Smiley face

Jumatatu, 22 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu, Maneno ya Mungu

Ni njia gani ambayo Mungu hutumia kumkamilisha mwanadamu? Ni vipengele vipi vinavyojumuishwa? Je, uko tayari kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unajua nini kuhusu maswali haya? Kama huwezi kuzungumzia maarifa kama haya, basi hii inaonyesha kwamba bado huijui kazi ya Mungu na hujapatiwa nuru katu na Roho Mtakatifu. Binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa. Wanaweza tu kupokea kiasi kidogo cha neema ili kufurahia kwa muda mfupi na haiwezi kuendelezwa kwa kipindi kirefu. Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu.  Baadhi wanaweza kutoshelezwa na amani na furaha ya mwili, maisha yenye furaha bila ya dhiki au msiba, huku wakiishi kwa amani na familia zao bila ya mapigano au ugomvi. Wanaweza hata kuamini kwamba hii ni baraka ya Mungu, lakini kwa kweli, ni neema ya Mungu tu. Hamwezi kutosheka tu kwa kufurahia neema ya Mungu. Kufikiria kwa aina hii ni kuchafu mno. Hata ukisoma neno la Mungu kila siku, uombe kila siku, na roho yako ihisi furaha na amani halisi, ilhali mwishowe huwezi kuzungumzia maarifa yoyote ya Mungu na kazi Yake au hujapata uzoefu wa mambo kama hayo, na haijalishi ni kiasi gani cha neno la Mungu ambacho umekula na kunywa, ukihisi tu amani na furaha katika roho yako na kwamba neno la Mungu ni tamu mno kiasi kwamba haliwezi kulinganishwa na kingine chochote, kana kwamba huwezi kulifurahia ukatosheka, lakini huna uzoefu halisi na huna hakika yoyote na neno la Mungu, basi ni nini unachoweza kupokea kutoka kwa aina hii ya imani katika Mungu? Kama huwezi kuishi kwa kudhihirisha kiini cha neno la Mungu, kula na kunywa kwako na maombi vyote vinahusu dini. Basi binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa na hawezi kupatwa na Mungu. Wale wote waliopatwa na Mungu ni wale wanaofuatilia ukweli. Kile ambacho Mungu hufaidi si mwili wa binadamu wala miliki zake, lakini sehemu iliyo ndani yake inayomilikiwa na Mungu. Ndiyo maana Ninasema kwamba Mungu huukamilisha moyo wa binadamu wala si mwili wake, ili moyo wa binadamu uweze kupatwa na Mungu. Kwa maneno mengine, kiini cha kusema kwamba Mungu humkamilisha mwanadamu ni kwamba Mungu huukamilisha moyo wa mwanadamu ili uweze kumgeukia Mungu na kumpenda Yeye.

Mwili wa binadamu hufa. Haifaidi chochote kwa Mungu kuupata mwili wa binadamu, kwani ndio ule ule ambao bila shaka huoza. Hauwezi kupokea urithi wa Mungu au baraka Zake. Kama Mungu anaupata tu mwili wa binadamu na kuuhifadhi mwili wa binadamu katika mfululizo huu, binadamu atakuwa katika mfululizo huu kwa jina tu, lakini moyo wa binadamu ungemilikiwa na Shetani. Basi binadamu hangeweza tu kuwa maonyesho ya Mungu, bali badala yake angekuwa mzigo Wake. Kwa hivyo Mungu kuchagua binadamu hakungekuwa na maana. Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu. Binadamu wa aina hii tu ndiye anayestahili kurithi baraka hizi alizofadhiliwa na Mungu:


1. Kupokea upendo mzima wa Mungu.

2. Kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu katika kila kitu.

3. Kupokea mwongozo wa Mungu, kuishi chini ya mwangaza wa Mungu, na kupatiwa nuru na Mungu.

4. Kuishi kwa kudhihirisha taswira inayopendwa na Mungu hapa ulimwenguni; kumpenda Mungu kwa kweli kama vile Petro alivyofanya, kusulubishwa kwa sababu ya Mungu na kustahili kufa kwa kuufidia upendo wa Mungu; kuwa na utukufu sawa na Petro.

5. Kupendwa, kuheshimiwa, na kuvutiwa na wote ulimwenguni.

6. Kushinda utumwa wote wa kifo na Kuzimu, kutoipatia fursa yoyote kazi ya Shetani, kumilikiwa na Mungu, kuishi ndani ya roho safi na changamfu, na kutokuwa na hisia zozote za uchovu.

7. Kuwa na hisia isiyoelezeka ya msisimko na furaha siku zote katika maisha yako yote, ni kana kwamba ameona kuja kwa siku ya utukufu wa Mungu.
8. Kupokea utukufu pamoja na Mungu, na kuwa na sura inayofanana na watakatifu wapendwa wa Mungu.

9. Kuwa kile ambacho Mungu anapenda zaidi ulimwenguni, yaani, mwana mpendwa wa Mungu.

10. Kubadilisha maumbile na kupaa juu pamoja na Baba kwenye mbingu ya tatu, na kuuzidi mwili.

Wale tu wanaoweza kurithi baraka za Mungu ni wale waliokamilishwa na Mungu na kupatwa na Mungu. Je, umefaidi chochote? Mungu amekukamilisha hadi kiwango gani? Mungu hamkamilishi binadamu bila mpango. Kunayo masharti na matokeo dhahiri yanayoweza kuonekana na binadamu. Si jinsi mwanadamu anavyoamini, kwamba mradi tu awe na imani katika Mungu, anaweza kukamilishwa na kupatwa na Mungu, na anaweza kupokea hapa ulimwenguni baraka na urithi wa Mungu. Mambo kama haya ni magumu mno, na hata zaidi inapohusu kubadilika kwa taratibu. Kwa sasa, kile ambacho mnafaa kutafuta kimsingi ni kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, na kukamilishwa na Mungu kupitia kwa watu wote, mambo yote na vitu vyote ambavyo mnakumbwa navyo, ili mambo zaidi ya kile Mungu Alicho yatashirikishwa ndani yenu. Lazima kwanza mpokee urithi wa Mungu ulimwenguni kabla ya kustahili kurithi baraka nyingi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu. Mambo yote haya ndiyo ambayo mnafaa kutafuta na ambayo kwanza mnafaa kuelewa. Zaidi unavyotafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, ndivyo utakavyoweza kuona mkono wa Mungu zaidi katika mambo yote, na hivyo kutafuta kwa bidii kuingia katika hali ya neno la Mungu na uhalisia wa neno Lake kupitia mitazamo tofauti na katika mambo tofauti. Huwezi kutosheka na hali hasi kama kutotenda dhambi tu, au kutokuwa na dhana, kutokuwa na filosofia ya maisha, na kutokuwa na hiari ya binadamu. Mungu humkamilisha mwanadamu kwa njia tofauti, na inawezekana katika mambo yote kwako kukamilishwa hatimaye. Huwezi tu kukamilishwa kwa kuzingatia mambo halisi, lakini pia mambo hasi, na hivyo kukuboresha wewe. Kila siku kunazo fursa za kukamilishwa na muda wa kupatwa na Mungu. Baada ya kipindi cha kupitia mambo kama haya, utabadilika pakubwa. Utaweza sasa kimaumbile kufaidi utambuzi katika mambo mengi ambayo hukuyaelewa awali; bila ya kuhitaji wengine kukufunza, bila kujua, utaweza kufahamishwa na Mungu, ili uweze kuwa na fahamisho katika mambo yote na mambo yote utakayopitia yatakuwa mengi. Mungu atakuongoza wewe ili usije ukapotoka kwa vyovyote vile. Kisha utawekwa wazi kwenye njia ya kufanywa kuwa mtimilifu na Yeye.

Kukamilishwa na Mungu hakuwezi kuwa kukamilishwa kupitia kwa kula na kunywa neno la Mungu tu. Aina hii ya uzoefu inaegemea upande mmoja sana na haijumuishi pande zote; inamzuia binadamu katika uwezo mdogo sana. Kwa hiyo, binadamu hukosa chakula cha kiroho kinachohitajiwa zaidi. Kama mtapenda kukamilishwa na Mungu, lazima mjifunze kupitia mambo yote na kupatiwa nuru katika yote mnayoyapitia. Kila unapokumbwa na kitu, kiwe kizuri au kibaya, unafaa kufaidi kutoka katika kitu hicho na hakifai kukufanya ukae tu. Haijalishi ni nini, unafaa kuweza kukitilia maanani kwa kusimama upande wa Mungu, na wala si kuchambua au kukisoma kutoka kwa mtazamo wa binadamu (huku ni kupotoka katika hali unayopitia). Kama hivi ndivyo utakavyopitia mambo katika maisha yako, basi moyo wako utazidiwa na mizigo ya maisha yako; utaishi siku zote katika mwanga wa uso wa Mungu na hutaweza kupotoka kwa urahisi katika matendo yako. Binadamu wa aina hii ana matarajio makubwa. Kunazo fursa nyingi za kukamilishwa na Mungu. Yote haya yanategemea kama ni nyinyi ndinyi mnaompenda Mungu kwa kweli na kama mnalo azimio la kukamilishwa na Mungu, kupatwa na Mungu, na kupokea baraka na urithi Wake. Haitakubalika kwenu kuwa na azimio tu. Lazima muwe na maarifa mengi, vinginevyo siku zote mtapotoka katika matendo yenu. Mungu yuko radhi kumkamilisha kila mmoja wenu. Kama ilivyo sasa, ingawa wengi tayari wamekubali kazi ya Mungu kwa muda mwingi, wamejiwekea mipaka ya kufurahia tu neema ya Mungu na wako radhi tu kupokea tulizo fulani la mwili kutoka Kwake. Hawako radhi kupokea ufunuo zaidi na wa kiwango cha juu zaidi, hali ambayo inaonyesha kwamba moyo wa binadamu ungali nje siku zote. Ingawa kazi ya binadamu, huduma yake, na moyo wake wa upendo kwa Mungu vyote vina kasoro chache zaidi, kuhusiana na kiini cha binadamu na kufikiria kwake kusiko na nuru, binadamu bado daima hutafuta amani na furaha ya mwili, na huwa hajali masharti na makusudio Mungu ya katika kumkamilisha binadamu ni yapi. Kwa hivyo maisha ya wengi yangali machafu na yaliyooza, bila dalili zozote za mabadiliko. Yeye hasa haichukilii imani katika Mungu kama suala lenye umuhimu. Badala yake, ni kana kwamba anayo imani tu kwa ajili ya binadamu mwengine, akitenda bila ukweli au kujitolea, na akiishi tu kwa vile viwango vya chini zaidi vya maisha, akiendelea kuwepo tu bila kusudi lolote. Wachache ndio wanaotafuta kuingia ndani ya neno la Mungu katika mambo yote, huku wakifaidi mambo mengi ya kusitawisha, wakiwa wenye utajiri mkubwa zaidi katika nyumba ya Mungu siku hii, na wakipokea baraka zaidi za Mungu. Kama unatafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote na unaweza kurithi ahadi za Mungu hapa ulimwenguni; kama unatafuta kupatiwa nuru na Mungu katika mambo yote na huiruhusu miaka kuyoyoma tu huku ukiwa umezubaa, hii ndiyo njia inayostahili kuingia kwa bidii. Ni kupitia kwa njia hii tu ndipo unastahili na unafaa kukamilishwa na Mungu. Wewe ndiwe kweli unayetafuta kukamilishwa na Mungu? Wewe ndiwe kweli uliye mwenye bidii katika mambo yote? Unayo roho sawa ya upendo kwa Mungu kama Petro? Unayo hiari ya kumpenda Mungu kama Yesu alivyofanya? Umekuwa na imani katika Yesu kwa miaka mingi; umeona namna Yesu alivyompenda Mungu? Yesu ndiye kweli unayemwamini? Unamwamini Mungu wa matendo wa siku hii; umeona namna ambavyo Mungu wa matendo katika mwili anavyompenda Mungu kule mbinguni? Unayo imani katika Bwana Yesu Kristo; hiyo ni kwa sababu kusulubishwa kwa Yesu ili kuwakomboa wanadamu na miujiza Aliyoifanya vyote kwa ujumla ni ukweli unaokubaliwa. Hata hivyo, imani ya mwanadamu haitokani na maarifa na ufahamu wa kweli wa Yesu Kristo. Unaamini tu katika jina la Yesu lakini huna imani katika Roho Wake, kwani hujali kuhusu namna Yesu alivyompenda Mungu. Imani yako katika Mungu ni changa sana. Ingawa umekuwa na imani katika Yesu kwa miaka mingi, hujui namna ya kumpenda Mungu. Je, jambo hili halikufanyi kuwa mjinga mkubwa zaidi kote ulimwenguni? Hii inaonyesha kwamba kwa miaka mingi umekila chakula cha Bwana Yesu Kristo bure. Simpendi tu binadamu wa aina hii, Naamini kwamba pia Bwana Yesu Kristo, ambaye unamwabudu, hampendi. Mtu wa aina hii anawezaje kukamilishwa? Huaibiki? Huhisi aibu? Bado unao ujasiri wa kumkabili Bwana Yesu Kristo? Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya maneno Yangu?


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni