanadamu) na sio kimo halisi cha mwanadamu. Baada ya kipindi cha kupitia uzoefu ambapo mwanadamu anakabiliana na shida nyingi, kimo halisi cha mwanadamu kinadhihirika katika mazingira kama hayo. Ni wakati huo tu ndipo mwanadamu anagundua kwamba kimo cha mwanadamu sio kikubwa sana, na ubinafsi, kujitumainia nafsi, na tamaa za mwanadamu vyote vinaibuka. Ni baada tu ya mizunguko kadhaa ya uzoefu kama huo ndipo wengi wa jinsi hiyo ambao wameamshwa ndani ya roho zao wanatambua kwamba haukuwa uhalisia wao hapo nyuma, bali ni mwangaza wa muda tu kutoka kwa Roho Mtakatifu, na mwanadamu alipokea mwangaza tu. Roho Mtakatifu anapompa nuru mwanadamu ili kuuelewa ukweli, mara nyingi huwa ni kwa namna ya wazi na dhahiri, bila muktadha. Yaani, Hayajumuishi matatizo ya mwanadamu katika ufunuo huu, na badala yake Anatoa ufunuo moja kwa moja. Mwanadamu anapokabiliana na matatizo katika kuingia, basi mwanadamu anaijumuisha nuru ya Roho Mtakatifu, na huu unakuwa uzoefu halisi wa mwanadamu. … Kwa hiyo, mnapoipokea kazi ya Roho Mtakatifu, mnapaswa hasa kujikita katika kuingia kwenu wakati huo huo, kuona hasa kazi ya Roho Mtakatifu ni gani na kuingia kwenu ni kupi, na vilevile kujumuisha kazi ya Roho Mtakatifu katika kuingia kwenu, ili kwamba muweze kukalishwa vizuri naye na kuiruhusu hulka ya kazi ya Roho Mtakatifu kutenda ndani yenu. Wakati mnapitia uzoefu wenu wa kazi ya Roho Mtakatifu, mnamjua Roho Mtakatifu, vilevile nyinyi wenyewe, na katikati ya mateso makali, mnajenga uhusianao wa kawaida pamoja na Mungu, na uhusiano baina yenu na Mungu unakuwa wa karibu siku baada ya siku. Baada ya michakato mingi ya kupogolewa na kusafishwa, mnakuza upendo wa kweli kwa Mungu. Hiyo ndiyo sababu mnapaswa kutambua kwamba mateso, mapigo, na dhiki havitishi; kinachoogopesha ni kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tu lakini sio kuingia kwenu. Siku inapofika ambapo kazi ya Mungu imemalizika, mtakuwa mmefanya kazi bure; ingawa mlipitia uzoefu wa kazi ya Mungu, hamtakuwa mmemjua Roho Mtakatifu au kuwa na kuingia kwenu wenyewe. Nuru anayopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu si ya kudumisha hisia za mwanadamu; ni kufungua njia kwa ajili ya kuingia kwa mwanadamu, na vilevile kumruhusu mwanadamu kumjua Roho Mtakatifu, na kuanzia hapo anakuza moyo wa heshima na ibada kwa Mungu.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili

9. Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na pia Amezungumzia kuingia kwao kwa njia nyingi mno. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni sana, maneno mengi ya Mungu hayajaweza kukita mizizi. Kuna sababu mbalimbali za ubora huu duni wa tabia, kama vile uharibifu wafikira na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri ambazo zimeuteka moyo wa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeingia maovu mengi katika pembe za ndani kabisa za moyo wa mwanadamu; ufahamu wa juujuu wa kusoma na kuandika kwa kitamaduni, wenye takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu katika kusoma na kuandika kwa kitamaduni na, aidha, wachache sana wakipata viwango vya juu vya elimu ya kitamaduni, kiasi kwamba kimsingi watu hawajui maana ya Mungu au Roho, bali wana taswira hafifu tu na isiyoeleweka ya sura ya Mungu waliyoipata kutoka katika makabaila ya usihiri; mivuto yenye madhara ambayo maelfu ya miaka ya "roho ya kiburi ya uzalendo" iliyo ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu fikra za kikabaila ambazo kwazo watu wamefungwa na kutiwa minyororo, bila uhuru hata kidogo, bila dhamira ya kutamani au kustahimili, bila tamaa ya kufanya maendeleo badala yake wakibakia wamekaa tu na wa kurudi nyuma, wakiwa wamekita mizizi katika akili ya utumwaNa kadhalika. Sababu hizi zenye lengo zimetoa ushindi mbaya na muovu sana kwa mtazamo wa kiitikadi, maadili na tabia ya wanadamu. Ingeonekana kwamba wanadamu wanaishi katika dunia ya giza la kigaidi, na hakuna anayetafuta kuvuka mipaka, na hakuna anayefikiria kwenda katika ulimwengu ulio bora. Badala yake, wanaridhika na waliyo nayo maishani[1], kutumia siku zao kuzaa na kuwalea watoto, wakikazana, wakitoka jasho, wakifanya kazi, wakiwa na njozi ya kuwa na familia nzuri na yenye furaha, upendo wa ndoa, kuwa na watoto wanaowapenda, kuwa na furaha katika maisha yao ya uzee wanapoishi kwa kudhihirisha kwa Amani…. Kwa makumi, maelfu, makumi ya elfu ya miaka hadi leo, watu wamekuwa wakipoteza muda wao kwa njia hii, bila yeyote kubuni maisha makamilifu, wote wakiazimia tu kuuana wenyewe kwa wenyewe katika ulimwengu huu wa giza, wakishindana kupata umaarufu na utajiri, na kufanyiana njama wao kwa wao. Nani amewahi kutafuta mapenzi ya Mungu? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuzingatia kazi ya Mungu? Sehemu zote za wanadamu zilizomilikiwa na ushawishi wa giza zimekuwa asili ya mwanadamu tangu zamani, na hivyo ni vigumu sana kufanya kazi ya Mungu, na hata watu hawazingatii kile Mungu amewaaminia leo. Kwa vyovyote vile, Ninaamini kwamba watu hawatanizingatia Ninapotamka maneno haya maana kile Ninachozungumzia ni historia ya maelfu ya miaka. Kuzungumza juu ya historia kuna maanisha ukweli, aidha, kashfa zinazojulikana na wote, sasa kuna maana gani kusema kitu ambacho ni kinyume na ukweli?
kutoka katika "Kazi na Kuingia (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
10. Shughuli za kishirikina ambazo watu wanashughulika nazo ndizo Mungu anazozichukia sana, lakini watu wengi bado hawawezi kuachana nazo, wakifikiri shughuli hizi za kishirikina zinafaa kuamriwa na Mungu hata leo bado hawajaondokana nazo kabisa. Mambo kama sherehe za arusi au mahari, zawadi za pesa na dhifa na namna nyingine zinazohusiana na matukio ya furaha, vinasherehekewa; kanuni ambazo zimerithishwa, shughuli zote za kishirikina zisizokuwa na maana zinazofanywa kwa niaba ya wafu na mazishi yanayoambatana nazo: yote haya Mungu anayachukia hata zaidi na. Hata Jumapili (Sabato, kama ilivyoadhimishwa na Wayahudi) pia inachukiwa sana na Mungu; na mahusiano ya kibinadamu na mawasiliano baina ya binadamu yote yanachukiwa yanadharauliwa na kukataliwa zaidi na Mungu. Hata Sikukuu ya Machipuko na Siku ya Krismasi, ambazo zinajulikana kwa kila mtu, hazijaamriwa na Mungu, sembuse wanasesere na mapambo (mashairi, keki ya Mwaka Mpya, mafataki, kandili, zawadi za Krismasi, sherehe za Krismasi, na Ushirika Mtakatifu) maana sikukuu hizi—je, sio sanamu katika akili za watu? Kumega mkate siku ya Sabato, mvinyo, na mavazi ya kitani navyo ni sanamu hasa. Siku zote za sherehe ambazo ni maarufu sana nchini China, kama vile Siku ya kuinua Vichwa vya Joka, Sikukuu ya Mashua ya Joka, Sikukuu ya Majira ya Kati ya Kupukutika, Sikukuu ya Laba, na Siku ya Mwaka Mpya, na sikukuu katika ulimwengu wa kidini, kama vile Pasaka, Siku ya Ubatizo, na Siku ya Krismasi, zote hizi ni sherehe zisizostahili ambazo zimepangwa na kurithishwa na watu wengi tangu zama za kale hadi leo, nazo hazina ulinganifu kabisa na jamii ya binadamu aliyeiumba Mungu. Ni uwezo mkubwa wa fikra za wanadamu na dhana bunifu ambazo zimewafanya kuzirithishwa hadi leo. Zinaonekana kuwa hazina kasoro, lakini kwa kweli ni hila ambazo Shetani huwafanyia wanadamu. Kadri Shetani anavyoenea katika sehemu fulani, na ndivyo sehemu hiyo inavyorudi nyuma kimaendeleo na kuwa isiyofaa, ndivyo desturi za kishirikina zinavyokita mizizi zaidi. Vitu hivi vinawafunga watu kwa nguvu, bila kuwaachia nafasi ya kusonga. Sikukuu nyingi katika ulimwengu wa kidini zinaonekana kuonyesha uhalisia mkubwa na kuunda daraja katika kazi ya Mungu, lakini kwa kweli vifungo visivyoonekana ambavyo Shetani hutumia kuwafunga watu wasije kumjua Mungu—vyote ni hila za ujanja wa Shetani. Kwa kweli, hatua ya kazi ya Mungu inapomalizika, tayari Ameharibu zana zake na mtindo wa wakati huo, bila kuacha alama yoyote. Hata hivyo, "waumini wasalihina" wanaendelea kuabudu vitu hivyo vya kushikika; wakati ule ule wanasahau kile Alicho nacho Mungu, bila hata kukichunguza zaidi, wakionekana kujawa na upendo wa Mungu lakini kwa kweli walimtoa Yeye kwa nguvu kutoka ndani ya nyumba kitambo na kumweka Shetani mezani kwa ajili ya kumwabudu. Sanamu za Yesu, Msalaba, Maria, Ubatizo wa Yesu na Meza ya Bwana ya Mwisho—watu wanaviheshimu vitu hivi kama Mungu wa Mbinguni, na wakati huo wote wakilia kwa sauti kwa kurudiarudia "Mungu Baba." Je, hii yote sio utani? Hadi leo, misemo mingi ya kimapokeo kama hiyo matendo ambayo yamerithishwa miongoni mwa wanadamu yanamchukiza Mungu; na yanazuia kabisa njia ya kuelekea kwa Mungu na, aidha, yanasababisha vipingamizi vikubwa katika kuingia kwa wanadamu. Mbali na kiwango ambacho Shetani amemharibu mwanadamu, sehemu za ndani za mwanadamu zimejaa vitu kama vile sheria ya Witness Lee, uzoefu wa Lawrence, uchunguzi wa Watchman Nee, na kazi ya Paulo. Mungu hana namna hasa ya kufanya kazi kwa wanadamu, kwa sababu ndani yao wana ubinafsi mwingi, sheria, kanuni, taratibu, mifumo, na kadhalika, ukiongezea vitendo vya watu vya imani za kishirikina, vitu hivi vimewakamata na kuwaharibu wanadamu. Ni kana kwamba mawazo ya watu ni filamu ya kupendeza inayosimulia hadithi ya vichimbakazi ikiwa na picha zenye rangi, watu wa ajabu wakiabiri mawinguni, ni bunifu sana kiasi cha kuwasisimua watu, ikiwaacha watu wakiwa wameduwaa na kutunduwaa.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

11. Njia bora kabisa ya kubadilisha tabia ya mwanadamu ni kugeuza sehemu hizo za mwanadamu ambazo zimeharibiwa kwa sumu, ikiwasababisha watu kuanza kubadilisha kufikiri maadili yao. Kwanza kabisa, watu wanapaswa kuona waziwazi kaida zote hizi za kidini, shughuli za kidini, miaka na miezi, na sikukuu zote anazichukia Mungu. Wanapaswa kuacha kufikiri huku kwa kishirikina na kuondoa dalili zote za hulka kuelekea ushirikina zilizokita mizizi. Haya yote yanajumuishwa katika kuingia kwa mwanadamu. Mnapaswa kuelewa kwa nini Mungu anawatoa watu kutoka katika ulimwengu wa kidunia, na tena kwa nini anawaelekeza binadamu kutokana na sheria na kanuni. Hili ndilo lango ambalo kwalo mtaingia, na ingawa haina uhusiano na uzoefu wenu wa kiroho, haya ni mambo makubwa kabisa yanayozuia kuingia kwenu, yanayowazuia kumjua Mungu. Yanatengeza mtego unaowakamata watu. Watu wengi wanasoma Biblia sana na hata wanaweza kukariri mafungu mengi kutoka katika Biblia kutoka akilini. Katika kuingia kwao leo, watu bila kujua wanaitumia Biblia kupima kazi ya Mungu, kana kwamba msingi wa hatua hii katika kazi ya Mungu ni Biblia na chanzo chake ni Biblia. Kazi ya Mungu inapokuwa sambamba na Biblia, watu wanaunga mkono kazi ya Mungu kwa dhati na kumheshimu Mungu tena; kazi ya Mungu isipolingana na Biblia, watu wanakuwa na dukuduku sana kiasi cha kuhangaika, wakitafuta kutoka kwayo msingi wa kazi ya Mungu; kama kazi ya Mungu haikutajwa katika Biblia, watu watampuuza Mungu. Inaweza kusemwa kwamba, kwa mujibu wa kazi ya Mungu leo, watu wengi wanaikubali kwa hadhari sana, wanaitii kwa kuchagua, na wanaichukulia hivi hivi; kuhusu mambo yaliyopita, wanashikilia nusu na kuacha nusu. Je, huku kunaweza kuitwa kuingia? Kushikilia vitabu vya wengine kama hazina, na kuvichukulia kama ufunguo wa dhahabu wa lango la ufalme, watu hawaonyeshi kuvutiwa kabisa na kile Mungu anachowahitaji kufanya leo. Aidha, "wataalamu wengi wenye akili" wanashikilia maneno ya Mungu huku katika mkono wa kushoto na "kazi kuu" za wengine katika mkono wa kulia, kana kwamba wanataka kutafuta msingi wa maneno ya Mungu katika kazi kuu hizi ili kuthibitisha kabisa kwamba maneno ya Mungu ni sahihi, na hata kuwafafanulia wengine kwa kuyanganisha na kazi kuu, kana kwamba walikuwa wanafanya kazi. Kusema kweli, kunao "watafiti wa kisayansi" wengi miongoni mwa wanadamu ambao hawajawahi kuheshimu mafanikio makubwa ya kisayansi ya leo, mafanikio ya kisayansi yasiyo na kigezo (yaani, kazi ya Mungu, maneno ya Mungu, na njia ya kuingia kwa maisha), hivyo watu "wanajitegemea," "wakihubiri" kotekote wakitegemea uwezo wao wa kuwashawishi watu kufanya mambo, na wakilionyesha "jina zuri la Mungu" kwa maringo. Wakati ule ule, kuingia kwao kwenyewe kuko hatarini na wanaonekana hawayafuati matakwa ya Mungu kama vitu vyote vilivyoumbwa kutoka wakati huu. Ni rahisi kiasi gani kufanya kazi ya Mungu?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (3)" katika Neno Laonekana katika Mwil

12. Inaonekana kuwa watu wamekwisha amua kuacha nusu yao kwa mambo ya zamani na kuleta nusu yao kwa wakati wa leo, kutoa nusu kwa Shetani na kumpa Mungu nusu, kana kwamba hii ndiyo njia ya kutuliza dhamiri zao na kuhisi utulivu fulani. Dunia za ndani za watu zinadhuru kwa siri sana, wanaogopa sio tu kupoteza kesho bali pia wanahofia kupoteza jana, wanaogopa sana kumkosea Shetani na kumkosea Mungu wa leo, Anayeonekana kuwa ndiye na ilhali kuwa siye. Kwa sababu watu wameshindwa kukuza fikra zao na maadili vyema, wanakosa sana katika utambuzi, na hawawezi kutambua tu kung’amua kama kazi ya leo ni ile kazi ya Mungu au la. Pengine ni kwa sababu fikra za kishirikina za watu zimekita mizizi kiasi kwamba waliuweka ushirikina na ukweli, Mungu na sanamu, katika kundi moja kitambo; bila kujali kutofautisha baina ya vitu hivi, na wanaonekana kushindwa kutofautisha wazi hata baada ya kutafakari. Hiyo ndio sababu wanadamu wamekwama na hawasongi mbele tena. Shida hizi zote zinasababishwa na watu kutokuwa na elimu ya itikadi ambayo ni sahihi, kitu ambacho kinasababisha matatizo mengi kwa kuingia kwao. Kwa hiyo, watu hawahisi mvuto wowote katika kazi ya Mungu wa kweli, bali wanashikilia kwa kung'ang'ania[2] kazi ya mwanadamu (kama vile watu wanaowaona kama watu wakubwa) kana kwamba imepigwa muhuri na rajamu. Je, hizi si mada mpya kabisa ambazo mwanadamu anapaswa kuingia kwazo?
kutoka katika "Kazi na Kuingia (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Tanbihi:
1. "Wanaridhika na waliyo nayo maishani" inaonyesha kwamba watu hushikilia amri na hawafanyi chochote kinachokiuka sheria.
2. "Wanashikilia kwa kung’ang’ania" inatumiwa kwa dhihaka. Kirai hiki kinaonyesha kwamba watu ni wakaidi na wasiodhibitiwa kwa urahisi, wakishikilia vitu vilivyopitwa na wakati na wasiopenda kuviachilia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni