Smiley face

Jumamosi, 30 Novemba 2019

Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Maisha ya kanisa
Yixin Jiji la Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei
Kabla, ningewasikia mara kwa mara ndugu zangu wa kiume na wa kike wakisema, “Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya matokeo mazuri; ndiyo yote wanayohitaji watu.” Nilikubali hili na kukubaliana nalo, lakini sikuwa na ufahamu wowote kupitia uzoefu wangu mwenyewe. Baadaye nilipata ufahamu kiasi kwa njia ya mazingira ambayo Mungu aliniumbia.

Ijumaa, 29 Novemba 2019

Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu

Umwombe Mungu
Xiaowei Mji wa Shanghai
Wakati fulani kitambo, hata kama daima nilipata msukumo kiasi na fadhila wakati dada mmoja aliyeshiriki nami alishiriki nuru aliyokuwa amepata wakati alipokula na kunywa neno la Mungu, pia kila wakati nilikuwa na hisia ya muda mrefu kuwa alikuwa anajionyesha. Ningejiuliza, “Nikimjibu sasa hivi, sitakuwa nikimtia moyo? Kwa namna hiyo, sitaonekana basi kuwa duni kuliko yeye?” Matokeo yake yakawa, nilikataa kutaja maoni yangu mwenyewe katika ushirika au kutoa maoni kuhusu mawazo yoyote aliyoshirikisha. Wakati mmoja, dada yangu, alipopata utambuzi fulani kutoka kwa kula na kunywa fungu fulani la neno la Mungu, alihisi kuwa kulikuwa na kasoro fulani na hali yetu na kuniuliza kama ningekuwa radhi kuwasiliana naye kuhusu fungu hilo la neno la Mungu. Mara tu alipouliza, mawazo haya yote na hisia za chuki zilitanda juujuu: “Unataka tu kujishuhudia mwenyewe, kuwa na wasikilizaji wa kuhubiria. Kwa nini niwasiliane na wewe?” Hata nilifika kiwango cha kuhepa mkutano ili isinibidi kumsikiliza. Baada ya muda, nilihisi uzito mkubwa moyoni mwangu, nilijua kitu fulani kilikuwa kibaya na hali yangu, lakini sikuweza kufikiria njia nzuri ya kutatua mgogoro wangu wa ndani. Kile nilichoweza kufanya tu ni kujishughulisha kikamilifu katika wajibu wangu, kula na kunywa neno la Mungu, na kuimba nyimbo za injili ili kujizuia kutokana na hisia hizi hasi. Hata hivyo, kila mara nililazimika kukabiliana na hali ya sasa, uharibifu huo huo ungeinuka katika moyo wangu—mambo yalikuwa yanazidi kuwa mabaya, sio mazuri—na sikuwa na dokezo la nini kufanya kuhusu hayo.

Alhamisi, 28 Novemba 2019

Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Kumwabudu Mungu
Wu Xia Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong
Baada ya kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli. Hata hivyo, ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mungu tu nilipoweza kuona kwamba kwa hakika sikujifahamu kulingana na neno la Mungu.

Jumatano, 27 Novemba 2019

Sitapumbazwa Tena na Nia Njema

Kumwabudu Mungu
Meng Yu Mji wa Pingdingshan, Mkoa wa Henan
Wakati mmoja nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, niliona kuwa ndugu fulani alikuwa akijaribu kuwafurahisha dada zake, maonyesho ya hali mbovu ya tabia yake machoni mwangu. Niliamua kutafuta fursa ya kumkumbusha haya mambo. Siku zilipita na nikaona utendaji wake wa wajibu ulikuwa wenye matokeo machache mazuri—ushahidi wa maoni yangu ya awali kumhusu. Kwa hiyo niliamua kuzungumza naye uso kwa uso. Hata hivyo, tulipogusia suala hili, alikataa kwa ukali maoni yangu yote na akajibu kwa ukali kwamba nilikuwa mwenye kukosoa sana. “Kwa miaka hii yote,” alisema, “wakati wowote unapowasiliana nami, unanikemea kwa mtazamo wa kudharau, na leo unasema kwa namna hiyo ya kudharau....” Mazungumzo hayo yakageuka kuwa mabaya zaidi kuliko yasiyozaa matunda—yalivunjika kwa kutokubaliana kabisa. Majibizo yake yaliniongoza kwa uamuzi mchungu, nikifikiri: “Niliwasiliana ili nisaidie, sio kukuaibisha kwa kufichua upungufu wako. Badala ya kusikiliza, ulinitafutia makosa na kunishutumu kuwa mwenye mtazamo wa kudharau. Sawa! Mimi nitakuacha uwe. Hata hivyo, nia zangu zilikuwa njema, na kukatalia kwako kunaonyesha tu kuwa hutafuti ukweli.” Tangu wakati huo, daima nimejichukulia kama yule ambaye alikuwa sahihi, wakati nikifikiri ndugu huyo ndiye aliyekuwa na makosa peke yake. Hata hivyo, hivi karibuni nilipata ufahamu kujihusu kwa njia ya kushughulikia watu, vitu na mambo ambavyo Mungu ameweka karibu nami.

Jumanne, 26 Novemba 2019

Ni Kwa Kuuelewa Ukweli tu Ndio Mtu Anaweza Kuwa na Utambuzi

Umwombe Mungu
Yi Ran Mji wa Laiwu , Mkoa wa Shandong
Wakati fulani awali, kwa sababu yangu kutoelewa kanuni iliyotumiwa na kanisa ya masahihisho ya wafanyakazi wa kanisa, wakati kanisa lilibadilisha kiongozi, dhana iliibuka ndani yangu. Kutoka kwa kile nilichoweza kuona, dada aliyebadilishwa alikuwa mzuri sana kwa kupokea na kushirikiana ukweli, na aliweza kuwa wazi juu ya maonyesho yake ya upotovu. Kwa hiyo sikuweza kujua asilani jinsi mtu fulani aliyetafuta ukweli sana angeweza kubadilishwa. Inawezekana kwamba yeye alizungumza juu ya maonyesho yake mwenyewe ya upotovu sana, na hivyo kiongozi wake kwa makosa alimchukua kuwa mtu asiyefuatilia ukweli, na kumbadilisha? Kama hili ndilo lililotokea kweli, basi si fursa ya mafunzo kwa mtu ambaye alikuwa anafuta ukweli imeangamizwa?

Jumatatu, 25 Novemba 2019

Watu Wasio na Hila Sio Lazima Wawe Waaminifu

Utambuzi wa Maisha
Cheng Mingjie Jiji la Xi’an, Mkoa wa Shaanxi
Mimi hujiona kuwa mtu wa aina ya kuwa wazi na mchangamfu. Mimi huzungumza na watu kwa njia ya waziwazi; chochote ninachotaka kusema, mimi husema—mimi sio aina ya mtu wa kuzungukazunguka. Katika kuingiliana kwangu na watu mimi huwa ni mwaminifu na wazi kiasi. Mara kwa mara, mimi hudanganywa na kudhihakiwa kwa sababu ya kuwaamini wengine kwa urahisi. Ilikuwa tu baada ya kuanza kwenda kanisani nilipopata mahali ambapo ningepaita pangu. Nilijiwazia mwenyewe: “Katika siku za nyuma kutokuwa na hila kwangu kumenifanya mwenye kuweza kudhuriwa na udanganyifu wa wengine; lakini katika kanisa Mungu anataka watu waaminifu, kwa hivyo mimi si lazima niwe na wasiwasi tena juu ya kuwa maasumu.” Nilihisi faraja hasa niliposikia kwamba Mungu anawapenda wale waaminifu na sahili, na kwamba ni waaminifu tu watakaopata wokovu wa Mungu. Nilipoona jinsi ndugu zangu wa kiume na wa kike walivyokuwa na majonzi walipoanza kutambua asili yao ya udanganyifu lakini hawakuweza kuibadilisha, nilihisi kufarijika hata zaidi kwamba, kuwa mwaminifu na waziwazi, isingenibidi kupitia majonzi kama hayo. Siku moja, hata hivyo, baada ya kupokea ufunuo kutoka kwa Mungu, hatimaye niligundua kwamba sikuwa mtu mwaminifu niliyedhani nilikuwa.

Jumapili, 24 Novemba 2019

Kwa Nini Sijabadilika Baada ya Miaka Mingi ya Imani

Kutafakari kwa Kikristo
Jinru Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan
Wakati ndugu wa kiume au wa kike alipoonyesha dosari zangu au hakusikiza kauli yangu ama sikuhisi kushawishika au nilibishana nao. Nilijutia vitendo vyangu baadaye, lakini nilipokabiliwa na mambo haya, sikuweza kujizuia mwenyewe kuifichua tabia yangu potovu. Nilisumbuliwa na hili kwa kina, na nikafikiri: Kwa nini maneno ya wengine yanaweza kuniaibisha hadi kukasirika? Na kwa nini sijabadilika hata kidogo licha ya miaka minane ya kumfuata Mungu? Nilikuwa na wasiwasi na tena na tena nilitafuta kutoka kwa Mungu, nikimuuliza kunipa nuru ili niweze kujua chanzo cha mbona tabia yangu potovu haikuwa imebadilika

Jumamosi, 23 Novemba 2019

Kupata Ahueni kwa Njia ya Kumwamini Mungu

Zenye Kupumzisha
Zhuanbian Mji wa Shanghai
Ingawa nilikuwa nikimfuata Mungu kwa miaka mingi, nilikuwa karibu sijafanya maendeleo yoyote na kuingia kwangu katika maisha, na hii ilinifanya nihisi kuwa na wasiwasi sana. Hasa wakati niliposikia rekodi ya mahubiri juu ya kuingia kwa maisha, na kusikia mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu akizungumza na ndugu wa kiume na wa, nilihisi nikiwa nimejawa na wasiwasi nikimsikia akisema jambo kama hili, “Nyinyi sasa mnamwamini Mungu na mmeonja uzuri wa ukimbizaji wa ukweli. Nyinyi mmeanza kuingia kwa njia sahihi na mmejaa imani katika ukimbizaji wenu wa wokovu.” Nikawaza, “Watu hawa wamemwamini Mungu kwa muda mfupi sana lakini wameingia tayari na wamejaa imani sana kuhusu kuokolewa. Na bado niko hapa nikiwa nimemwamini Mungu hadi sasa na bado sijaipata ukweli na tabia yangu katika maisha haijapitia mabadiliko yoyote kamwe, bila kujali kuwa nilikuwa nimeingia kwa njia sahihi. Ni rahisi kuongelea kufikia wokovu kuliko kukuweka katika vitendo!” Niliwaza jinsi hao wa hapo juu walifanya ushirika kwamba ukweli ungeweza kutatua upotovu wote wa wanadamu, lakini sikuwa nimepitia jambo hili kamwe. Hata nilihisi kwamba ukweli ungeweza kutatua upotovu wa watu wengine lakini sio wangu mwenyewe, kwa hiyo nilipoteza imani katika ukimbizaji wangu wa ukweli na wa wokovu. Ingawa nilikuwa na ufahamu kwamba hali yangu mwenyewe haikuwa sahihi, hapakuwa na njia yoyote ambayo ningeweza kuiepuka, hivyo ningeweza tu kumlilia Mungu kwa msaada. Baadaye, maneno Yake yalinipatia nuru, yakinifanya nione ni kwa nini nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi hivyo na bado sikuwa nimeendelea katika maisha, na kwa nini hali yangu haikuwa imepitia mabadiliko yoyote. Mungu pia aliniweka kwa njia ya kutenda na kuingia katika ukweli.

Ijumaa, 22 Novemba 2019

Mateso na Maafa Yalinisaidia Kukua

Theluji
Baituo Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Kabla, nilijua tu kwamba hekima ya Mungu ilitumiwa kwa msingi wa njama za Shetani, kwamba Mungu ni Mungu mwenye hekima na kwamba Shetani milele atakuwa adui mshinde wa Mungu katika nadharia, lakini sikuwa na ufahamu halisi au maarifa. Baadaye, ni ndani tu ya mazingira yaliyopangwa na Mungu nilipopata uzoefu halisi wa kipengele hiki cha kweli.

Alhamisi, 21 Novemba 2019

Asili ya Upendo wa Mungu Ni Nini?

Zenye Kupumzisha
Siqiu Mji wa Suihua, Mkoa wa Heilongjiang
Wakati wowote ninapoona kifungu kinachofuata cha neno la Mungu, “Ikiwa daima umekuwa mwaminifu sana Kwangu na kunipenda, lakini unapitia mateso ya maradhi, umaskini wa maisha, na kutelekezwa na marafiki na jamaa au kupitia maafa mengine yoyote maishani, basi, uaminifu na mapenzi yako Kwangu yataendelea kuwepo?” (“Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ninahisi hasa nisiye na furaha—hisi ya huzuni hunyatia ndani yangu na moyo wangu husema malalamiko yake yasiyoghuna: Ewe Mungu, Unawezaje kuruhusu wale walio waaminifu Kwako na wanaokupenda Wewe kukutana na msiba wa jinsi hiyo? Matokeo yake, nimekuwa na wakati mgumu kuelewa maana ya mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu ambaye alisema, “Mahitaji ya mwisho ya Mungu ya mtu ni ya kupenda na ya kweli.”

Jumatano, 20 Novemba 2019

Kazi ya Mungu Ni ya Hekima Sana

Zenye Kupumzisha
Shiji Jiji la Ma’anshan, Mkoa wa Anhui
Wakati wa kufanya kazi kwangu kama kiongozi katika kanisa, kiongozi wangu mara nyingi angeshirikiana mifano ya kushindwa kwa wengine ili kutumikia kama somo kwetu. Kwa mfano: Viongozi wengine walizungumza tu kuhusu elimu na mafundisho lakini walikosa kutaja upotovu wao au kuwasiliana kwa karibu kuhusiana na ufahamu wao wa jinsi ukweli unavyotumika kwa ukweli. Kama matokeo, hawakuweza kufanya kazi ya utendaji, wakigeuka kuwa viongozi wa uwongo wa kubadilishwa. Viongozi wengine wangejionyesha, kujiinua na kujishuhudia wenyewe ili kulinda hadhi yao. Mwishowe, viongozi kama hawa waliwaongoza watu mbele yao na wakawa wapinga Kristo ambao walikuwa wametenda aina zote za uovu na ambao walifukuzwa kutoka kanisani. Viongozi wengine, wakati wa kazi yao, wangeonyesha nadhari kubwa mno kwa miili yao wenyewe, wakitamani wasaa wa burudani na bila kufanya kazi yoyote halisi kamwe. Viongozi hao walikuwa kama vimelea wanaotegemea faida za hadhi ya kanisa. Hatimaye, walifichuliwa na kuondoshwa. … Baada ya kusikia visa hivi vya kushindwa, swali lilikuja katika mawazo yangu: Si Mungu ni Mwenye Uweza? Kwa kuwa viongozi hawa walikuwa wanafanya uovu, wakimpinga Mungu na kuathiri vibaya kazi ya kanisa, kwa nini Mungu hakuingilia haraka ili kuwafichua na kuwaondosha viongozi hawa wa uongo? Kwa njia hii, si maisha ya ndugu zangu wa kiume na wa kike na kazi zote za kanisa zingekuwa bila madhara? Swali hili lilibakia katika mawazo yangu bila jibu.

Jumanne, 19 Novemba 2019

Roho ya Majivuno Kabla ya Kuanguka

Kumwabudu Mungu
Baixue Mji wa Shenyang
Kwa sababu ya mahitaji ya kazi, nilihamishiwa hadi sehemu nyingine ya kazi. Wakati huo, nilikuwa na shukurani sana kwa Mungu. Nilihisi kwamba nilikuwa ninapungukiwa sana, lakini kwa njia ya ukuzwaji mtakatifu na Mungu, nilipewa nafasi ya kutimiza wajibu wangu katika eneo la kazi la ajabu hivyo. Niliweka nadhiri kwa Mungu moyoni mwangu: Ningefanya lote ninaloweza kumlipa Mungu.

Jumatatu, 18 Novemba 2019

Mbona Ujihusishe na Hila Unapomtumikia Mungu

Sala ya kweli
Hu Qing Jijini Suzhou, Mkoani Anhui
Nilipoona maneno ya Mungu yakisema: “Wale ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli walivyo na uwezo. …Wao daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi?” (“Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo), Nilifikiri mwenyewe: Nani ana ujasiri kama huo kujaribu kupata ujanja mpya ya ubunifu? Nani hajui kuwa tabia ya Mungu haistahimili kosa la mwanadamu? Bila shaka siwezi kuthubutu! Mimi binafsi niliamini kuwa nilikuwa na moyo wa kumcha Mungu, na katika kazi yangu sikuthubutu kujaribu kutafuta mbinu. Hata hivyo, ilikuwa tu katika ufunuo wa Mungu wa ukweli ndio nilitambua kuwa kujaribu kutafuta mbinu mpya sio kile mtu huthubutu au hathubutu kufanya—kunaamuliwa kabisa na asili ya kiburi.

Jumapili, 17 Novemba 2019

Niliona Kimo Changu cha Kweli kwa Dhahiri

Umwombe Mungu
Ding Xiang Jijini Tengzhou, Mkoa wa Shandong
Katika mkutano wa viongozi wa kanisa niliowahi kuhudhuria, kiongozi wa kanisa aliyekuwa amechaguliwa hivi karibuni alisema: “Sina kimo cha kutosha. Mimi ninahisi sifai kuutimiza wajibu huu. Mimi ninahisi kushinikizwa na vitu vingi sana, kwa kiwango kwamba mimi sijaweza kupata usingizi kwa siku na usiku kadhaa mtawalia….” Wakati huo, mimi nilikuwa nimebeba mizigo katika kumfuatilia Mungu, kwa hivyo niliwasiliana naye: “Kazi zote hufanywa na Mungu; mwanadamu hushirikiana kidogo tu. Ikiwa tunahisi kulemewa, kuja mbele za Mungu mara nyingi na kumtegemea Mungu bila shaka kutatufanya tuone uweza wote na hekima ya Mungu. Kuhisi mzigo kutokana na kazi zetu ni kitu kizuri. Lakini ikiwa mzigo unageuka kuwa mfadhaiko, huo utakuwa kizuizi, na utasababisha uhasi na hata kutoelewana kuhusiana na Mungu.” Chini ya mwongozo wa Mungu, nilihisi mawasiliano yangu yalikuwa hasa yenye mwanga. Dada pia alitambua ya kwamba alikuwa katika hali ambapo Mungu hakukuwa na nafasi katika moyo wake, na kwamba alikuwa akijifanyia mwenyewe badala ya kumtegemea Mungu, na hivyo akapata njia ya kuingia. Mimi nilikuwa na furaha sana wakati huo kwa sababu nilidhani ningeweza kutatua shida ya yule dada, kudhibitisha kwamba nilimiliki uhalisi wa sehemu hii ya ukweli.

Jumamosi, 16 Novemba 2019

Maneno ya Mungu Yameniamsha

Sala ya kweli
Miao Xiao Mji wa Jinan, Mkoa wa Shandong
Katika siku zilizopita, nilikuwa daima nikifikiri kuwa Mungu aliposema “kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi” Alikuwa anaashiria wale wanaoikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho lakini ambao baadaye wanarudi nyuma. Kwa hivyo, wakati wowote nilipoona ndugu wakijiondoa katika njia hii kwa sababu yoyote ile, moyo wangu ungejawa na dharau kwao. Huyo, kibaraka na msaliti mwingine anatoroka kutoka kwa kiti kikuu cheupe cha enzi ambaye atapokea adhabu ya Mungu. Wakati uo huo, nilijihisi nikiwa nikitenda ifaavyo kwa kukubali hukumu ya Mungu na nilikuwa siko mbali na kukubali ukombozi wake Mungu.

Ijumaa, 15 Novemba 2019

Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu

Maisha ya kanisa
Heyi Mji wa Zhuanghe, Mkoa wa Liaoning
Nilikuwa nimechaguliwa karibuni tu kuchukua jukumu la kiongozi wa kanisa. Lakini baada ya kipindi cha kazi ngumu, sio tu kuwa kazi ya kiinjili ilikuwa bila uhai kiasi, lakini ndugu zangu wa kiume na wa kike katika kikundi cha kiinjili walikuwa pia wakiishi katika hali hasi na ya udhaifu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, sikuweza tena kudhibiti hisia zangu. Ni vipi tena ningeweza kuiamsha kazi ya kiinjili? Baada ya kupiga ubongo wangu, hatimaye nilifikiria suluhisho zuri: Kama ningefanya sherehe ya kila mwezi kwa kikundi cha kiinjili na kuwachagua watu waliojipambanua na wahubiri wa kielelezo, yeyote ambaye angeshinda roho zaidi kwa ajili ya Mungu angepewa thawabu, na yeyote ambaye angeshinda roho chache angeonywa. Hili halingeisisimua shauku yao tu, lakini lingewainua ndugu wa kike na wa kiume waliokuwa hasi na dhaifu. Nilipofikiria hili, nilifurahishwa sana na hili “tendo langu la werevu”. Niliwaza “Wakati huu kwa kweli nitamshangaza kila mtu.”

Alhamisi, 14 Novemba 2019

Kutambua Kuwa Niliitembea Njia ya Mafarisayo

Umwombe Mungu
Wuxin Mji wa Taiyuan, Mkoa wa Shanxi
Kitu ambacho tumezungumzia mara kwa mara katika ushirikiano wa awali ni njia ambazo zilitembewa na Petro na Paulo. Inasemekana kwamba Petro alizingatia kujijua mwenyewe na kumjua Mungu, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimpenda, ilhali Paulo alizingatia tu kazi yake, sifa na hadhi yake, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimdharau. Daima nimekuwa na hofu ya kuitembea njia ya Paulo, ambayo ndiyo sababu mimi kwa kawaida mara nyingi husoma maneno ya Mungu kuhusu uzoefu wa Petro ili kuona jinsi alivyopata kumjua Mungu. Baada ya kuishi hivi kwa muda, nilihisi kwamba nilikwishakuwa mtiifu zaidi kuliko hapo awali, hamu yangu ya sifa na hadhi ilikuwa imedidimia, na kwamba nilikuwa nimepata kujijua kidogo. Wakati huu, niliamini kwamba ingawa sikuwa kabisa kwa njia ya Petro, inaweza kusemwa kuwa nilikuwa nimegusa ukingo wake, na angalau ilimaanisha sikuwa naelekea kwa njia ya Paulo. Hata hivyo, ningeaibishwa na ufichuzi wa neno la Mungu.

Jumatano, 13 Novemba 2019

Kiini cha Kutumia Mamlaka Vibaya Kwa Ajili ya Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi

Kiini cha Kutumia Mamlaka Vibaya Kwa Ajili ya Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi
Zhou Li Mji wa Xintai, Mkoa wa Shandong
Wakati fulani kitambo, tulihitaji kuzichora wilaya katika eneo letu, na kwa msingi wa kanuni zetu kwa ajili ya uteuzi wa viongozi, kulikuwa na ndugu mmoja wa kiume aliyekuwa mtaradhia mzuri kiasi. Nilitayarisha kumchagua kuwa kiongozi wa wilaya. Siku moja nilipokuwa nikizungumza na ndugu huyu, alitaja kwamba alihisi kuwa nilikuwa mwenye nguvu sana katika kazi yangu, mkali sana, na kwamba katika mkusanyiko pamoja nami hapakuwa na furaha nyingi…. Niliposikia jambo hili, nilihisi kuwa nilikuwa nimedunishwa. Nilihisi vibaya sana; mara moja nikakuza maoni fulani ya ndugu huyu, na sikukusudia tena kumchagua kuwa kiongozi wa wilaya.

Jumanne, 12 Novemba 2019

Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa
Ding Ning Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong
Katika siku chache zilizopita, kanisa limepanga mabadiliko katika kazi yangu. Nilipopokea wajibu huu mpya, niliwaza, “Ninahitaji kuchukua fursa hii ya mwisho kuita mkutano na ndugu zangu wa kiume na wa kike, niongee nao wazi juu ya mambo, na niwaache na picha nzuri.” Kwa hiyo, nilikutana na mashemasi kadhaa, na kufikia mwisho wa wakati wetu pamoja, nikasema, “Nimeulizwa kuondoka hapa na kuenda kwa kazi tofauti. Natumaini mtamkubali kiongozi ambaye anakuja kuchukua nafasi yangu na kufanya kazi pamoja naye kwa moyo mmoja na wazo moja.” Mara tu waliposikia nikisema maneno haya, baadhi ya dada waliokuwepo walipauka, na tabasamu zikawatoka nyusoni. Baadhi yao walishika mikono yangu, baadhi yao walinikumbatia, na hali wakilia walisema, “Huwezi kutuacha! Huwezi kututupa kando na kupuuza mahitaji yetu! …” Dada wa familia mwenyeji hasa hakuwa radhi kuniruhusu niende. Aliniambia, “Ni vizuri sana kwamba uko hapa pamoja nasi. Wewe ni mtu ambaye anaweza kuvumilia shida, na wewe ni mzuri katika kushirikiana juu ya ukweli. Bila kujali ni wakati upi tulikuhitaji, daima ulikuwa hapo kutusaidia kwa uvumilivu. Kama ukienda, tutafanya nini? …” Kwa kuona kusita kwao kutengana nami, moyo wangu ulijaa furaha na ridhaa. Niliwafariji kwa maneno haya: “Mtegemeeni Mungu. Nitakapoweza, nitarudi na kuwatembelea….”

Jumatatu, 11 Novemba 2019

Hakuna Utendewaji Maalum katika Kanisa

Hakuna Utendewaji Maalum katika Kanisa

Liu Xin Mji wa Liaocheng, Mkoa wa Shandong
Baada ya kumfuata Mungu kwa miaka hii, nilikuwa nikitekeleza wajibu wangu mbali na nyumbani na nilihisi kuwa nilikuwa nimevumilia mateso na kulipa gharama fulani, kwa hiyo nilianza kuyategemea mapato yangu ya zamani na kuringia ukubwa wangu. Nilipowaona watu kanisani waliotolewa kutoka katika vyeo vyao, na kutumwa nyumbani kufanya ibada zao za kiroho na kujiwazia, kwa sababu walikuwa wazembe katika kutekeleza wajibu wao, na walikatiza na kuharibu kazi ya kanisa, niliwaza: Nimeondoka nyumbani kwa miaka mingi. Katika hali hii, kanisa hakika litanitunza. Hata nisipofanya kazi yangu vizuri hawatanituma nyumbani. Si zaidi ya hayo wataniondoa tu na kunielekeza kufanya kazi nyingine. Kutokana na kufikiri kama huko, sikuwa na mzigo wowote kamwe katika kazi yangu. Nilipuuza kila kitu, na hata nikaiona kazi ya injili kama mzigo, daima nikiishi katika matatizo na visingizio. Hata kama nilihisi moyo wangu kama umeshutumiwa na dhamira yangu kulaumiwa kwa sababu nilimwia Mungu mengi zaidi kupitia kwa tabia yangu ya uzembe, na kwamba ningeondoshwa siku moja, bado tu nilitangatanga pamoja na fikira ya kutumaini kupata bahati zaidi, nikipoteza wakati wa siku zangu kwa kuzembea katika kanisa.

Jumapili, 10 Novemba 2019

Si Rahisi Kwako kwa Hakika Kujijua Mwenyewe

Si Rahisi Kwako kwa Hakika Kujijua Mwenyewe
Zhang Rui Mji wa Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang
Niliona katika maneno ya Mungu kwamba Mungu anawapenda watu waaminifu na anawachukia watu wadanganyifu, na ni watu wanyofu tu watakaopata sifa Zake. Kwa hiyo, nilitaka kuwa mtu mnyofu, kwa utambuzi kufanya mazoezi ya kuzungumza kwa usahihi, kuwa bila upendeleo na wa busara, na kutafuta ukweli kutoka kwa mambo ya hakika wakati wa kutoa taarifa juu ya masuala. Katika kazi yangu, kama iwe ni kosa au upungufu, mimi nililielezea kwa undani kwa kiongozi. Pia kwa utambuzi niliuchangua na kuufichua upotovu wangu mwenyewe. Kila wakati nilipoweka hili katika matendo, nilihisi kuwa nilikuwa nimepitia mabadiliko fulani na nilipata mfano kidogo wa kuwa mtu mnyofu.

Jumamosi, 9 Novemba 2019

Huyu Ni Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

Huyu Ni Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli
Moran Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Tangu nilipokuwa mtoto, siku zote nilishikiza umuhimu mkubwa kwa jinsi watu wengine walivyoniona na ukadiriaji wao kwangu. Ili niweze kupata sifa kutoka kwa wengine kwa kila kitu nilichokifanya, sikubishana na yeyote asilani wakati wowote kitu chochote kilichoibuka, ili kuepuka kuharibu picha nzuri watu wengine walikuwa nayo kwangu. Baada ya kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, niliendelea kwa njia hii, nikizingatia kwa kila njia iwezekanayo picha nzuri ambayo ndugu zangu wa kiume na wa kike walikuwa nayo kwangu. Hapo awali, wakati nilipokuwa ninasimamia kazi, kiongozi wangu mara nyingi angesema kwamba utendaji wangu ulikuwa kama “bwana ndiyo,” wala sio utendaji wa mtu ambaye huweka ukweli katika vitendo. Sikuathiriwa nalo asilani, lakini kwa kinyume kama watu wengine walinifikiria kuwa mtu mzuri, basi nilihisi kuridhika.

Ijumaa, 8 Novemba 2019

Umuhimu wa Uratibu katika Huduma

Umuhimu wa Uratibu katika Huduma
Mei Jie Jijini Jinan, Mkoani Shandong
Hivi karibuni kanisa lilitoa mpangilio wa kazi likihitaji viongozi wa kanisa katika ngazi zote kuanzisha mbia (mfanyikazi mwenza kufanya kazi pamoja nao). Wakati huo, nilifikiri kwamba huu ulikuwa mpangilio mzuri. Nilikuwa wa ubora wa tabia wa chini na nilikuwa na kazi nyingi; kwa kweli nilihitaji mbia wa kunisaidia kukamilisha kila aina ya kazi kanisani.

Alhamisi, 7 Novemba 2019

Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu
Wuzhi Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 2006, nilinyang’anywa cheo changu kama kiongozi na nikarudishwa nilikotoka kwa sababu nilifikiriwa kuwa “bwana ndiyo” sana. Niliporejea mara ya kwanza, nilitumbukia ndani ya kikalibu cha mateso na maumivu makubwa. Sikuwahi kufikiri kwamba baada ya miaka mingi ya uongozi mambo yangeharibika kwa sababu ya kuwa “bwana ndiyo.” Huu ulikuwa ndio mwisho kwangu, nilidhani, kila mtu aliyenijua angejua juu ya kushindwa kwangu na ningefanywa kama mfano mbaya katika kanisa. Ningewezaje kukabiliana na wengine baada ya haya yote? Jinsi nilivyozidi kufikiria, ndivyo nilivyozidi kuwa hasi, mpaka hatimaye nikapoteza imani ya kuendelea kutafuta ukweli. Hata hivyo, wakati nilifikiri juu ya sadaka zote na matumizi niliyoyatoa katika miaka hii michache iliyopita, sikuweza kushawishika kuondoka Na nikafikiria: “Kama nikijimaliza kabisa na kukubali kushindwa, si jitihada zangu zote zitakuwa bure? Si watu watanidunisha hata zaidi? Siwezi kuruhusu hilo lifanyike! Ni lazima nijitetee na nisiwaache wengine waniangalie kwa dharau. Sasa, bila kujali ni jinsi gani ninavyopaswa kujitahidi, ni makosa mangapi yanayonipata, ni lazima nifanye haraka—siwezi kuondoka nusu njia! Almradi ninakumbuka mafundisho ya kushindwa na kuzingatia kutafuta ukweli, labda siku moja naweza kuwa kiongozi tena.” Mawazo haya yakiwa katika kumbukumbu, uhasi wote na huzuni zilififia na nilihisi nguvu iliyofanywa upya katika ukimbizaji wangu.

Jumatano, 6 Novemba 2019

Kumshinda Shetani katika Mapambano

Kumshinda Shetani katika Mapambano
Chang Moyang Mjini Zhengzhou, Mkoani Henan
Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “Ukiasi dhidi ya mwili wako, bila shaka kutakuwa na vita ndani yako. Shetani atajaribu kufanya watu kuifuata, atajaribu kuwafanya wafuate dhana za kimwili na kutekeleza maslahi ya kimwili—ila maneno ya Mungu yatawapa nuru watu na kuwaangazia kwa ndani, na wakati huu itakuwa juu yako ikiwa utamfuata Mungu au utamfuata Shetani. Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie (“Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila mara niliposoma kifungu hiki kutoka maneno ya Mungu, ningetafakari kuhusu yafuatayo: Je, kutenda ukweli ni kugumu kiasi hicho? Wakati watu hawauelewi ukweli, hawawezi kuutenda. Mara wanapouelewa, kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu hakutatosha? Je kungeweza kuwa kwenye uzito kweli kama “ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona”? Haikuwa hadi baadaye, kupitia uzoefu wangu halisi, kuwa niliona kwamba kutenda ukweli si rahisi kwa kweli. Aliyosema Mungu yanalingana kabisa na ukweli; hayajatiwa chumvi hata kidogo.

Jumanne, 5 Novemba 2019

Huwezi Kumtambua Mtu kwa Kuonekana Kwake

Huwezi Kumtambua Mtu kwa Kuonekana Kwake
Yang Rui Mji wa Yuci, Mkoa wa Shanxi
Moyoni mwangu, niliamini kuwa babangu alikuwa mtu mzuri. Lakini siku moja, nilisikia kwa ghafla kuwa baba yangu alifukuzwa kutoka kanisani. Nilishangaa kabisa wakati huo na sikuweza kuelewa. Katika moyo wangu, baba yangu alikuwa ndiye mtu mkuu mno duniani. Ingawa ana hasira mbaya, alitutunza sana sisi ndugu wa kike na kamwe hakutupiga au kutukemea. Licha ya harakati za familia yetu, hangeturuhusu tuone hasira bila kujali ni shida kiasi gani angepaswa kustahimili. Baada familia yetu yote kuikubali kazi ya Mungu, baba yangu alikuwa aidha amilifu katika kutekeleza wajibu wake, na mara nyingi alitutia moyo kutimiza wajibu wetu vizuri. Ingawa baba yangu alikuwa mkali kidogo wakati mwingine, mara tu palipokuwa na wajibu wa kutimiza, bila kujali upepo na mvua au kiwango cha ugumu, angetafuta njia ya kulikamilisha hilo. Mtu mwema kama huyo angewezaje kufukuzwa? Ikiwa hawezi kupokea wokovu, basi ni nani anayeweza? Hali hiyo iliujaza moyo wangu hasira na mgongano, kwa sababu nilihisi kanisa halikumtendea baba yangu haki. Ingawa sikulisema, niliona vigumu kuutuliza moyo wangu na niliumia vibaya katika mateso.

Jumatatu, 4 Novemba 2019

Kuzing’uta Pingu za Roho

Kuzing’uta Pingu za Roho
Wu Wen Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Nilikuwa mtu dhaifu na mwenye tabia nyepesi kuhisi. Wakati sikumwamini Mungu, mara kwa mara ningejihisi mwenye huzuni na masikitiko kutokana na mambo yaliyokuja katika maisha. Kulikuwa na nyakati nyingi kama hizi, na siku zote nilihisi kwamba maisha yangu yalikuwa magumu; hapakuwa na furaha, hamkuwa na ridhisho moyoni mwangu ya kuzungumzia. Uchungu huu ulikuwa tu kama pingu zilizonifunga kabisa kila mara, zikinifanya niwe mwenye huzuni. Ilikuwa tu baada kumwamini Mwenyezi Mungu ndipo nilipata kiini cha matatizo ndani ya maneno ya Mungu na nikapata uhuru polepole.

Jumapili, 3 Novemba 2019

Ufahamu Kiasi Kuhusu Kuokolewa

Ufahamu Kiasi Kuhusu Kuokolewa
Lin Qing Jijini Qingzhou, Mkoa wa Shandong
Kwa miaka hii mingi ya kumfuata Mungu, nimeacha familia yangu na raha za mwili, na nimekuwa na shughuli nyingi siku nzima nikitimiza wajibu wangu kanisani. Kwa hiyo niliamini: Mradi tu nisiache kazi yangu katika kanisa, nisimsaliti Mungu, nisiache kanisa, na kumfuata Mungu hadi mwisho, nitahurumiwa na kuokolewa na Mungu. Niliamini pia kuwa nilikuwa nikitembea katika njia ya wokovu na Mungu, na yote niliyokuwa niyafanye ni kumfuata Yeye mpaka mwisho.

Ijumaa, 1 Novemba 2019

Roho Mtakatifu Hufanya Kazi kwa Njia Yenye Maadili

Roho Mtakatifu Hufanya Kazi kwa Njia Yenye Maadili
Qin Shuting Jijini Linyi, Mkoani Shandong
Kwa muda fulani, ingawa sikuwa nimeacha kula na kunywa manen ya Mungu, sikuhisi mwanga kamwe. Nilikuwa nimeomba kwa Mungu kwa ajili ya hili lakini, baadaye, bado sikuwa nimepata nuru. Hivyo niliwaza, “Kuna wakati wa Mungu kumpa kila mwanadamu nuru, kwa hivyo hakuna maana ya kuiharakisha.” Baadaye, nilishika amri na kula na kunywa maneno ya Mungu bila wasiwasi, nikingoja kwa “subira” kutoa nuru kwa Mungu.

Kuibuka Kutoka Kwenye Ukungu

Kuibuka Kutoka Kwenye Ukungu
Zhenxi Jijini Zhenzhou, Mkoani Hena
Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu mipangilio ya kanisa. Ningetii ikiwa ilinifaa, lakini iwapo haingenifaa ningechagua iwapo ningetii au la. Hili lilisababisha kukiuka sana mipangilio ya kazi wakati wa kutimiza wajibu wangu. Nilifanya jambo langu mwenyewe na kuichukiza tabia ya Mungu, na hivyo baada ya hapo nilitumwa nyumbani. Baada ya miaka kadhaa ya kujitafakari, nilikuwa kwa kiwango fulani na maarifa ya asili yangu mwenyewe, lakini kuhusu kipengele cha ukweli ambacho ni kiini cha Mungu bado sikuwa na maarifa mengi. Baadaye, kanisa lilinipangia kusimamia kazi ya injili, nilianza kuwa na shaka kumhusu Mungu: Mimi ni mpotovu sana na pia nilikuwa nimeichukiza tabia ya Mungu. Ni kwa nini Mungu angenitumia mimi? Je, Ananidanganya? Je, nitaondolewa baada ya kudanganywa? Aa! Kwa kuwa kanisa lilinipa nafasi nitaitunza, hata kama ni lazima niwe mtenda huduma. Kuanzia wakati huo kuendelea, nilitimiza wajibu wangu nikiwa na akili kama hiyo, lakini bila kutafuta lengo la juu—kufanywa mkamilifu na Mungu.