Smiley face

Jumamosi, 29 Juni 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

   Mwenyezi Mungu anasema, Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu. Hata ingawa hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika.

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

 Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. Leo, ufalme ujapo kuwepo rasmi duniani, binadamu wote bado hujui kinachopaswa kukamilishwa, ulimwengu ambao binadamu hatimaye ataletwa ndani, wakati wa Enzi ya Ufalme. Kuhusu haya, Naogopa watu wote wako katika hali ya mkanganyiko.

Alhamisi, 27 Juni 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

 Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje, bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Hata ingawa Nimeyaweka maneno Yangu wazi, kuna yeyote aliyeelewa? Nilitoka Sayuni Nikaja miongoni mwa wa nadamu.

Jumatano, 26 Juni 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Mbili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

  Mwenyezi Mungu anasema, Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangazwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya asili, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya.

Jumanne, 25 Juni 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja


Mwenyezi Mungu anasema, Ingawa Nasema malaika wameanza kutumwa mbele kuchunga wana na watu Wangu, hakuna anayeweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Nikujapo binafsi miongoni mwa binadamu, malaika wanaanza wakati huo huo kazi ya uchungaji, na wakati huo wa uchungaji wa malaika, wana na watu wote hawapati tu majaribio na uchungaji, lakini wanaweza pia kuona, na macho yao, tukio la kila aina ya maono.

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi


Enzi ya Ufalme ni, hata hivyo, tofauti na nyakati za kale. Haihusu kile anachofanya mwanadamu. Badala yake, Mimi binafsi Natekeleza kazi Yangu baada ya kushuka duniani—kazi ambayo wanadamu hawawezi kuelewa wala kufanikisha. Tangu kuumbwa kwa ulimwengu mpaka leo, miaka hii yote daima imehusu kujenga kanisa, lakini hakuna mtu anayesikia kamwe kuhusu kujenga ufalme. Japokuwa Nazungumza kuhusu haya kwa kinywa Changu mwenyewe, yupo yeyote anayejua asili yake? Wakati mmoja Nilishuka kwenye ulimwengu wa binadamu Nikapitia na Nikaangalia kwa makini mateso yao lakini bila ya kutimiza lengo la kupata mwili Kwangu.

Jumapili, 23 Juni 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima kifikie viwango Ninavyohitaji Mimi. Sisemi kwamba uwe tu kama wingu linalofuata upepo, bali uwe kama theluji inayong'aa, na uwe na hali kama yake na hata zaidi uwe na thamani yake. Kwa sababu Nilitoka katika nchi takatifu, si kama yungiyungi, ambalo lina jina tu na halina dutu kwa sababu lilikuja kutoka katika matope na si kutoka nchi takatifu. Wakati ambapo mbingu mpya inashuka duniani na nchi mpya kuenea juu ya anga ndio pia wakati hasa ambao Ninafanya kazi kirasmi miongoni mwa binadamu.

Jumamosi, 22 Juni 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na wakati hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambapo watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo Zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu dunia katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza nafsi Yangu na wanafaa kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu.

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba


          Matawi yote ya magharibi yanapaswa kuisikiliza sauti Yangu:
Je, mmekuwa waaminifu Kwangu hapo awali? Je, mmekuwa mkiyasikia maneno Yangu mazuri ya ushauri? Je, mnayo matumaini ambayo ni halisi na yasiyo na mashaka? Utiifu wa mwanadamu, mapenzi yake, imani yake—hamna kipatikanacho ila kutoka Kwangu, hamna hata kimoja ila kilichotawazawa na Mimi.

Alhamisi, 20 Juni 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima – Tamko la Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu.

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

 Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, wewe unalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je umeona umuhimu ulioko humu? Je, unajua juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yako? Je, unaweza thubutu kuweka wazi kila ulichofanya mbele Yangu? Na mna ujasiri wa kujiita watu Wangu usoni Mwangu—hamna hisia za aibu, pia, bila mantiki yoyote! Wakati mmoja au mwingine, watu kama hawa watafukuzwa kutoka katika nyumba Yangu.

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno "Mungu" na mafungu ya maneno kama "kazi ya Mungu", hawamjui Mungu, sembuse kujua kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, kwamba wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa uzito kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao.

Jumatano, 19 Juni 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, 

Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu? Je, Nilikuwa Nimejaza nyoyo zenu zote? Je, maneno Yangu yalitimiza kiasi gani ndani yenu? Msinichukue kama mpumbavu! Hivi vitu viko wazi kabisa Kwangu! Leo, sauti ya wokovu Wangu inapopazwa nje, je, kumekuwa na ongezeko la upendo wenu Kwangu? Je, sehemu ya uaminifu wenu Kwangu imekuwa safi? Je, ufahamu wenu kunihusu umezidishwa? Je, sifa ya zamani iliweka msingi dhabiti kwa maarifa yenu leo hii? Je, ni kiasi gani cha undani wenu kinamilikiwa na Roho Wangu? Mfano Wangu unamiliki sehemu kiasi gani ndani yenu? Je, matamshi Yangu yamewagonga katika sehemu yenu ya udhaifu? Je, mnahisi kwa kweli kuwa hamna mahali pa kuficha aibu yenu? Je, mnaamini kwa kweli kuwa hamjafuzu kuwa watu Wangu? Iwapo hutambui kabisa maswali haya, basi hii inaashiria kuwa unafanya kazi gizani, kwamba uko tu pale kuongeza idadi, na kwamba katika muda ulioamuliwa na Mimi kabla ya siku hii, kwa hakika utaangamizwa na kutupwa katika shimo lisilo na mwisho kwa mara ya pili.

Jumatatu, 17 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”



Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”

Mwenyezi Mungu anasema, “Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata uzoefu wa maisha ya binadamu, Nikichunguza kwa karibu matendo yote ya mwanadamu. Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona kwa vitendo vya ukweli uzima wote wa uungu Wangu.

Jumapili, 16 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli.

Jumamosi, 15 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Tatu


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Tatu
   

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa sababu Mungu hana upotovu wowote wa mwanadamu na hana chochote sawa na, au kinachofanana na tabia potovu ya mwanadamu ama kiini cha Shetani, kutoka mtazamo huu tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu. Mungu hafichui upotovu wowote, na ufunuo wa kiini Chake katika kazi Yake yote ni thibitisho tunalohitaji kwamba Mungu Mwenyewe ni mtakatifu. Je, mnaona hili? Sasa, kujua asili takatifu ya Mungu, kwa sasa wacha tuangalie hivi vipengele viwili: 1) Hakuna tabia potovu ndani ya Mungu; 2) kiini cha kazi ya Mungu kwa mwanadamu kinamruhusu mwanadamu kuona kiini cha Mungu mwenyewe na kiini hiki ni kizuri kabisa. Kwa kuwa vitu ambavyo kila namna ya kazi ya Mungu inamletea mwanadamu ni vitu vizuri.”


Tazama Video: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” Yaliyopendekezwa: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo.

Alhamisi, 13 Juni 2019

Maonyesho ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu" Sehemu ya Tano



Maonyesho ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu" Sehemu ya Tano

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu "Neno Laonekana katika Mwili".
Maudhui ya video hii: Aina Tano za Watu Aina ya Kwanza: Hatua ya Mtoto Mchanga aliyefungwa kwa Vitambaa Aina ya Pili: Hatua ya Mtoto Mchanga Anayenyonya Aina ya Tatu: Hatua ya Mtoto Mchanga Anayeachishwa Ziwa, au Hatua ya Mtoto Mdogo Aina ya Nne: Hatua ya Mtoto Anayekomaa, au Kipindi cha Utoto Aina ya Tano: Hatua ya Maisha Yaliyokomaa, au Hatua ya Mtu Mzima

Jumatano, 12 Juni 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" (Sehemu ya Kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema, "Yesu aliwakilisha Roho wa Mungu, na Alikuwa Roho wa Mungu Akifanya kazi moja kwa moja. Alifanya kazi ya enzi mpya, kazi ambayo hakuna aliyekuwa amefanya mbeleni. Yeye Alifungua njia mpya, Alimwakilisha Yehova, na Alimwakilisha Mungu Mwenyewe. Ilhali kwa Petro, Paulo na Daudi, bila kujali walichoitwa, waliwakilisha tu utambulisho wa kiumbe wa Mungu, ama walitumwa na Yesu na Yehova.

Jumatatu, 10 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii: Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza 1. Maisha Mapya Yanazaliwa Kulingana na Mipango ya Muumba 2. Kwa Nini Binadamu Tofauti Wanazaliwa Katika Hali Tofauti Kukua: Awamu ya Pili 1. Hali Ambazo Mtu Hukulia Ndani Zimepangwa na Muumba 2. Hali Mbalimbali Ambazo Watu Hukulia Ndani Husababisha Wajibu Tofauti
   
          Mwenyezi Mungu anasema:

Hakuna yeyote aliye na chaguo kuhusu sehemu hizi za awamu hii; zote ziliamuliwa kabla, mapema kabisa na Muumba.

Jumapili, 9 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima



Matamshi ya Mungu | “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele


Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia.

Jumamosi, 8 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haijafichwa, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi kimakusudi kujaribu kujificha Mwenyewe ili watu wasiweze kumjua Yeye au kumwelewa Yeye. Tabia ya Mungu siku zote imekuwa wazi na siku zote imekuwa ikitazama kila mtu kwa njia ya uwazi. Katika usimamizi wa Mungu, Mungu hufanya kazi Yake akitazama kila mmoja; na kazi Yake ndiyo inafanywa kwa kila mtu.

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu (Lyrics Video)



Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu (Lyrics Video)
Mungu awahimiza makabila yote, mataifa na nyanja zote: Sikizeni sauti Yake, muione kazi Yake; mzingatie hatima ya wanadamu; mfanye Mungu Mtakatifu na Mheshimiwa, Mkuu na wa pekee wakuabudiwa, ulimwengu wote, na wanadamu, waishi chini ya baraka Yake Mungu, kama vizazi vya Ibrahimu, walivyoishi na ahadi ya Yehova, kama viumbe vya Mungu, Adamu na Hawa, walivyoishi bustani Edeni. Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yavumayo hakuna wa kumzuia au kumsimamisha.

Ijumaa, 7 Juni 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali.

Jumatano, 5 Juni 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu” | How to Be a Loyal Servant of God



Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu” | How to Be a Loyal Servant of God

    Mwenyezi Mungu anasema, “Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi.

2019 Swahili Gospel Worship Song | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" (Lyrics Video)



2019 Swahili Gospel Worship song | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" (Lyrics Video)

I Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, ni jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo la Mungu. Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu, na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

Jumanne, 4 Juni 2019

Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians



Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians
I
Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, ni jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo la Mungu. Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu, na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake. Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu, na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

Jumatatu, 3 Juni 2019

Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma


Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma

Kutoka Mashariki ya ulimwengu (Mashariki ... Mashariki ...),
mwale wa mwanga unatokea (mwanga ... mwanga ...),
ukiangaza njia yote kwenda magharibi.
Mwana wa Adamu ameshuka duniani.
Mwokozi amerejea, Yeye ni Mwenyezi Mungu. Akionyesha ukweli, Ameanzisha enzi mpya. Mwana wa Adamu ameonekana. (Siyo?) Mungu amekuja. (Eh!) Yeye huwaletea binadamu njia ya uzima wa milele (njia ya uzima wa milele).

Jumamosi, 1 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu
1. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe
2. Mielekeo Mbalimbali ya Wanadamu kwa Mungu
3. Mwelekeo Ambao Mungu Anahitaji Mwanadamu Awe Nao Kwake

Mwenyezi Mungu anasema:

Tumefikia mwisho wa mada ya “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote,” vilevile na ile ya “Mungu ni wa kipekee Mungu Mwenyewe.” Baada ya kufanya hivyo, tunahitaji kufanya muhtasari. Muhtasari wa aina gani? Unaomhusu Mungu Mwenyewe.