Smiley face

Jumatano, 31 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,neno la Mungu,kazi ya Mungu

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yananayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku.

Jumatatu, 29 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?


Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndinyi mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu.

Neno la Mwenyezi Mungu | Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Neno la Mungu,kazi ya Mungu

Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (katika siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima.

Jumapili, 28 Julai 2019

Matamshi ya Mungu | Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu,kumjua mungu,Yesu Kristo

Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo. Ufahamu wa Mungu wa vitendo unajumuisha kujua na kuyapitia maneno Yake, na kuelewa sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. Kwa hivyo, pia, inajumuisha kujua kwamba kila tendo la Mungu katika mwili linaongozwa na Roho, na kwamba maneno Anenayo ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho.

Ijumaa, 26 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ufalme wa Milenia Umewasili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Enzi ya Ufalme,Mwenyezi Mungu

Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu. Na hivyo kila hatua ya kazi Yake inafanywa na Mungu Mwenyewe.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Amri za Enzi Mpya

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mmeambiwa kuwa mjiandae kwa maneno ya Mungu, ya kuwa pasipo kujali mlichoandaliwa ninyi, yote yamepangwa kwa mkono wa Mungu, na kwamba hakuna haja ya kuomba kwa bidii au kusali kwenu—hayana maana. Ilhali kulingana na hali ya sasa, shida za kiutendaji mnazokumbana nazo hazifikiriki kwenu. Kama mnasubiri mipango ya Mungu tu, basi kuendelea kwenu kutakuwa polepole sana, na kwa wale wasiojua jinsi ya kupitia kutakuwa na kulaza damu kwingi. Kwa hivyo, ikiwa umeshindwa kabisa kuyalewa mambo haya, basi umechanganyikiwa na kuwa mpumbavu katika uzoefu wako.

Alhamisi, 25 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Jinsi ya Kuujua Uhalisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Maisha ya kanisa,Kumwabudu Mungu

Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.

Jumatano, 24 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,kumjua Mungu

Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao kwa Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako. Ukifika mahali hapo utafurahia kujua imani katika Mungu ni nini, namna ya kumwamini Mungu vizuri, na kile unachopaswa kufanya ili kutenda mambo kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu.

Jumatatu, 22 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Waovu Lazima Waadhibiwe

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mamlaka ya Mungu

Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Mtaitwa wenye haki kwa sababu mnaweza kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu mnakubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. Jinsi mnavyozidi kukubali maneno ya Mungu wakati huu, ndivyo mnavyozidi kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo mnavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kukidhi mahitaji Yake.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu, Maneno ya Mungu

Ni njia gani ambayo Mungu hutumia kumkamilisha mwanadamu? Ni vipengele vipi vinavyojumuishwa? Je, uko tayari kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unajua nini kuhusu maswali haya? Kama huwezi kuzungumzia maarifa kama haya, basi hii inaonyesha kwamba bado huijui kazi ya Mungu na hujapatiwa nuru katu na Roho Mtakatifu. Binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa. Wanaweza tu kupokea kiasi kidogo cha neema ili kufurahia kwa muda mfupi na haiwezi kuendelezwa kwa kipindi kirefu. Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu.

Jumapili, 21 Julai 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Maisha ya Kanisa,Kuijua Sauti ya Mungu

     Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watiifu kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini.

Jumamosi, 20 Julai 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kazi ya Roho Mtakatifu,

Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. Mungu huja hapa ulimwenguni kimatendo ili kufanya kazi Yake na kuwasiliana na watu ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake.

Ijumaa, 19 Julai 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki , Neno la Mungu


Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Mtu anaweza kusema kwamba binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa sababu ya hili, kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani. Vinginevyo, upendo wa binadamu ni upendo usio safi, ni upendo wa Shetani, na ule ambao hauwezi kabisa kupokea idhini ya Mungu.

Jumatano, 17 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,kumjua Mungu,

Mwenyezi Mungu anasema, Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu.

Neno la Mwenyezi Mungu|Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni.

Jumatatu, 15 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaelekea kikomo, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
        
      Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.

Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana.

Jumapili, 14 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Siku hiyo ambayo vitu vyote vilifufuliwa, Nilikuja miongoni mwa wanadamu, na Nimeshinda naye kwa siku zilizokuwa za ajabu usiku na mchana. Ni katika hatua hii tu ndipo mwanadamu anaona wepesi Wangu wa kufikiwa, na vile uhusiano wake na Mimi unavyozidi kuwa mwingi, anaona baadhi ya kile Ninacho na Nilicho—na kwa sababu hii, anapata ufahamu kunihusu. Miongoni mwa watu wote, Ninainua kichwa Changu na kutazama, na wote wananiona. Hata hivyo, wakati maafa yanaikumba dunia, wanakuwa na wasiwasi mara moja, na sura Yangu inatoweka kutoka katika nyoyo zao; wakishikwa na hofu kutokana na kufika kwa maafa, hawasikii kusihi Kwangu.

Ijumaa, 12 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Nilipokuja kutoka Zayuni, vitu vyote vilikuwa vimenisubiri, na Niliporudi Zayuni, Nilisalimiwa na wanadamu wote. Nilipokuja na kwenda, hatua Zangu hazikuwahi zuiliwa na vitu vilivyokuwa na uadui Kwangu, na kwa hivyo kazi Yangu iliendelea kwa utaratibu. Leo, Ninapokuja miongoni mwa viumbe vyote, vitu vyote vinanisalimu kwa kimya, kwa uoga mkuu kuwa Nitaondoka tena na Niondoe usaidizi kwao. Vitu vyote vinafuata uongozi Wangu, na vyote vinaangalia upande ulioashiriwa na mkono Wangu.

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

   Mwenyezi Mungu anasema, Mienendo ya binadamu haijawahi kuugusa moyo Wangu kamwe, wala kuonekana Kwangu kama kitu cha thamani. Machoni mwa mwanadamu, Mimi humweka katika sheria kali kila wakati, na kila mara Nimemweka chini ya mamlaka kali. Ndani ya matendo yote ya mwanadamu, ni mambo machache sana anayonifanyia Mimi, na mara nyingi hapana kitendo chake kisimamacho imara machoni Pangu. Hatimaye, kila kitu kinachomhusu mwanadamu kimeporomoka polepole mbele Yangu, na ni katika nyakati kama hizi ndipo matendo Yangu hudhihirika, na kumfanya kila mmoja, katika upotovu wake, kunitambua Mimi.

Alhamisi, 11 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni.

Jumanne, 9 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: Muda unapita, na kufumba na kufumbua leo imefika. Chini ya uongozi wa Roho Wangu, watu wote wanaishi katikati ya mwanga Wangu, na hakuna anayefikiria yaliyopita ama kuiwekea jana maanani. Nani hajawahi kuishi katika wakati wa sasa? Ni nani ambaye hajapitia katika siku na miezi ya ajabu katika ufalme? Ni nani hajaishi chini ya jua? Ingawa ufalme umeshuka miongoni mwa mwanadamu, hakuna ambaye amepata kupitia ukunjufu wake; mwanadamu anautambua tu kutoka nje, bila kufahamu dutu lake.

Jumatatu, 8 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kuadibu kwangu kunawajia watu wote, lakini pia kunakaa mbali na watu wote. Maisha yote ya kila mtu yamejaa upendo na pia chuki Kwangu, na hakuna mtu ambaye amewahi kunijua na kwa hivyo mtazamo wa mwanadamu Kwangu ni wa sitasita, na hauna uwezo wa kuwa kawaida. Lakini Nimekuwa Nikimlea na kumchunga mwanadamu na ni kwa sababu ya upumbavu wake ndiyo maana hana uwezo wa kuona matendo Yangu yote na kuelewa nia Zangu.

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu

Mamlaka ya Mungu,Wokovu wa Mungu,Umeme wa Mashariki

Ninapopaza sauti Yangu, macho Yangu yanapofyatua moto, Ninaitazama kwa uangalifu dunia nzima, Ninatazama kwa uangalifu ulimwengu mzima. Wanadamu wote wananiomba Mimi, wameinua macho yao kuelekea Kwangu, wakiomba Nipunguze hasira, na kuapa kutoniasi tena. Lakini haya siyo yaliyopita; bali yaliyopo kwa sasa. Ni nani anayeweza kubadilisha mapenzi Yangu? Kwa kweli sio sala katika moyo wa mwanadamu, wala maneno yanayotoka midomoni mwao? Ni nani ambaye ameweza kuishi hadi wakati huu, isipokuwa ni kwa nguvu Zangu? Ni nani anayeishi ila kwa maneno ya kinywa Changu? Ni nani asiyekaa chini ya uangalifu wa macho Yangu? Ninapofanya kazi Zangu katika ulimwengu mzima, ni nani ambaye ameweza kuiepuka kazi hiyo? Inawezekana kuwa milima imeiepuka kutokana na urefu wayo? Inawezekana kuwa maji kwa wingi na upana wake, yameweza kuizuia kazi hii? Katika mpango Wangu, Sijawahi kuachilia kitu chochote kiende kwa wepesi, hivyo basi hakuna mtu yeyote, wala kitu chochote, ambacho kimeepuka mikono Yangu.

Jumapili, 7 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani.

Ijumaa, 5 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa urejesho Wangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulikane waliko na gharika hili la urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya ya maji; na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao basi wamefuata mafuriko mpaka sasa.

Alhamisi, 4 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
   
 
     Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao. Kwa hivyo, miongoni mwa watu hakuna mtu aliyewahi kuishi katika hali halisi, na watu wote huishi maisha yasiyo na maana.

Jumatano, 3 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Sauti ya Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, Ni shughuli sahihi ya mwanadamu kuchukua maneno Yangu kama msingi wa maisha yake. Mwanadamu lazima aanzishe fungu lake binafsi katika kila sehemu ya maneno Yangu; kutofanya hivyo kutakuwa kuuliza matata, kutafuta maangamizo yake mwenyewe. Binadamu haunijui, na kwa sababu ya hili, badala ya kuleta maisha yake Kwangu badala, anachofanya ni kujipanga tu mbele Yangu na takataka mikononi mwake, na hivyo kujaribu kuniridhisha. Lakini, mbali na kuridhishwa na mambo yalivyo, Naendelea kutoa matakwa kwa binadamu. Napenda sifa za mwanadamu, lakini Nachukia wizi wake.

Jumanne, 2 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane

Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oh, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu? Wanawezaje, katika mwanga, kukosa kuendeleza kazi zao? Dunia si kimya na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena.

Jumatatu, 1 Julai 2019

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

 Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani.

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, Kuna mengi ambayo Natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simwangamizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wake wa nguvu, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya kazi Yangu tu, na kuongea jinsi ambavyo Nimefanya, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua ndani kabisa ya nyoyo zao, na watanikumbuka katika mawazo yao.