Mwenyezi Mungu alisema, Ninyi nyote mara nyingi mmepata uzoefu wa hali ya kuwa katika mkutano, na kuhisi kana kwamba huna chochote cha kuhubiri kuhusu—hatimaye unajilazimisha na unasema kitu cha juu juu. Unajua vizuri kuwa maneno haya ya juu juu ni kanuni, lakini unahubiri kuyahusu hata hivyo, na mwishowe unahisi kuwa huna shauku, na watu chini yako wanasikiliza na wanahisi kuwa yanachosha sana—je hilo halijafanyika?
Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu.
NYUMBANI
Usomaji wa Maneno ya Mwenyezi Mungu
Filamu za Injili
Kwaya za Injili
Maisha ya Kanisa—Mfululizo wa Maonyesho Mbalimbali
Video za Nyimbo na Ngoma
Msururu wa MV za Ufalme
Video za Nyimbo za Dini
Filamu za Maisha ya Kanisa
Filamu za Uzoefu wa Mateso
Kufunua Mfululizo wa Video za Ukweli
Sehemu za Filamu
Aina za Dondoo za Video
Inaonyesha machapisho ya hoja yaliyopangwa kwa uhusiano ukweli. Panga kwa tarehe Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho ya hoja yaliyopangwa kwa uhusiano ukweli. Panga kwa tarehe Onyesha machapisho yote
Jumamosi, 9 Desemba 2017
Jumamosi, 11 Novemba 2017
Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata
1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La
Mwenyezi Mungu alisema: Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli.
Ijumaa, 12 Januari 2018
Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini?
Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini?
Xiaohe Mji wa Puyang, Mkoa wa Henan
Hapo awali, kila wakati niliposoma maneno yaliyofichuliwa na Mungu kuhusu jinsi watu hawakubali ukweli, sikuamini kwamba maneno hayo yangetumika kwangu. Nilifurahia kula na kunywa neno la Mungu na kuwasiliana kuhusu neno la Mungu, na niliweza kukubali na kukiri kila kitu ambacho Mungu amesema kuwa ukweli—bila kujali jinsi kilivyoumiza moyo wangu au jinsi hakikuambatana na mawazo yangu. Aidha, bila kujali kiwango cha dosari kaka na dada zangu wangeonyesha, ningekikiri na kukikubali. Sikutafuta kujitetea mwenyewe, hivyo nilidhani kwamba nilikuwa mtu ambaye kwa hakika alikubali ukweli.
Alhamisi, 5 Desemba 2019
Kukubali Ukweli kwa Hakika Ni Nini
Xiaohe Mji wa Puyang, Mkoa wa Henan
Hapo awali, kila wakati niliposoma maneno yaliyofichuliwa na Mungu kuhusu jinsi watu hawakubali ukweli, sikuamini kwamba maneno hayo yangetumika kwangu. Nilifurahia kula na kunywa neno la Mungu na kuwasiliana kuhusu neno la Mungu, na niliweza kukubali na kukiri kila kitu ambacho Mungu amesema kuwa ukweli—bila kujali jinsi kilivyoumiza moyo wangu au jinsi hakikuambatana na mawazo yangu. Aidha, bila kujali kiwango cha dosari kaka na dada zangu wangeonyesha, ningekikiri na kukikubali. Sikutafuta kujitetea mwenyewe, hivyo nilidhani kwamba nilikuwa mtu ambaye kwa hakika alikubali ukweli. Ni watu wale tu ambao hasa walikuwa wenye kiburi na majivuno na waliokuwa na mawazo kuhusu neno la Mungu, ambao hawangekiri kuwa neno la Mungu ni ukweli ndio ambao hawangekubali ukweli. Nilikuwa kwa kawaida nikifikiri hivi hadi siku moja nilipokuwa nikisikiliza “Ushirika na Mahubiri kuhusu Kuingia kwa Maisha”, ndipo nilipoelewa kweli kilichomaanisha kukubali ukweli.
Jumanne, 10 Desemba 2019
Uzoefu wa Kutenda Ukweli
Hengxin Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan
Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia “Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha,” jambo ambalo lilinielekeza kuelewa kwamba ni wale tu wanaotenda ukweli wanaoweza kupata ukweli na hatimaye kuwa wale ambao wanaomiliki ukweli na ubinadamu hivyo kupata kibali cha Mungu. Kuanzia hapo kwendelea, kwa makusudi nilifanya jitihada za kuunyima mwili wangu na kutenda ukweli katika maisha yangu ya kila siku. Wakati fulani baadaye, nilitambua kwa furaha kwamba ningeweza kutenda ukweli kiasi. Kwa mfano, siku za nyuma niliogopa kuonyesha upande wangu mwovu kwa wengine. Sasa kwa makusudi nilikuwa wazi na ndugu wa kiume na wa kike, nikichangua tabia yangu potovu. Kabla, wakati nilipopogolewa na kushughulikiwa, ningetoa udhuru na kukwepa wajibu. Sasa nilifanya jitihada makusudi kujikana badala ya kujaribu kuhalalisha tabia yangu mbaya. Katika siku za nyuma, nilipopata msuguano na wenzangu kazini, nilikuwa na mawazo finyu, uchwara na wa kuelekea kununa. Sasa nilipokabiliwa na hali hizo ningeunyima mwili wangu na kutumia stahamala na subira na wengine. … Kila wakati nilipofikiria maendeleo yangu katika kutenda ukweli, ningejihisi kuwa na furaha mno. Nilidhani kuwa uwezo wangu wa kutenda ukweli kiasi ulimaanisha kwamba nilikuwa mweledi halisi wa ukweli. Kwa njia hii, bila kujua nikawa mwenye maringo na wa kujipongeza.
Jumamosi, 14 Septemba 2019
Matamshi ya Mungu|Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana
Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo yote husika na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kwa kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inapozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi.
Jumamosi, 28 Oktoba 2017
Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli
Mwenyezi Mungu alisema: Katika matendo, amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri. Kutenda ukweli na kuzishika amri sio vitendo vinavyopingana, lakini badala yake vinahusiana.
Jumamosi, 20 Januari 2018
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana
![]() |
| Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio Tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana |
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana
Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo hayo yote na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani.
Jumatano, 6 Desemba 2017
Sura ya 42. Kwa Kutafuta Ukweli tu Ndio Unaweza Kupata Mabadiliko katika Tabia Yako
Mwenyezi Mungu alisema, Kwa kutafuta ukweli tu ndipo utapata mabadiliko katika tabia yako: Hili ni jambo unalofaa kulielewa na kulielewa vizuri kabisa. Usipoelewa ukweli vya kutosha, utateleza kwa urahisi na kupotoka. Kutafuta kukua katika maisha lazima utafute ukweli katika kila kitu. Haijalishi suala gani laweza kutokea, lazima utafute kukumbana nalo katika njia inayopatana na ukweli, kwa sababu ukikumbana nayo kwa njia isiyo safi kabisa, basi unaenda kinyume na ukweli. Chochote ufanyacho, lazima kila wakati ufikirie thamani yake.
Sura ya 44. Kuutoa Ukweli Ndiyo Njia ya Kweli ya Kuwaongoza Wengine
Mwenyezi Mungu alisema, Ikiwa mnataka kufanya kazi nzuri katika kuwaongoza wengine na kuhudumu kama mashahidi wa Mungu, la muhimu zaidi, lazima uwe na ufahamu wa kina wa kusudi la Mungu katika kuwaokoa watu na kusudi la kazi Yake. Lazima uyaelewe mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake mbalimbali ya watu. Unapaswa kuwa mwenye utendaji katika juhudi zenu; upitie tu kiasi unachoelewa na kuwasiliana tu kile unachokijua. Usijisifu, usitie chumvi, na usiseme maneno yasiyopaswa. Ukitia chumvi, watu watakuchukia na utahisi mwenye kushutumiwa baadaye; hili ni jambo lisilofaa kabisa.
Alhamisi, 7 Desemba 2017
Sura ya 41. Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu
Je, ni vitu vipi vya asili ya mwanadamu? Unajua tu kuhusu upotovu wa mwanadamu, uasi, upungufu, dosari, fikra, na dhamira, lakini huwezi kugundua sehemu za ndani za asili ya mwanadamu—unafahamu tu safu ya nje, lakini huwezi kugundua chanzo chake. Baadhi hata hufikiri haya mambo ya juu kuwa ni asili ya mwanadamu, wakisema, “Tazama, ninaelewa asili ya mwanadamu; ninatambua ufidhuli wangu. Je, hiyo si asili ya mwandamu?” Je, haitoshi kuikubali kikanuni pekee? Ufidhuli ni kitu cha asili ya mwanadamu; huu ni ukweli kabisa.
Jumatano, 18 Julai 2018
Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo - Kupata Ahueni kwa Njia ya Kumwamini Mungu
Kupata Ahueni kwa Njia ya Kumwamini Mungu
Zhuanbian Mji wa Shanghai
Ingawa nilikuwa nikimfuata Mungu kwa miaka mingi, nilikuwa karibu sijafanya maendeleo yoyote na kuingia kwangu katika maisha, na hii ilinifanya nihisi kuwa na wasiwasi sana. Hasa wakati niliposikia rekodi ya mahubiri juu ya kuingia kwa maisha, na kusikia mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu akizungumza na ndugu wa kiume na wa kike waliokuwepo na kusikiliza mahubiri, nilihisi nikiwa nimejawa na wasiwasi nikimsikia akisema jambo kama hili, "Nyinyi sasa mnamwamini Mungu na mmeonja uzuri wa ukimbizaji wa ukweli.
Jumapili, 12 Novemba 2017
Sura ya 11. Kutatua Asili na Kutenda Ukweli
1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Mwenyezi Mungu alisema: Watu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli.
Jumamosi, 7 Desemba 2019
Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo
Fan Xing Mji wa Zhumadian, Mkoa wa Henan
Katika siku za nyuma, nilikuwa nimeunganishwa na dada mmoja kufanya kazi kwa wajibu fulani. Kwa sababu nilikuwa na majisifu na mwenye kiburi na sikutafuta ukweli, nilikuwa na mawazo kiasi ya kabla kuhusu dada huyu ambayo niliweka moyoni mwangu daima na sikuzungumza waziwazi naye. Tulipotengana, sikuwa nimeingia katika ukweli wa uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha. Baadaye, kanisa lilinipangia kufanya kazi na dada mwingine nami nikaweka azimio mbele ya Mungu: Kuanzia sasa kuendelea, sitatembea katika njia za kufeli. Nimejifunza mafundisho yangu na hivyo kwa sasa wakati huu bila shaka nitakuwa na mawasiliano ya wazi zaidi na dada huyu na kufikia uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha.
Jumatatu, 19 Novemba 2018
Umeme wa Mashariki | Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo
Fan Xing Mji wa Zhumadian, Mkoa wa Henan
Katika siku za nyuma, nilikuwa nimeunganishwa na dada mmoja kufanya kazi kwa wajibu fulani. Kwa sababu nilikuwa na majisifu na mwenye kiburi na sikutafuta ukweli, nilikuwa na mawazo kiasi ya kabla kuhusu dada huyu ambayo niliweka moyoni mwangu daima na sikuzungumza waziwazi naye. Tulipotengana, sikuwa nimeingia katika ukweli wa uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha.
Jumamosi, 23 Novemba 2019
Kupata Ahueni kwa Njia ya Kumwamini Mungu
Zhuanbian Mji wa Shanghai
Ingawa nilikuwa nikimfuata Mungu kwa miaka mingi, nilikuwa karibu sijafanya maendeleo yoyote na kuingia kwangu katika maisha, na hii ilinifanya nihisi kuwa na wasiwasi sana. Hasa wakati niliposikia rekodi ya mahubiri juu ya kuingia kwa maisha, na kusikia mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu akizungumza na ndugu wa kiume na wa, nilihisi nikiwa nimejawa na wasiwasi nikimsikia akisema jambo kama hili, “Nyinyi sasa mnamwamini Mungu na mmeonja uzuri wa ukimbizaji wa ukweli. Nyinyi mmeanza kuingia kwa njia sahihi na mmejaa imani katika ukimbizaji wenu wa wokovu.” Nikawaza, “Watu hawa wamemwamini Mungu kwa muda mfupi sana lakini wameingia tayari na wamejaa imani sana kuhusu kuokolewa. Na bado niko hapa nikiwa nimemwamini Mungu hadi sasa na bado sijaipata ukweli na tabia yangu katika maisha haijapitia mabadiliko yoyote kamwe, bila kujali kuwa nilikuwa nimeingia kwa njia sahihi. Ni rahisi kuongelea kufikia wokovu kuliko kukuweka katika vitendo!” Niliwaza jinsi hao wa hapo juu walifanya ushirika kwamba ukweli ungeweza kutatua upotovu wote wa wanadamu, lakini sikuwa nimepitia jambo hili kamwe. Hata nilihisi kwamba ukweli ungeweza kutatua upotovu wa watu wengine lakini sio wangu mwenyewe, kwa hiyo nilipoteza imani katika ukimbizaji wangu wa ukweli na wa wokovu. Ingawa nilikuwa na ufahamu kwamba hali yangu mwenyewe haikuwa sahihi, hapakuwa na njia yoyote ambayo ningeweza kuiepuka, hivyo ningeweza tu kumlilia Mungu kwa msaada. Baadaye, maneno Yake yalinipatia nuru, yakinifanya nione ni kwa nini nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi hivyo na bado sikuwa nimeendelea katika maisha, na kwa nini hali yangu haikuwa imepitia mabadiliko yoyote. Mungu pia aliniweka kwa njia ya kutenda na kuingia katika ukweli.
Jumatano, 11 Oktoba 2017
Umeme wa Mashariki | Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu
![]() |
| Umeme wa Mashariki Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako |
Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilamali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa.Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.
Ijumaa, 6 Desemba 2019
Uso halisi wa Mtu Anayedaiwa Kuwa Mtu Mzuri
Kemu Jiji la Zhumadian, Mkoa wa Henan
Katika mawazo yangu mwenyewe, daima nimejifikiria kuwa na ubinadamu mzuri. Nimefikiria hivi kwa sababu, majirani zangu mara nyingi walinisifu mbele ya wazazi wangu kwa kuwa mwenye busara na wa kuijali familia yetu; wakisema kuwa mimi nilikuwa kipenzi cha wazazi wangu. Baada ya kuolewa, wakwe zangu walinishukuru mbele ya majirani kwa kuwa wema na mtoto wao. Katika mahali pangu pa kazi, kiongozi wangu alinisifu kwa kuwa mwaminifu na mwenye ustadi. Na tangu nikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, nimekuwa mtii kwa chochote kanisa huniomba kufanya. Huwa sipingani kamwe na kiongozi hata nikikemewa na kiongozi huyu kwa kutofanya kazi nzuri, na mara nyingi mimi huwasaidia ndugu wa kiume na wa kike walio na mahitaji. Kwa hivyo, ninaamini kuwa mimi ni wa maana, mwenye huruma, na mtu mwema mwenye ubinadamu. Sijawahi kujifikiria mwenyewe kwa njia ya maneno ambamo Mungu hufichua kuwa mwanadamu hana ubinadamu au kwamba mtu ana ubinadamu dhaifu. Wakati wa kuwasiliana maneno ya Mungu na ndugu wa kiume na wa kike, ingawa najua nahitaji kuwa na ufahamu wa asili yangu mwenyewe, bado mimi hudumisha mtazamo wangu mwenyewe, nikifikiria moyoni mwangu: Hata kama mimi si mtu wa ubinadamu mzuri, bado nina ubinadamu bora kiasi ukilinganisha na wengine. Aidha, bila kujali neno la Mungu linavyosema au kile ndugu wa kiume na wa kike wanavyosema, siko tayari kujitenga na wazo la kuwa mtu wa ubinadamu mzuri.
Jumapili, 4 Februari 2018
Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa
Mwenyezi Mungu alisema, Imesemwa “Yeye afuataye hadi mwisho ataokolewa,” lakini hili ni rahisi kuweka katika vitendo? Sio, na watu wengine hawawezi kufuata hadi mwisho. Pengine watakapokabiliwa na wakati wa majaribu, ama uchungu, ama jaribio, basi wanaweza kuanguka, na kutoweza kusonga mbele tena. Mambo ambayo hufanyika kila siku, yawe ni makubwa ama madogo, yanaweza kutikisa uthabiti wako, kuumiliki moyo wako, kuzuilia uwezo wako wa kufanya jukumu lako, ama kudhibiti kuendelea kwako mbele—vitu hivi vyote vinahitaji kuchukuliwa kwa uzito, lazima vichunguzwe kwa makini ili kuutafuta ukweli, na ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu.
Alhamisi, 3 Oktoba 2019
Matamshi ya Kristo | Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia
Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)









