Smiley face

Jumamosi, 14 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Majina na Utambulisho

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Kuhusu Majina na Utambulisho

Iwapo unataka kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu, lazima uijue kazi ya Mungu; lazima uijue kazi Aliyofanya awali (katika Agano Jipya na la Kale), na, zaidi ya hayo, lazima uijue kazi Yake ya leo. Ndiyo kusema, ni lazima uzitambue hatua tatu za kazi ya Mungu ya zaidi ya miaka 6,000. Ukiulizwa ueneze injili, basi hutaweza kufanya hivyo bila kuijua kazi ya Mungu. Watu watakuuliza yote kuhusu Biblia, na Agano la Kale, na nini Yesu alisema na kufanya wakati huo. Watasema, “Mungu wenu hajawaeleza haya yote? Kama Yeye (Mungu) hawezi kuwaeleza ni nini hasa yanayoendelea kwa Biblia, basi Yeye si Mungu; kama Anaweza, basi tumeamini.” Mwanzoni, Yesu alizungumzia sana Agano la Kale na wanafunzi Wake.

Ijumaa, 13 Oktoba 2017

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu

Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu.

Alhamisi, 12 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuujua Uhalisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuujua Uhalisi


Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. 

Jumatano, 11 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu  Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno


Mwenyezi Mungu alisema, Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu.

Umeme wa Mashariki | Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako


Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilamali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa.Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.

Kuhusu Biblia (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kuhusu Biblia (4)


Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. 

Jumanne, 10 Oktoba 2017

Kuhusu Biblia (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kuhusu Biblia (3)

Sio kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa kibinadamu, na ufasiri wa ajabu wa kibinadamu. 

Jumatatu, 9 Oktoba 2017

Kuhusu Biblia (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kuhusu Biblia (2)

Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika “Agano Jipya” linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka, uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye linta kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe).