Smiley face

Jumapili, 31 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Pili

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya, na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, kitu chochote, au kifaa chochote, na haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili.

Jumamosi, 30 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile walichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe.

Ijumaa, 29 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 30

Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri. Mwisho wa dunia unafunguka mbele ya macho yenu wenyewe, majanga makubwa yanakaribia upesi; Je, maisha yenu ni muhimu au kulala, kula, kunywa, na kuvaa kwenu ndivyo muhimu? Wakati umekuja wa ninyi kufikiria kwa makini mambo haya. Msiwe wenye shaka tena na msiogope kuwa na uhakika!

Jumanne, 26 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 29

Je, ulijua kwamba wakati uko karibu? Hivyo kwa muda mfupi wa hivi karibuni utanitegemea Mimi na kuyatupilia mbali mambo yote kutoka kwako ambayo hayalingani na tabia Yangu: upumbavu, upole wa kuonyesha hisia, mawazo yasiyo wazi, moyo wa upole, nia hafifu, upuuzi, hisia zilizotiwa madoido mengi, kuchanganyikiwa na ukosefu wa utambuzi. Haya lazima yatupiliwe mbali upesi iwezekanavyo. Mimi ndimi mwenyezi Mungu! Mradi tu uko radhi kushirikiana na Mimi, Nitayatibu yote yanayokuuguza. Mimi ni Mungu anayeangalia ndani kabisa ya mioyo ya watu, Naujua magonjwa yako yote na kule ambako dosari zako ziko.

Jumatatu, 25 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 28

Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? 

Jumamosi, 23 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Tano

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Tano

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Kuhusu Ayubu
Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake
Maonyesho ya Ubinadamu wa Ayubu Wakati wa Majaribio Yake (Kuelewa Utimilifu wa Ayubu, Unyofu, Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu Wakati wa Majaribio Yake)
Urazini wa Ayubu
Asili Halisi ya Ayubu: Mkweli, Aliyetakaswa, na Asiye na Uongo
Utenganisho wa Ayubu kati ya Upendo na Chuki
Ukarimu na Uaminifu wa Ayubu
Uhusiano Kati ya Mungu kumpa Shetani Ayubu na Malengo ya Kazi ya Mungu
Kubali Mitihani ya Mungu, Shinda Majaribio ya Shetani, na Mruhusu Mungu Kupata Nafsi Yako Nzima
Onyo na Nuru Iliyotolewa kwa Vizazi vya Baadaye Na Ushuhuda wa Ayubu

Ijumaa, 22 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. ... Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu.

Jumatano, 20 Machi 2019

Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne

Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi
Upendo wa Ayubu wa Njia ya Mungu Unazidi Yote Mengine
Katikati ya Mateso makuu, Ayubu Anatambua kwa kweli Utunzaji wa Mungu wa Wanadamu
Maonyesho Mengine ya Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu kwa Ayubu ni Kutukuza Kwake Jina la Mungu Katika Mambo Yote
Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu
Ayubu Anailaani Siku Ya Kuzaliwa Kwake Kwa Sababu Hamtaki Mungu Kupata Maumivu Kwa Sababu Yake
Ayubu Amshinda Shetani na Kuwa Binadamu Wa Kweli Machoni pa Mungu

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Tatu

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Maonyesho Mahususi ya Kumcha Mungu kwa Ayubu na Kujiepusha na Maovu katika Maisha Yake ya Kila siku
Mungu Amruhusu Shetani Kumjaribu Ayubu ili Imani ya Ayubu iweze Kufanywa Kuwa Timilifu
Kwamba Ayubu Anajiwajibikia Yeye Mwenyewe Kurudisha Vyote Anavyomiliki Kunatokana na Kumcha Kwake Mungu

Jumapili, 17 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" Sehemu ya Pili

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Mungu Anawajali tu Wale Wanaoweza Kutii Maneno Yake Na Kufuata Amri Zake
Mungu ni Mwenye Wingi wa Rehema Kwa Wale Anaowajali, na Mwenye Hasira Kali kwa Wale Anaowachukia na Kukataa
Watu Wa Siku Za Mwisho Wanaiona tu Hasira Ya Mungu Katika Maneno Yake, na Hawaipitii kwa Kweli Hasira Ya Mungu
Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu

Jumamosi, 16 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Hakuna Awezaye Kuzuia Kazi Ambayo Mungu Anaamua Kufanya
Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Wanadamu Yaanza na Ibrahimu Kumtoa Isaka
Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli
Binadamu Anapata Baraka za Mungu kwa Sababu ya Uaminifu na Utii Wake
Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaoweza Kumshuhudia Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika

Ijumaa, 15 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Kwanza

Jumatano, 13 Machi 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili.

Jumatatu, 11 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”

Matamshi ya Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa.

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”

Mwenyezi Mungu anasema, “Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka shtaka rasmi lililoandikwa; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika enzi zote, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga.

Jumamosi, 9 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 27

Mungu mmoja wa kweli anayetawala vitu vyote katika ulimwengu—Kristo mwenyezi! Huu ndio ushuhuda wa Roho Mtakatifu, ni ushahidi dhahiri! Roho Mtakatifu anafanya kazi kuwa na ushuhuda kila mahali, ili kusiwe na mtu yeyote mwenye shaka yoyote. Mfalme wa ushindi, Mwenyezi Mungu! Yeye ameushinda ulimwengu, Ameishinda dhambi na kufanikisha ukombozi! Anatuokoa, kundi hili la watu ambao wamepotoshwa na Shetani, na Anatukamilisha kutekeleza mapenzi Yake. Anatawala dunia nzima, Anaichukua tena na kumfukuza Shetani hadi ndani ya shimo lisilo na mwisho. Anauhukumu ulimwengu, na hakuna mtu anayeweza kukwepa kutoka mikononi Mwake. Anatawala kama Mfalme.

Ijumaa, 8 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 26

Wanangu, yatilieni maanani maneno Yangu, sikiliza kwa utulivu sauti Yangu na Nitafichua kwako. Uwe na utulivu ndani yangu, kwa maana Mimi ni Mungu wako, Mkombozi wenu wa pekee. Mnatakiwa kutuliza mioyo yenu nyakati zote, mkae ndani yangu; Mimi ni mwamba wako, msaidizi wenu. Msiwe na nia nyingine, lakini mnitegemee kwa mioyo yenu yote na Mimi nitaonekana kwenu kwa hakika—Mimi ni Mungu wenu!

Jumatano, 6 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia” 

Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni.

Jumatatu, 4 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”

Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo.

Jumapili, 3 Machi 2019

Wimbo wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Watu wa Mungu wa Mataifa Yote Huonyesha Hisia Zao Kama Mtu Mmoja”

Wimbo wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Watu wa Mungu wa Mataifa Yote Huonyesha Hisia Zao Kama Mtu Mmoja” | Praise and Thank God's Love

Uangalie ufalme wa Mungu, ambako Mungu anatawala juu ya yote.
Kutoka wakati uumbaji ulipoanza mpaka siku ya sasa,
wana wa Mungu waliongozwa wakipitia taabu.
Katika milima na mabonde walienda. Lakini sasa katika nuru Yake wanakaa.
Nani asiyelia juu ya udhalimu wa jana?
Ni nani asiyelia machozi kwa ajili ya maisha magumu leo?
Ni nani asiyechukua nafasi hii kutoa mioyo yao kwa Mungu?
Nani hataki kutoa sauti kwa shauku na uzoefu wake?

Ijumaa, 1 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 25

Mwenyezi Mungu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani, Mungu wetu Anatawala! Mwenyezi Mungu anaweka miguu Yake kwenye Mlima wa Mizeituni. Uzuri ulioje! Sikiliza! Sisi walinzi tunapaza sauti zetu: tunaimba kwa pamoja kwa sauti zetu, kwa kuwa Mungu amerudi Sayuni. Tunaona kwa macho yetu wenyewe ukiwa wa Yerusalemu. Furahieni na kuimba kwa sauti kwa pamoja, kwa kuwa Mungu ametufariji na Ameukomboa Yerusalemu. Mungu ameweka wazi mkono Wake mtakatifu machoni pa mataifa yote, mtu halisi wa Mungu amejitokeza! Miisho yote ya dunia imeona wokovu wa Mungu wetu.