Smiley face

Jumamosi, 17 Agosti 2019

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili)

13. Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kweli kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yangechipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa cha watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, wasijue waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani. "Wanajificha tu katika unyenyekevu." Ukweli ni kwamba, wachache miongoni mwenu wanajua makusudi ya Mungu kuhusu siku za mwisho. Wachache sana miongoni mwenu wanajua wayo wa Mungu, na hata wachache zaidi wanajua jinsi utimilifu wa mwisho wa Mungu utakavyokuwa. Hata hivyo kila mtu, kwa utashi mtupu, anakubali kufundishwa nidhamu na kushughulikiwa na wengine, kana kwamba anajitayarisha[3] na kusubiri siku ambayo hatimaye wamefanikiwana wanaweza kustarehe. Sitatoa maoni yoyote juu ya "maajabu" haya miongoni mwa watu, lakini kuna hoja moja ambayo nyotemnapaswa kuielewa. Kwa sasa watu wengi wanaelekea katika hali isiyo ya kawaida[4], hatua zao za kuingia tayari zikielekea katika mwisho kabisa[5]. Pengine watu wengi wanafikiri kwamba hilo ndilo "Shangri-La" (bonde la utulivu) mwanadamu anatamani, wakiamini kuwa ni mahali pa uhuru. Kwa kweli, sivyo. Ama mtu anaweza kusema kwamba watu wamekwisha potoka.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili

14. Mungu amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, lakini hakuna mtu yeyote aliyejua kuhusu jambo hilo. Hata leo hii, hakuna mtu anayelitambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajitambulishi. Mtu anaweza kusema kwamba ni kana kwamba hatua hii ya kazi Yake inafanyika katika ulimwengu wa mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua. Mungu atakapomaliza hatua hii ya kazi Yake, kila mtu atazinduka kutoka katika ndoto yake ndefu na kugeuza mtazamo wake wa zamani[6]. Nakumbuka Mungu akisema wakati mmoja, "Kuja katika mwili wakati huu ni sawa na kuanguka katika tundu la duma." Hii ina maana kwamba kwa sababu awamu hii ya kazi ya Mungu imemfanya Mungu kuja katika mwili na kuzaliwa katika makazi ya joka kuu jekundu, kuja Kwake duniani wakati huu kumeambatana na hatari nyingi hata zaidi. Anachokabiliana nacho ni visu na bunduki na rungu; Anachokabiliana nacho ni vishawishi; Anaokutana nao ni umati wa watu wenye sura hatari zinazoonyesha kutaka kuua. Ana hatari ya kuuawa wakati wowote. Mungu alikuja na ghadhabu. Hata hivyo, Alikuja ili Aweze kufanya kazi ya kukamilisha, ikiwa na maana kwamba kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake inayoendelea baada ya kazi ya wokovu. Kwa ajili ya hatua hii ya kazi Yake, Mungu amejitolea mawazo na uangalizi wa hali ya juu kabisa na Anatumia njia yoyote inayoweza kufikiriwa ili kuepuka mashambulio ya majaribu, Akijificha kwa unyenyekevu Wake na kamwe haringii utambulisho Wake. Katika kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, Yesu alikuwa Anakamilisha tu kazi ya wokovu; Hakuwa anafanya kazi ya kukamilisha. Hivyo ni nusu tu ya kazi ya Mungu ndiyo ilikuwa inafanywa, na kukamilisha kazi ya ukombozi ilikuwa ni nusu tu ya mpango Wake mzima. Kwa kuwa enzi mpya ilikuwa inakaribia kuanza na ile ya zamani kukaribia kutoweka, Mungu Baba alianza kufikiria kwa makini kuhusu sehemu ya pili ya kazi Yake na Akaanza kujiandaa kwa ajili yake. Wakati uliopita, kupata mwili huku katika siku za mwisho huenda hakukutolewa unabii, na hivyo kuliweka msingi wa usiri mkubwa unaozunguka ujio wa Mungu katika mwili katika kipindi hiki. Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari amewasili duniani. Mungu alifanya kazi hivi ili Aifanye kazi Yake kwa urahisi na kupata matokeo bora zaidi, na pia ilikuwa ni kwa sababu ya kuepuka majaribu zaidi. Mwanadamu anapoamka kutoka usingizini, kazi ya Mungu itakuwa imekwisha kamilika zamani sana na Ataondoka, na kukamilisha maisha Yake ya kutembeatembea na kusafiri duniani. Kwa kuwa kazi ya Mungu inamtaka Mungu kutenda na kuzungumza Yeye binafsi, na kwa kuwa hakuna namna ambayo mwanadamu anaweza kusaidia, Mungu amevumilia maumivu makali ili kuja duniani kufanya kazi Yeye mwenyewe. Mwanadamu hawezi kushikilia nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hiyo Mungu alijihatarisha mara elfu kadhaa kuliko ilivyokuwa katika wakati wa Enzi ya Neema ili kuja chini mahali ambapo joka kuu jekundu linaishi ili kufanya kazi Yake, kuweka mawazo Yake yote na uangalizi katika kuokoa kundi hili la watu maskini, kulikomboa kundi hili la watu lililochafuliwa katika rundo la samadi. Ingawa hakuna anayejua uwepo wa Mungu, Mungu hahangaiki kwa sababu ni faida kubwa sana kwa kazi ya Mungu. Kila mtu ni mwovu sana, sasa inawezekanaje mtu yeyote avumilie uwepo wa Mungu? Ndiyo maana duniani Mungu yuko kimya siku zote. Haijalishi mwanadamu ni katili kiasi gani, Mungu haathiriwi nayo, bali Anaendelea tu kufanya kazi Anayotaka kuifanya ili kutimiza agizo kuu ambalo Baba wa mbinguni Alimpatia. Ni nani miongoni mwenu ametambua uzuri wa Mungu? Ni nani anayejali sana mzigo Alio nao Mungu Baba kuliko Mwana Wake Anavyofanya? Ni nani awezaye kuelewa mapenzi ya Mungu Baba? Roho wa Mungu Baba aliye mbinguni Anasumbuka kila mara, na Mwana Wake duniani Anaomba mara kwa mara juu ya mapenzi ya Mungu Baba, Akihofu sana. Kuna mtu yeyote anayejua kuhusu upendo wa Mungu Baba kwa Mwana Wake? Kuna mtu yeyote anayejua jinsi ambavyo Mwana mpendwa Anavyomkumbuka Mungu Baba? Wakipata shida ya kuchagua kati ya mbingu na nchi, wote wawili wanatazamana kutoka mbali, sambamba katika Roho. Ee wanadamu! Ni lini mtaufikiria moyo wa Mungu? Ni lini mtaielewa nia ya Mungu? Baba na Mwana siku zote Wamekuwa Wakitegemeana. Kwa nini basi Watenganishwe, mmoja juu mbinguni na mmoja chini duniani? Baba anampenda Mwana Wake kama vile Mwana anavyompenda Baba Yake. Kwa nini basi Anapaswa kusubiri kwa shauku hivyo na kwa muda mrefu huku Akiwa na hamu hivyo? Ingawa kwa muda mrefu, je, mtu yeyote anajua kwamba Baba tayari Amekuwa Akitaka sana kwa shauku kwa siku nyingi na Amekuwa Akitarajia kwa muda mrefu kurudi haraka kwa Mwana Wake mpendwa? Anatazama, Anakaa kwa utulivu, Anasubiri. Haya yote ni kwa ajili ya kutaka Mwana Wake mpendwa Arudi haraka. Ni lini Atakuwa tena na Mwana ambaye Anazungukazunguka duniani? Ingawa watakapokuwa pamoja tena, Watakuwa pamoja milele, Anawezaje kustahimili maelfu ya siku za utengano, mmoja juu mbinguni na mwingine chini duniani. Makumi ya miaka duniani ni kama maelfu ya miaka mbinguni. Mungu Baba anawezaje kutokuwa na wasiwasi? Mungu anapokuja duniani, Anapitia mabadiliko mengi ya ulimwengu wa kibinadamu jinsi mwanadamu anavyopitia. Mungu Mwenyewe hana hatia, hivyo kwa nini kumruhusu Mungu ateseke maumivu kama mwanadamu? Si ajabuMungu Baba Anatamani sana Mwana Wake Arudi haraka; nani awezaye kuuelewa moyo wa Mungu? Mungu humpa mwanadamu vitu vingi sana; mwanadamu anawezaje kuulipa moyo wa Mungu kikamilifu? Lakini mwanadamu anampatia Mungu kidogo sana; kwa hivyo Mungu angewezaje kutokuwa na wasiwasi?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili

15. Ni wachache sana miongoni mwa wanadamu wanaouelewa moyo muhimu wa Mungu kwa sababu tabia za watu ni duni sana na hisia zao za kiroho zimefifia sana, na kwa sababu hawaoni wala kutilia maanani kile ambacho Mungu anafanya. Hivyo Mungu anaendelea kuwa na hofu juu ya mwanadamu, kana kwamba asili ya kinyama ya mwanadamu inaweza kuonekana muda wowote. Hii inaonyesha zaidi kwamba kuja kwa Mungu duniani kunaambatana na majaribu makubwa. Lakini kwa ajili ya kukamilisha kundi la watu, Mungu, Akiwa Amejawa na utukufu, Alimwambia mwanadamu juu ya kila kusudi lake, bila kuficha chochote. Ameamua kwa dhati kukamilisha kundi hili la watu. Kwa hiyo, ije shida yoyote au jaribu, Anatazama kando na kuyapuuzia yote. Anafanya kazi yake kimyakimya tu, Akiamini kabisa kwamba siku moja ambapo Mungu atapata utukufu, mwanadamu atamjua Mungu, na kuamini kwamba mwanadamu atakapokuwa amekamilishwa na Mungu, atauelewa moyo wa Mungu kikamilifu. Sasa hivi kunaweza kuwepo watu wanaomjaribu Mungu au kumwelewa vibaya Mungu au kumlaumu Mungu; Mungu wala hayazingatii haya moyoni. Mungu atakapoingia katika utukufu, watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni kwa ajili ya ustawi wa binadamu, na watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ili binadamu aweze kuishi vizuri. Ujio wa Mungu umeambatana na majaribu, na Mungu pia Anakuja na uadhama na ghadhabu. Mungu anapomwacha mwanadamu, Atakuwa tayari Amepata utukufu, na Ataondoka Akiwa Amejawa na utukufu mwingi na furaha ya kurudi. Mungu anayefanya kazi duniani Hazingatii mambo moyoni Mwake haijalishi watu wamemkataa kiasi gani. Yeye anafanya tu kazi Yake.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili

16. Uumbaji wa Mungu wa ulimwengu ulianza maelfu ya miaka iliyopita, Amekuja duniani kufanya kazi isiyoweza kupimika, na Amepitia uzoefu mkubwa wa kukataliwa na kashfa na ulimwengu wa kibinadamu. Hakuna anayekaribisha ujio wa Mungu; kila mtu anamwangalia tu kwa jicho kavu. Katika kipindi hiki cha maelfu ya miaka ya taabu, matendo ya mwanadamu yamevunja kabisa moyo wa Mungu tangu zamani. Hazingatii tena uasi wa watu, lakini badala yake Anatengeneza mpango tofauti ili kumbadilisha na kumsafisha mwanadamu. Dhihaka, kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu amepitia Akiwa katika mwili—Mungu amepitia ya kutosha. Mungu katika mwili Ameteseka shida za ulimwengu wa wanadamu kikamilifu. Kwa muda mrefu Roho wa Mungu Baba wa mbinguni Aliona mambo hayo hayavumiliki na Akapumzika, Akisubiri Mwana Wake mpendwa arudi. Yote Anayoyatamani ni kwamba watu wote wasikie na kutii, waweze kuhisi aibu kubwa mbele ya mwili Wake, na wasiasi dhidi Yake. Anachokitamani ni kwamba watu wote waamini kwamba Mungu yupo. Aliacha zamani sana kutaka mambo makubwa kutoka kwa mwanadamu kwa sababu Mungu amelipa gharama kubwa sana, lakini mwanadamu hana wasiwasi[7], pasipo kuzingatia kabisa kazi ya Mungu.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Leo nyote mnajua kwamba Mungu anawaongoza watu katika njia sahihi ya uzima, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuchukua hatua inayofuata kuingia katika enzi nyingine, ambayo inamwongoza mwanadamu kuishinda enzi hii yenye giza, ya kale, kutoka katika mwili, kutoka kwenye ukandamizaji wa nguvu za giza na ushawishi wa Shetani, ili kila mtu aishi katika ulimwengu wa uhuru. Kwa manufaa ya kesho ya kupendeza, na ili kwamba watu waweze kuwa wajasiri kabisa hatua zao kesho, Roho wa Mungu anapanga kila kitu kwa ajili ya mwanadamu, na ili kwamba mwanadamu aweze kuwa na furaha kubwa zaidi, Mungu hutenga jitihada Zake zote katika mwili Akiandaa njia mbele ya mwanadamu, Akiiharakisha siku ambayo mwanadamu anaitamani sana. Nyote mnaweza kufurahia wakati huu mzuri, si rahisi kukutana pamoja na Mungu. Ingawa hamjawahi kumjua, mna muda mrefu tangu mmeshakutana naye. Ikiwa tu kila mtu angeweza kukumbuka siku zote hizi nzuri lakini fupi milele, na kuzifanya kuwa milki zao za kuwafurahisha duniani.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (5)" katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Kwa maelfu ya miaka, Wachina wamekuwa wakiishi maisha ya utumwa, na hii imebana mawazo, dhana, maisha, lugha, tabia na matendo yao kiasi kwamba wameachwa bila uhuru wowote. Maelfu kadhaa ya miaka ya historia imewafanya watu muhimu kutawaliwa na roho na kuwasuta mara kwa mara na kuwa kitu kinachofanana na maiti iliyoondokewa na roho. Wengi wao wanaoishi chini ya upanga wa Shetani, wengi wanaishi katika makazi yanayofanana na mapango ya wanyama, wengi wanakula chakula kama wanachokula ng'ombe au farasi, na wengi ni wapumbavu na katika hali ya vurugu huko "ahera." Katika umbo la nje, watu hawana tofauti na mtu wa asili, sehemu yake ya kupumzika ni kama kuzimu, kwa kuwa wandani wake wanazingirwa mashetani na mapepo wachafu wa kila aina. Kwa nje, wanadamu wanaonekana kuwa ni "wanyama" wa hali ya juu; kimsingi wanaishi na kukaa na mashetani wachafu. Bila mtu yeyote wa kuwashughulikia, watu wanaishi ndani ya mavizio ya Shetani, wamenaswa katika kazi zake za sulubu kiasi kwamba hawawezi kutoroka. Badala ya kusema kwamba wanakusanyika na wapendwa wao katika makazi yao ya furaha, wakiishi maisha ya furaha na kuridhisha, mtu anapaswa kusema kwamba wanadamu wanaishi Kuzimu, wakishughulika na mapepo na kushirikiana na mashetani. Kimsingi, watu bado wamefungwa na Shetani, wanaishi mahali ambapo pepo wachafu wanakusanyika, na wanatawaliwa na hawa mapepo wachafu, kana kwamba vitanda ni mahali pa maiti zao kulalia, kana kwamba ni mahali pa starehe.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (5)" katika Neno Laonekana katika Mwili

19. Mwanadamu anaishi bega kwa bega na wanyama, na wanashirikiana kwa amani bila ugomvi au vita vya maneno. Mwanadamu ni mgumu kuridhisha jinsi anavyowajali na kushughulika na wanyama, na wanyama wanaishi kwa ajili ya kuishi kwa mwanadamu, hasa kwa maslahi ya mwanadamu, bila wao kunufaika na chochote na kumtii mwanadamu kikamilifu. Kwa namna zote, uhusiano kati ya mwanadamu na mnyama ni wa karibu[8] na wenye mapatano[9]—na pepo wachafu, inaweza kuonekana ni muungano kamilifu wa mwanadamu na mnyama. Hivyo, mwanadamu na pepo wachafu duniani wana urafiki wa karibu zaidi na hawawezi kuachana: Ingawa mwanadamu yuko mbali na pepo wachafu, anabakia ameunganika nao; wakati ule ule, pepo wachafu hawamnyimi mwanadamu kitu chochote, na "wanatoa" vyote walivyo navyo kwake. Kila siku, watu wanachacharika katika "kasri la mfalme wa kuzimu," wakichezacheza wakiwa pamoja na "mfalme wa kuzimu" (babu yao,) na kutawaliwa naye. Ili, leo, watu wamepakwa masizi, na baada ya kuishi kwa muda mrefu sana Kuzimuni, wana muda mrefu toka waache kutamani kurudi katika "dunia ya viumbe hai." Hivyo, mara tu wanapoiona nuru, na kutazama matakwa ya Mungu, na tabia ya Mungu, na kazi Yake, wanakuwa na wasiwasi; bado wakitamani sana kurudi kuzimu na kuishi na mizimu. Walishamsahau Mungu zamani sana, na hivyo wamekuwa wakizungukazunguka katika makaburi kila mara.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (5)" katika Neno Laonekana katika Mwili

20. Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi. Mwanadamu hajui chochote kuhusu lengo la kazi ya Mungu, wala kusudi la mpango wa Mungu kwa ajili ya siku za mwisho. Kwa sababu mbalimbali, watu daima wako vuguvugu na wenye shaka[10] kuhusiana na kuingia ambako Mungu anataka, kitu ambacho kimeleta shida kubwa katika kazi ya Mungu katika mwili. Watu wanaonekana kuwa vizuizi na, hadi leo, bado hawana ufahamu sahihi. Kwa hiyo Nitazungumza juu ya kazi ambayo Mungu anafanya kwa mwanadamu, na makusudi ya Mungu ya haraka, ili kwamba nyinyi nyote muwe watumishi waaminifu wa Mungu ambao, kama Ayubu, ingekuwa bora kufa kuliko kumkataa Mungu na mtastahimili kila fedheha, na ambao, kama Petro, mtatoa hali zenu zote kwa Mungu na kuwa wandani ambao Mungu aliwapata katika siku za mwisho. Ninawasihi ndugu na dada wote kufanya yote iwezekanayo kutoa hali zao zote kwa mapenzi ya mbinguni ya Mungu, kuwa watumishi watakatifu katika nyumba ya Mungu, na kufurahia ahadi zisizokuwa na kikomo zilizofadhiliwa na Mungu, ili kwamba moyo wa Mungu Baba ufurahie pumziko la amani hivi punde. "Kukamilisha mapenzi ya Mungu Baba" kunapaswa kuwe wito wa wote wanaompenda Mungu. Maneno haya yanapaswa kutumika kama mwongozo wa mwanadamu kwa ajili ya kuingia na dira inayoongoza matendo yake. Hili ndilo azimio ambalo mwanadamu anapaswa kuwa nalo. Kukamilisha kabisa kazi ya Mungu duniani na kushirikiana na kazi ya Mungu katika mwili–huu ni wajibu wa mwanadamu. Siku moja, kazi ya Mungu itakapokuwa imekamilika, mwanadamu atamuaga Anaporudi mapema kwa Baba yake mbinguni. Je, huu sio wajibu ambao mwanadamu anapaswa kuutimiza?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (6)" katika Neno Laonekana katika Mwili

21. Kwa mwanadamu, Mungu kusulubiwa kulihitimisha kazi ya Mungu kupata mwili, kuliwakomboa binadamu wote, na kukamruhusu kutwaa ufunguo wa Kuzimu. Kila mtu anadhani kwamba kazi ya Mungu imekamilika kikamilifu. Kwa uhalisia, kwa Mungu, ni sehemu ndogo tu ya kazi Yake ndiyo imekamilika. Amemkomboa tu binadamu; Hajawashinda wanadamu, sembuse kubadilisha ubaya wa Shetani ndani ya binadamu. Hiyo ndio maana Mungu anasema, "Ingawa mwili Wangu ulipitia maumivu ya kifo, hilo halikuwa lengo lote la Mimi kupata mwili. Yesu ni Mwana Wangu mpendwa na Alisulubishwa msalabani kwa ajili Yangu, lakini hakukamilisha kazi Yangu kikamilifu. Alifanya tu sehemu ya kazi hiyo." Hivyo Mungu akaanza sehemu ya pili ya mipango ili kuendeleza kazi ya kupata mwili. Lengo kuu la Mungu ni kumkamilisha na kumpata kila mmoja aokolewe kutoka katika mikono ya Shetani, hiyo ndiyo sababu Mungu alijiandaa tena kujihatarisha ili kuja katika mwili.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (6)" katika Neno Laonekana katika Mwili

22. Katika maeneo mengi, Mungu ametabiri kupata kundi la washindi katika nchi ya Sinim. Ni upande wa Mashariki mwa ulimwengu ambapo washindi wanapatikana, hivyo mahali pa kupata mwili mara ya pili ambapo Mungu atatua bila shaka ni nchi ya Sinim, mahali hasa ambapo joka jekundu linaishi. Hapo Mungu atawapata warithi wa joka kuu jekundu ili lipate kushindwa na kuaibishwa. Mungu anataka kuwaamsha watu hawa walioteseka sana, kuwaamsha kabisa, na kuwafanya waondoke katika ukungu na kulikataa joka kuu jekundu. Mungu anataka Awaamshe kutoka katika ndoto zao, kuwafanya waelewe tabia ya joka kuu jekundu, waitoe mioyo yao yote kwa Mungu, wainuke kutoka katika nguvu kandamizi za giza, wasimame Mashariki mwa dunia, na kuwa uthibitisho wa ushindi wa Mungu. Hapo basi tu ndipo Mungu atapata utukufu. Kwa sababu hii tu, Mungu aliipeleka kazi ambayo ilisitishwa Israeli katika nchi ambako linakaa joka kuu jekundu na, takribani miaka elfu mbili baada ya kuondoka, Amekuja tena katika mwili ili kuendeleza kazi ya Enzi ya Neema. Machoni pa mwanadamu, Mungu anazindua kazi mpya katika mwili. Lakini kwa Mungu, Anaendeleza kazi ya Enzi ya Neema, ikitofautiana kwa muda wa miaka elfu kadhaa, na badiliko tu la eneo la kufanyia kazi na mradi wa kazi. Ingawa taswira ya mwili ambayo Mungu ameichukua katika kazi ya leo ni mtu mwingine tofauti na Yesu hasa, wanashiriki hulka na mzizi mmoja, na wanatoka katika chanzo kimoja. Pengine wana tofauti za umbo la nje, lakini kweli za ndani za kazi Zao zinafanana kabisa. Hata hivyo, enzi zenyewe, ni tofauti kama ilivyo usiku na mchana. Inawezekanaje kazi ya Mungu isibadilike? Au inawezekanaje kazi ziingiliane?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (6)" katika Neno Laonekana katika Mwili

23. Yesu alionekana katika umbo la Myahudi, Alifuata mavazi ya Wayahudi, na Alikua akila chakula cha Kiyahudi. Hii ni hali yake ya kawaida ya kibinadamu. Lakini Mungu katika mwili wa leo Anachukua umbo la watu wa Asia na Anakua Akila chakula cha taifa la joka kuu jekundu. Hii haiingiliani na lengo la Mungu kupata mwili. Badala yake, vinakamilishana, na zaidi vinakamilisha maana ya kweli ya Mungu kupata mwili. Kwa sababu Mungu katika mwili Anarejelewa kuwa "Mwana wa Adamu" au "Kristo," umbo la nje la Kristo wa leo haliwezi kulinganishwa na Yesu Kristo. Hata hivyo, mwili unaitwa "Mwana wa Adamu" na upo katika sura ya mwili. Kila hatua ya kazi ya Mungu inahusisha maana ya kina sana. Sababu ya Yesu kuzaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu ni kwa sababu Alipaswa kuwakomboa wenye dhambi. Alitakiwa Asiwe na dhambi. Isipokuwa tu mwishoni Alipolazimishwa kufanana na mwili wa dhambi na kuchukua dhambi za wenye dhambi ndipo Aliwaokoa kutoka katika laana ya msalaba ambao Mungu aliutumia kuwaadibu watu. (Msalaba ni zana ya Mungu kwa ajili ya kuwalaani na kuwaadibu watu; mitajo ya kulaani na kuadibu mahususi inahusu kuwalaani na kuwaadibu wenye dhambi.) Lengo lilikuwa ni kuwafanya wenye dhambi wote watubu na kuutumia kusulubiwa kuwafanya waungame dhambi zao. Yaani, kwa ajili ya kuwakomboa binadamu wote, Mungu alijiweka katika mwili uliozaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu na Akachukua dhambi za binadamu wote. Namna ya kawaida ya kuelezea hii ni kutoa mwili mtakatifu kwa kubadilishana na wenye dhambi wote, ikilinganishwa na Yesu kuwa sadaka ya dhambi aliyewekwa mbele ya Shetani ili "kumsihi" Shetani kuwarudisha binadamu wote wasio na hatia kwa Mungu, ambao alikuwa amewakandamiza. Hivyo ili kukamilisha hatua hii ya kazi ya wokovu kulihitaji utungaji mimba kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hili lilikuwa ni sharti la lazima, "mkataba" wakati wa vita kati ya Mungu Baba na Shetani. Hii ndio maana Yesu alikabidhiwa kwa Shetani, na ni baada ya hapo tu ndipo hatua hii ya kazi ikahitimishwa. Hata hivyo, kazi ya ukombozi ya Mungu leo tayari ni ya umuhimu usio kifani, na Shetani hana sababu ya kufanya madai, hivyo Mungu kufanyika mwili hakuhitaji utungaji mimba kwa njia ya Roho Mtakatifu, maana Mungu kwa asili ni mtakatifu na Asiye na hatia. Hivyo Mungu mwenye mwili wa wakati huu sio tena Yesu wa Enzi ya Neema. Lakini bado ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na kwa ajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu Baba. Hii inaweza kuchukuliwaje kuwa ni msemo usiokuwa na maana? Je, lazima Mungu kupata mwili kufuate kanuni kadhaa?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (6)" katika Neno Laonekana katika Mwili

24. Watu wengi wanatafuta ushahidi katika Biblia, wakitaka kutafuta unabii wa Mungu kupata mwili. Inawezekanaje fikra hafifu za mwanadamu kujua kwamba Mungu aliacha "kufanya kazi" muda mrefu uliopita kwenye Biblia na "Ameachana" nayo na kufurahia kazi ambayo Alipanga kwa bidii kwa muda mrefu lakini Hakuwahi kumwambia mwanadamu? Watu wanakosa sana ufahamu. Baada tu ya kuonja tabia ya Mungu, kwa kawaida wanasimama kwenye jukwaa refu na kukaa kwenye "kiti mwendo" cha hali ya juu wakikagua kazi ya Mungu, na hata kuanza kumfundisha Mungu kwa mazungumzo ya misamiati migumu. "Mzee" akiwa amevaa miwani na kupapasa ndevu zake, anafunua shajara yake ya "mwaka kuukuu" (Biblia) ambayo amekuwa akiisoma maisha yake yote. Akisema maneno kimyakimya na macho yakionekana kung’aa, sasa anarudi katika Kitabu cha Ufunuo na sasa katika kitabu cha Danieli, na sasa katika Kitabu kinachojulikana sana cha Isaya. Akikodolea macho ukurasa ulioandikwa maneno mengi madogo, anasoma kimya, akili yake ikizunguka bila kupumzika. Ghafula mkono unaopapasa ndevu unasita na kuanza kuzivuta. Kila mara mtu anasikia sauti ya ndevu zikivunjwa. Tabia hiyo isiyo ya kawaida inamstaajabisha mtu. "Kwa nini kutumia nguvu zote hizo? Kilichowakasirisha hivyo ni nini?" Tukirudi kwa mtu mzee, nyusi zake sasa zimesimama. Nyusi zenye rangi ya fedha zimeanguka kama manyoya ya bata bukini sentimita mbili kamili kutoka katika kope za mzee huyu, kama tu kwa bahati lakini kwa usahihi kabisa, mzee huyu anapoendelea kukaza macho yake katika kurasa zinazoonekana nzee. Anarudia mtiririko huo wa matendo mara kadhaa, kisha anashindwa kuvumilia bali anasimama na kuanza kupiga domo kana kwamba anafanya porojo[11] na mtu, ingawa mwanga katika macho yake bado haujatoka katika shajara yake ya mwaka. Ghafula anafunika ukurasa aliokuwa anausoma na kuugeukia "ulimwengu mwingine." Nyendo zake ni za haraka sana na za kuogofya takribani kuwashtua watu. Sasa, panya ambaye alikuwa ametoka katika shimo lake na alikuwa tu ameanza "kujisikia huru" wakati wa ukimya wake alishtushwa sana na mizunguko yake isiyoeleweka na kukimbia kurudi moja kwa moja katika shimo, na kutoweka asionekane tena. Sasa mkono wa kulia wa mzee uliokuwa umetulia unarudia mwendo wake wa kupapasa ndevu juu chini. Anaondoka kwenye kiti, na kuacha kitabu mezani. Upepo unaingia ndani kupitia mlango ulio wazi kidogo na dirisha lililo wazi, , unapeperusha kitabu bila kujali nacho kinajifunika, kisha kinafunguka, kinajifunika, kisha kinafunguka tena. Kunao ukiwa usioweza kuelezeka kuhusu tukio hili, isipokuwa tu kwa sauti ya kurasa za kitabu zinazopeperushwa na upepo, kila kitu kinaonekana kuwa kimya. Yeye, akiwa amefumbata mikono nyuma, anatembeatembea chumbani, sasa anasimama, sasa anaanza, anatikisa kichwa chake mara kwa mara, anaonekana kurudia kusema "Ee! Mungu! Ungeweza kweli kufanya hivyo?" Anatikisa kichwa pia mara kwa mara, "Ee Mungu! Nani anaweza kuijua kazi Yako? Je, si vigumu kuzitafuta hatua Zako? Ninaamini Hufanyi vitu visivyokuwa na maana." Sasa mzee huyu anaukunja uso, anayafumba macho yake kwa nguvu, akionyesha haya, pia anaonyesha maumivu makali kupita kiasi, kana kwamba anataka kutafakari taratibu. Hii kweli inampatia changamoto "mzee huyu wa fahari." Katika hatua hii ya maisha yake, "kwa bahati mbaya" amekutana na suala hili. Nini kinaweza kufanywa ili kukabiliana nalo? Nami pia nimekanganyika na sina uwezo wa kufanya kitu chochote. Nani aliyeifanya shajara yake ya mwaka kuchakaa? Nani aliyezifanya ndevu na nyusi zake zote kukua bila huruma kama theluji nyeupe katika sehemu mbalimbali ya uso wake? Ni kana kwamba ndevu zake zinawakilisha usuli wake. Lakini nani angejua mwanadamu angekuwa mpumbavu kwa kiasi hiki, akiutafuta uwepo wa Mungu katika shajara ya mwaka kuukuu? Shajara hii ya mwaka ya zamani inaweza kuwa na karatasi ngapi? Je, inaweza kweli kurekodi matendo yote ya Mungu? Nani anathubutu kuhakikisha hilo? Mwanadamu kimsingi anatafuta umbo la Mungu na anajaribu kutimiza mapenzi ya Mungu kwa kuchanganua maneno mno[12]. Je, kujaribu kuingia katika uzima kwa namna hii ni rahisi? Je, huku sio kufikiri bila mantiki na kimakosa? Huoni hii inachekesha?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (6)" katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

3. "Anajitayarisha" imesemwa kwa dhihaka.

4. "Isiyo ya kawaida" inaonyesha kwamba kuingia kwa watu kumeacha maadili na uzoefu wao unaegemea upande mmoja.

5. "Mwisho kabisa" unaonyesha kuwa watu wanatembelea njia ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu.

6. "Geuza mtazamo wake wa zamani" inahusu jinsi dhana za watu na maoni kuhusu Mungu yanavyobadilika mara tu wanapomjua Mungu.

7. "Hana wasiwasi" inaonyesha kwamba watu hawajali juu ya kazi ya Mungu na hawaioni kama muhimu.

8. "Wa karibu" inatumiwa kwa dhihaka.

9. "Wenye mapatano" inatumiwa kwa mzaha.

10. "Wenye shaka" inaashiria kwamba watu hawana umaizi dhahiri katika kazi ya Mungu.

11. "Porojo" ni istiara kwa ajili ya sura mbaya ya watu wanapochunguza katika kazi ya Mungu.

12. "Kuchanganua maneno mno" kunatumiwa kudhihaki wataalam katika hoja za uwongo, ambao hubishana juu ya tofauti ndogondogo kuhusu maneno lakini hawautafuti ukweli au kujua kazi ya Roho Mtakatifu.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni