Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuhusu-Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuhusu-Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 19 Novemba 2017

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I(Sehemu ya Tatu)


Mwenyezi Mungu alisema: Kisha, tutazungumzia hadithi ya Nuhu na namna ambavyo inahusiana na mada ya kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe.
Mnaona Mungu akimfanya nini Nuhu kwenye sehemu hii ya maandiko? Pengine kila mmoja aliyeketi hapa anajua kitu kuhusu hayo baada ya kusoma maandiko: Mungu alimfanya Nuhu kujenga safina, kisha Mungu akatumia gharika kuangamiza ulimwengu. 

Ijumaa, 10 Novemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu  Tamko la Kumi na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Mwenyezi Mungu alisema: Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao.

Alhamisi, 2 Novemba 2017

Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu


Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani. 

Jumamosi, 28 Oktoba 2017

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje


Mwenyezi Mungu alisema: Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

Ijumaa, 27 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake


Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. Kwa sasa hakuna hata mmoja wenu aliye mkamilifu. Wakati mwingine mnaweza kutekeleza aina moja ya kazi na wakati mwingine mnaweza kutekeleza mbili; mradi tu mnampa Mungu nguvu zenu zote na kujitoa kwa ajili Yake, hatimaye mtafanywa wakamilifu na Mungu. 

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho


Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili. Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo.

Jumatano, 18 Oktoba 2017

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu


Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako. Ukifika mahali hapo utafurahia kujua imani katika Mungu ni nini, namna ya kumwamini Mungu vizuri, na kile unachopaswa kufanya ili kutenda mambo kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu.

Jumapili, 15 Oktoba 2017

Neno la Mungu Humwongoza Mtu Kuishi Maisha Mapya | Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana



Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana
I
Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaimba nyimbo za sifa kubwa Kwako.
Wewe hutuleta katika maisha ya ufalme.
Sisi watu wa ufalme tu katika karamu yako ya fahari,
tukifurahia maneno Yako, tukitakaswa upotovu wetu.
Neno Lako hutuongoza na sisi kukufuata kwa karibu.

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu


Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mnamwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka.Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? 

Ijumaa, 13 Oktoba 2017

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu

Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu.

Alhamisi, 12 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuujua Uhalisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuujua Uhalisi


Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. 

Jumatano, 11 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu  Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno


Mwenyezi Mungu alisema, Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu.