Smiley face

Jumatatu, 30 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

    Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe.

Jumapili, 29 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo| Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili)

Wakati kazi ya Mungu inafikia hatua fulani, na usimamizi Wake kufikia hatua fulani, wale wanaoutafuta moyo Wake wote huwa na uwezo wa kutimiza matakwa yake. Mungu humwekea mwanadamu matakwa kulingana na viwango Vyake mwenyewe, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Akiwa anazungumzia usimamizi Wake, Yeye humwonyesha njia mwanadamu , na kumpa mwanadamu namna ya kudumu. Usimamizi wa Mungu na vitendo vya mwanadamu vipo katika hatua sawia kikazi, na yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mungu yanagusia mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, na yanazungumzia kuhusu yale yafaayo kufanywa na mwanadamu, na mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, hugusia kazi ya Mungu; hakuna wakati ambao haya mawili yanaweza kutenganishwa.

Jumamosi, 28 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo|Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)

Kazi ya Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu.

Ijumaa, 27 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi.

Alhamisi, 26 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili)

Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo sio kazi ya hukumu.

Jumatano, 25 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza)

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, Mungu ni lazima Awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi.

Jumanne, 24 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili)


Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima afahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia inazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu.

Jumatatu, 23 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu|Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili)


Kazi ya mwanadamu ina mipaka na kadiri inavyoweza kufika. Mtu mmoja anaweza kufanya kazi ya wakati fulani na hawezi kufanya kazi ya enzi nzima—vinginevyo anaweza kuwaongoza watu katika kanuni. Kazi ya mwanadamu inaweza kufaa tu katika kipindi au awamu fulani. Hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu una mipaka. Mtu hawezi kulinganisha kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu. Namna mwanadamu anavyofanya mambo na maarifa yake ya ukweli yote yanatumika tu katika mawanda fulani. Huwezi kusema kwamba njia ambayo mwanadamu anaiendea ni matakwa ya Roho Mtakatifu kabisa, kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa nuru na Roho Mtakatifu tu na hawezi kujazwa kikamilifu na Roho Mtakatifu.

Jumamosi, 21 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)

Kupata Mwili,Yesu Kristo,Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ni kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, kimsingi, ni kwa kurejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au kaka na dada wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hapa, kazi ya mwanadamu hairejelei kazi ya Mungu mwenye mwili bali mawanda na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu.

Matamshi ya Mungu | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili)


Petro alifanywa mkamilifu kwa kupitia ushughulishaji na usafishaji. Alisema, “Mimi ni lazima nikidhi mapenzi ya Mungu wakati wote. Kwa yote nifanyayo mimi natafuta tu kukidhi mapenzi ya Mungu, na kama mimi ninaadibiwa, au kuhukumiwa, bado nina furaha kufanya hivyo.” Petro alimpa Mungu kila kitu chake, na kazi yake, maneno, na maisha yote yalikuwa yote kwa ajili ya kumpenda Mungu. Alikuwa mtu ambaye alitafuta utakatifu, na alipopitia zaidi, ndivyo upendo wake wa Mungu ndani ya moyo wake ulikuwa mkubwa zaidi. Paulo, wakati huo huo, alifanya tu kazi ya nje, na ingawa alitia bidii katika kazi yake, juhudi zake zilikuwa kwa ajili ya kufanya kazi yake vizuri na hivyo kupata tuzo.

Alhamisi, 19 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza)

kazi ya Mungu,kumjua Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Uyahudi. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyotoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Wanaisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Wanaisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Uyahudi, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kwa kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi pekee, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Wanaisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaowakomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote.

Jumanne, 17 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu|Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu


Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde mnapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia wako utakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kazi yako. Kwa njia hiyo, tajriba na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua ukweli wote, hutapoteza kitu maishani na hutapotea. Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache.

Matamshi ya Mungu|Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Mungu Kupata Mwili,Bwana Yesu,Kazi ya Mungu

Kazi ya Mungu katika mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na kumsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, si mwanadamu ni adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa amehitimu kumshuhudia Mungu? Kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu—je, huu si udanganyifu? Kama unayatoa maisha yako kwa haya mambo yasiyokuwa na uhalisia, yasiyoweza kutekelezeka, huoni kama unafanya kazi bure? Unawezaje kuwa mwandani wa Mungu wakati hujui Mungu ni nani? Kufuatilia huko si kusio dhahiri na kwa dhahania? Je, sio kwa udanganyifu? Mtu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Kuna maana gani kivitendo kuwa mwandani wa Mungu? Je, unaweza kuwa mwandani wa Roho wa Mungu? Huwezi kuona jinsi Roho alivyo mkubwa na alivyoinuliwa? Kuwa mwandani wa Mungu asiyeonekana, asiyeshikika—hii sio dhana isiyoeleweka na dhahania? Maana tendaji ya kufuatilia huku ni gani? Je, sio udanganyifu mtupu tu? Kile unachokitafuta ni kuwa mwandani wa Mungu, lakini bado ni mtumwa wa Shetani, maana humfahamu Mungu, na kumtafuta “Mungu wa vitu vyote,” asiye kuwepo ambaye haonekani, hashikiki, na mitazamo yako mwenyewe.

Jumatatu, 16 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu|Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?


Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali.

Jumamosi, 14 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu|Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo yote husika na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kwa kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inapozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili)

Yesu,Mungu Kupata Mwili,kumjua Mungu

Mwanzoni, wakati Yesu alikuwa bado hajafanya rasmi huduma Yake, kama wanafunzi waliomfuata, wakati mwingine pia Yeye alihudhuria mikutano, na kuimba tenzi, Akasifu, na kusoma Agano la Kale kwa hekalu. Baada Yeye kubatizwa na kupanda, Roho alishuka rasmi juu yake na kuanza kufanya kazi, Akifichua utambulisho Wake na huduma Aliyokuwa afanye. Kabla ya haya, hakuna aliyejua utambulisho Wake, na mbali na Maria, hata Yohana hakujua. Yesu alikuwa 29 Alipobatizwa. Baada ya ubatizo wake kukamilika, mbingu zilifunguliwa, na sauti ikasema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Baada ya Yesu kubatizwa, Roho Mtakatifu alianza kumshuhudia kwa njia hii.

Alhamisi, 12 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu: Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili)


Kwanza Mungu alimwumba Adamu na Hawa, na pia Alimwumba nyoka. Miongoni mwa mambo haya yote, nyoka ndiye aliyekuwa mwenye sumu zaidi; mwili wake ulikuwa na sumu, na Shetani aliitumia sumu hiyo ili kufaidika. Ni nyoka aliyemjaribu Hawa hadi akatenda dhambi. Adamu alitenda dhambi baada ya Hawa kutenda, na wawili hawa waliweza kutofautisha kati ya mema na maovu. Kama Yehova Alikuwa Amejua kwamba nyoka angemjaribu Hawa, na kwamba Hawa angemjaribu Adamu, kwa nini Akawaweka wote pale katika bustani? Kama Aliweza kutabiri mambo haya kwa nini Akamwumba nyoka na kumweka ndani ya Bustani ya Edeni? Kwa nini Bustani ya Edeni ilikuwa na tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Alinuia wao walile hilo tunda? Wakati Yehova alipokuja, Adamu wala Hawa hawakuthubutu kumkabili Yeye, na ulikuwa tu wakati huu ambapo Yehova alijua kwamba walikuwa wamelila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kujipata katika ujanja wa yule nyoka.

Jumatano, 11 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza)

Yesu Kristo,Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu

Iwapo unataka kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu, lazima uijue kazi ya Mungu; lazima uijue kazi Aliyofanya awali (katika Agano Jipya na la Kale), na, zaidi ya hayo, lazima uijue kazi Yake ya leo. Ndiyo kusema, ni lazima uzitambue hatua tatu za kazi ya Mungu ya zaidi ya miaka 6,000. Ukiulizwa ueneze injili, basi hutaweza kufanya hivyo bila kuijua kazi ya Mungu. Watu watakuuliza yote kuhusu Biblia, na Agano la Kale, na nini Yesu alisema na kufanya wakati huo. Watasema, "Mungu wenu hajawaeleza haya yote? Kama Yeye (Mungu) hawezi kuwaeleza ni nini hasa yanayoendelea kwa Biblia, basi Yeye si Mungu; kama Anaweza, basi tumeamini." Mwanzoni, Yesu alizungumzia sana Agano la Kale na wanafunzi Wake. 

Matamshi ya Mungu | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza)


Ukamilifu wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova bado hakuwa amepanga hatua ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; hatua ya pili ya kazi, ile ya neema; au hatua ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kutokana na hili Angeweza kuushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi Yake yote ilifanywa bila kupangwa.

Jumatatu, 9 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Yesu asulubiwa kuwakomboa wanadamu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufunua ubovu wa Shetani.

Jumapili, 8 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kazi katika Enzi ya Sheria

Kumjua Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
  
Kazi ambayo Yehova Alifanya kwa Waisraeli ilianzishwa miongoni mwa binadamu mahali pa asili pa Mungu hapa ulimwenguni, pahali patakatifu ambapo Alikuwepo. Hii kazi Aliiwekea mipaka miongoni mwa watu wa Israeli tu. Kwanza, hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Alichagua watu Alioona kwamba walifaa ili kuwawekea mipaka upana wa kazi Yake. Israeli ndipo mahali ambapo Mungu Aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka kwenye vumbi la mahali hapo, Yehova Alimwumba mwanadamu; ndio msingi wa kazi Yake ya hapo ulimwenguni. 

Sauti ya Mungu | Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile. 

Jumamosi, 7 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Neno la Mungu

Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani aweze kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumwonea shauku kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, kwa Yesu Mwokozi kuwarudia watu ambao Amekuwa mbali nao kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumai kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atazisamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi.

Ijumaa, 6 Septemba 2019

sauti ya Mungu | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kupona kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba "siku za mwisho" ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria.

Alhamisi, 5 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Neno la Mungu

Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ulikuwa hata umeshaamuliwa kabla zaidi Nilipoiumba dunia. Watu hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho, na pia hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini Nilikuwa Nimeshamwambia adui Yangu lilipokuwa linapambana na Mimi kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kwa muda mrefu walikuwa watoto wa Shetani, na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake.

Jumanne, 3 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?


Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vyema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni? Ingawa watu wameshuhudia matukio ya kiajabu ya mbinguni wakati huu na wamepata kusikia kuhusu elimu kuu ambayo mwanadamu hajapata kuwa nayo awali, bado wako gizani kuhusu mambo mengi ya kawaida, na ambao ni ukweli ambao haujafikiriwa.

Jumatatu, 2 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unajua Nini Kuhusu Imani?

kumjua Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Je, unaweza kuonyesha tabia ya Mungu ya nyakati kwa lugha inayofaa iliyo na umuhimu wa nyakati? Kupitia uzoefu wako wa kazi ya Mungu, unaweza kueleza kwa undani tabia ya Mungu? Utaielezaje vizuri, kikamilifu? Ili kupitia haya, watu wengine wapate kufahamu uzoefu wako. Utawezaje kupitisha uliyoyaona na kupitia kwa maskini hawa wa kuhurumiwa, na waumini wa kidini wa kumcha Mungu waliojitolea na waliojawa na njaa na kiu ya haki na wanaongoja uwe mchungaji wao? Ni watu wa aina gani ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Unaweza kuwaza kweli? Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? Utahudumu vipi kama kiongozi mzuri wa wakati unaofuata? Je, unao hisia nzuri ya uongozi? Utaeleza mkuu wa kila kitu kama nini? Je, ni mkuu wa kila kitu kilicho hai na viumbe vyote duniani? Una mipango ipi ya kuendelea kwa hatua inayofuata ya kazi? Ni watu wangapi ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Je, jukumu lako ni nzito? Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, "Njia iko wapi?" Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi.