Smiley face
Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja neema. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja neema. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote

Jumapili, 1 Desemba 2019

Nilijifunza Kufanya Kazi na Wengine

Maisha ya kanisa
Liu Heng Mkoa wa Jiangxi
Kupitia neema ya Mungu, nilichukua jukumu la kuwa kiongozi wa kanisa. Wakati huo, nilikuwa na shauku mno na niliweka azimio mbele ya Mungu: Bila kujali kinachonikabili, sitayatelekeza majukumu yangu. Nitafanya kazi vizuri na yule dada mwingine na nitakuwa mtu anayetafuta ukweli. Lakini nilikuwa nimeamua tu, na sikujua jinsi ya kuingia katika uhalisi wa uhusiano wa kufanya kazi kwa mpangilio wa kuridhisha. Nilipoanza kwanza kupanga masuala ya kanisa na dada ambaye nilikuwa nikifanya kazi naye, na tulipokuwa na maoni tofauti, ningemwomba Mungu kwa uwazi nikimuuliza Yeye kuulinda moyo wangu na roho yangu ili nisimlaumu mshirika wangu. Hata hivyo, nilizingatia tu kudhibiti vitendo vyangu ili nisiwe na migogoro na mshirika wangu, kwa hivyo sikuwa nimeingia katika ukweli. 

Ijumaa, 29 Novemba 2019

Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu

Umwombe Mungu
Xiaowei Mji wa Shanghai
Wakati fulani kitambo, hata kama daima nilipata msukumo kiasi na fadhila wakati dada mmoja aliyeshiriki nami alishiriki nuru aliyokuwa amepata wakati alipokula na kunywa neno la Mungu, pia kila wakati nilikuwa na hisia ya muda mrefu kuwa alikuwa anajionyesha. Ningejiuliza, “Nikimjibu sasa hivi, sitakuwa nikimtia moyo? Kwa namna hiyo, sitaonekana basi kuwa duni kuliko yeye?” Matokeo yake yakawa, nilikataa kutaja maoni yangu mwenyewe katika ushirika au kutoa maoni kuhusu mawazo yoyote aliyoshirikisha. Wakati mmoja, dada yangu, alipopata utambuzi fulani kutoka kwa kula na kunywa fungu fulani la neno la Mungu, alihisi kuwa kulikuwa na kasoro fulani na hali yetu na kuniuliza kama ningekuwa radhi kuwasiliana naye kuhusu fungu hilo la neno la Mungu. Mara tu alipouliza, mawazo haya yote na hisia za chuki zilitanda juujuu: “Unataka tu kujishuhudia mwenyewe, kuwa na wasikilizaji wa kuhubiria. Kwa nini niwasiliane na wewe?” Hata nilifika kiwango cha kuhepa mkutano ili isinibidi kumsikiliza. Baada ya muda, nilihisi uzito mkubwa moyoni mwangu, nilijua kitu fulani kilikuwa kibaya na hali yangu, lakini sikuweza kufikiria njia nzuri ya kutatua mgogoro wangu wa ndani. Kile nilichoweza kufanya tu ni kujishughulisha kikamilifu katika wajibu wangu, kula na kunywa neno la Mungu, na kuimba nyimbo za injili ili kujizuia kutokana na hisia hizi hasi. Hata hivyo, kila mara nililazimika kukabiliana na hali ya sasa, uharibifu huo huo ungeinuka katika moyo wangu—mambo yalikuwa yanazidi kuwa mabaya, sio mazuri—na sikuwa na dokezo la nini kufanya kuhusu hayo.

Jumamosi, 23 Novemba 2019

Kupata Ahueni kwa Njia ya Kumwamini Mungu

Zenye Kupumzisha
Zhuanbian Mji wa Shanghai
Ingawa nilikuwa nikimfuata Mungu kwa miaka mingi, nilikuwa karibu sijafanya maendeleo yoyote na kuingia kwangu katika maisha, na hii ilinifanya nihisi kuwa na wasiwasi sana. Hasa wakati niliposikia rekodi ya mahubiri juu ya kuingia kwa maisha, na kusikia mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu akizungumza na ndugu wa kiume na wa, nilihisi nikiwa nimejawa na wasiwasi nikimsikia akisema jambo kama hili, “Nyinyi sasa mnamwamini Mungu na mmeonja uzuri wa ukimbizaji wa ukweli. Nyinyi mmeanza kuingia kwa njia sahihi na mmejaa imani katika ukimbizaji wenu wa wokovu.” Nikawaza, “Watu hawa wamemwamini Mungu kwa muda mfupi sana lakini wameingia tayari na wamejaa imani sana kuhusu kuokolewa. Na bado niko hapa nikiwa nimemwamini Mungu hadi sasa na bado sijaipata ukweli na tabia yangu katika maisha haijapitia mabadiliko yoyote kamwe, bila kujali kuwa nilikuwa nimeingia kwa njia sahihi. Ni rahisi kuongelea kufikia wokovu kuliko kukuweka katika vitendo!” Niliwaza jinsi hao wa hapo juu walifanya ushirika kwamba ukweli ungeweza kutatua upotovu wote wa wanadamu, lakini sikuwa nimepitia jambo hili kamwe. Hata nilihisi kwamba ukweli ungeweza kutatua upotovu wa watu wengine lakini sio wangu mwenyewe, kwa hiyo nilipoteza imani katika ukimbizaji wangu wa ukweli na wa wokovu. Ingawa nilikuwa na ufahamu kwamba hali yangu mwenyewe haikuwa sahihi, hapakuwa na njia yoyote ambayo ningeweza kuiepuka, hivyo ningeweza tu kumlilia Mungu kwa msaada. Baadaye, maneno Yake yalinipatia nuru, yakinifanya nione ni kwa nini nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi hivyo na bado sikuwa nimeendelea katika maisha, na kwa nini hali yangu haikuwa imepitia mabadiliko yoyote. Mungu pia aliniweka kwa njia ya kutenda na kuingia katika ukweli.

Alhamisi, 21 Novemba 2019

Asili ya Upendo wa Mungu Ni Nini?

Zenye Kupumzisha
Siqiu Mji wa Suihua, Mkoa wa Heilongjiang
Wakati wowote ninapoona kifungu kinachofuata cha neno la Mungu, “Ikiwa daima umekuwa mwaminifu sana Kwangu na kunipenda, lakini unapitia mateso ya maradhi, umaskini wa maisha, na kutelekezwa na marafiki na jamaa au kupitia maafa mengine yoyote maishani, basi, uaminifu na mapenzi yako Kwangu yataendelea kuwepo?” (“Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ninahisi hasa nisiye na furaha—hisi ya huzuni hunyatia ndani yangu na moyo wangu husema malalamiko yake yasiyoghuna: Ewe Mungu, Unawezaje kuruhusu wale walio waaminifu Kwako na wanaokupenda Wewe kukutana na msiba wa jinsi hiyo? Matokeo yake, nimekuwa na wakati mgumu kuelewa maana ya mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu ambaye alisema, “Mahitaji ya mwisho ya Mungu ya mtu ni ya kupenda na ya kweli.”

Alhamisi, 31 Oktoba 2019

Ninapata njia ya kumjua Mungu

Ninaona njia ya kumjua Mungu
Xiaocao Mji wa Changzhi, Mkoa wa Shanxi
Siku moja, niliona kifungu hiki kifuatacho cha neno la Mungu kwa maandishi “Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu”: “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. … Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi cha kwamba aligeuka na kuwa mwepesi na mchangamfu kama njiwa, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyeathirika na hali ya hewa. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache” (Neno Laonekana katika Mwili).

Jumatano, 30 Oktoba 2019

Maneno ya Mungu Yaliondoa Dhana Zangu

Maneno ya Mungu Yaliniongoza Kutoka Katika Matatizo
Xiao Rui Mji wa Panzhihua, Mkoa wa Sichuan
Nilipokuwa nikihubiri injili nilikutana na viongozi wa dini ambao walisema uongo ili kupinga na kuvuruga, na kuwaita polisi. Hili lilisababisha wale niliokuwa nikihubiria kutothubutu kuwasiliana nasi, na wale ambao walikuwa tu wameikubali injili kutoweza kuwa na imani katika kazi ya Mungu. Nilipofanya kazi kwa bidii sana lakini matokeo yalikuwa duni, nilifikiri: kazi ya Kiinjili ni ngumu sana kutekeleza. Lingekuwa jambo la kustaajabisha sana kama Mungu angeonyesha miujiza kiasi na kuwaadhibu wale ambao husema uongo pamoja na wale ambao kwa uzito kabisa humpinga Mungu kuwaonyesha wale ambao wamedanganywa. Basi si kazi ya injili ingetekelezwa kwa haraka zaidi? Haingekuwa vigumu sana kwetu kuhubiri injili.... 

Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu

Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu
Qingxin Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Zamani, sikuelewa kazi ya Mungu ya kuwaokoa binadamu. Nilidhani kuwa almradi mtu fulani hufichua upotovu katika kazi yake au hufanya makosa ambayo huiharibu kazi ya kanisa, mtu huyo atakabiliwa na rada, au kupoteza kazi yake au aathiriwe na adhabu. Hiyo ni haki ya Mungu. Kutokana na ufahamu huu usio sahihi, pamoja na hofu ya kupoteza kazi yangu kutokana na kufanya makosa katika kazi yangu, nilifikiria juu ya utaratibu “mjanja”: Wakati wowote ninapofanya kitu vibaya, mimi hujaribu niwezavyo kutowaacha viongozi wajue kwanza, na kwa haraka kujaribu kukifidia mwenyewe na kufanya kila linalowezekana ili kukisawazisha. Je, si hilo basi litanisaidia kuhifadhi kazi yangu? Kwa hiyo, wakati wowote nilipowapa ripoti juu ya kazi yangu, ningepunguza masuala makubwa kuwa madogo na masuala madogo kuwa si kitu. Iwapo wakati mwingine nilikuwa baridi ningefanya liwezekanalo ili kulifunika mbele ya viongozi na kujifanya kuwa mtendaji zaidi na chanya, nikiwa na hofu kwamba viongozi wangenifikiria kuwa asiyeweza na kuacha kunitumia. Hiyo hivyo tu, ningelindwa kwa makini sana dhidi ya Mungu na viongozi katika kila kitu nilichokifanya.

Jumapili, 20 Oktoba 2019

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.Huzuni iliyoje! Kuokolewa kwa mwanadamu hakuwezi kutenganishwa na usimamizi wa Mungu, aidha hakuwezi kutenganishwa na mipango ya Mungu. Na bado mwanadamu hafikirii chochote kuhusu usimamizi wa Mungu, na hivyo anaendelea kujitenga mbali na Mungu. Kutokana na hayo, idadi ya watu wanaomfuata Mungu inaendelea kuongezeka bila kujua mambo yanayohusiana na kuokolewa kwa mwanadamu kama vile uumbaji ni nini, kuamini kwa Mungu ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na kadhalika. Kufikia sasa, basi, lazima tuzungumze kuhusu usimamizi wa Mungu, ndiposa kila mfuasi ajue wazi umuhimu wa kumfuata Mungu na kumwamini. Watakuwa na uwezo wa kuchagua njia watakayoifuata ipasavyo, badala ya kumfuata Mungu tu ili kupata baraka, au kuepukana na majanga, au kuwa na mafanikio.

Alhamisi, 17 Oktoba 2019

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kunayo siri kubwa moyoni mwako, ambayo hujawahi kuifahamu kamwe, kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu bila mwanga. Moyo wako na roho yako vimepokonywa na yule mwovu. Macho yako yamezuiwa kwa giza yasione, na huwezi kuliona jua angani wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu, na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako kwa haki, kila kitu ambacho Mwenye uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya mateso isiyokuwa na mwisho, bila nguvu ya kukuokoa, bila matumaini ya kurudi ukiwa hai, na yote unayofanya ni kupambana na kusonga kila siku.… Tokea wakati huo, hungeweza kuepuka kuteswa na yule mwovu, uliwekwa mbali na baraka za mwenye Uweza, mbali na kukimu kwa mwenye Uweza, unatembea katika njia ambayo huwezi kurejea nyuma tena. Kuitwa mara milioni hakuwezi kusisimua moyo wako na roho yako. Unalala fofofo mikononi mwa yule mwovu, ambaye amekushawishi katika ulimwengu usio na mipaka, bila mwelekeo na bila alama za barabarani. Tokea hapo, umepoteza hali yako ya asili ya kutokuwa na hatia na utakatifu wako, na kuanza kujificha kutokana na utunzaji wa mwenye Uweza. Ndani ya moyo wako, yule mwovu anakuelekeza katika kila jambo na anakuwa uhai wako. Humwogopi tena, kumwepuka, au kumshuku; badala yake, unamchukulia kama Mungu aliye moyoni mwako. Unaanza kumtunza na kumwabudu, na nyinyi wawili mnakuwa msiotengana kama mwili na kivuli chake, kila akitoa nafsi yake kwa mwingine katika uzima na mauti. Hujui lolote kabisa kuhusu mahali ulikotoka, kwa nini ulizaliwa, au kwa nini utakufa. Unamtazama Mwenye uweza kama mgeni; hujui mwanzo Wake, sembuse yale yote ambayo Amekutendea. Kila kitu kitokacho Kwake kimekuwa cha kuchukiza kwako. Huvitunzi wala kujua thamani yavyo. Unatembea kando na yule mwovu, kuanzia siku ile ulipoanza Mwenye uweza alianza kukukimu. Wewe na yule mwovu mmepitia maelfu ya miaka ya dhoruba na tufani pamoja, na pamoja naye, mnampinga Mungu ambaye alikuwa chanzo cha uhai wako. Hujui lolote kuhusu kutubu, sembuse kwamba umefikia ukingo wa kuangamia. Unasahau kwamba yule mwovu amekujaribu na kukutesa; umesahau asili yako. Kwa njia hii, yule mwovu amekuwa akikuharibu, hatua baada ya hatua, hata mpaka leo. Moyo wako na roho yako vimekufa ganzi na vimeoza. Umeacha kulalamika juu ya maudhi ya dunia ya wanadamu, na huamini tena kwamba dunia si ya haki. Bado hujali sana kama Mwenye uweza yupo. Hii ni kwa sababu ulimchukulia yule mwovu kuwa baba yako wa kweli kitambo, na huwezi tena kutengana naye. Hii ndiyo siri iliyo moyoni mwako.

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewazia hili: Mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. Nyote mmetazamia kufika kwa wakati huo, na uaminifu wenu ni wa kusifika, imani yenu kweli ni ya kuleta wivu, lakini mnatambua kuwa mmefanya kosa kuu? Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: Wingu hili jeupe linaashiria nini? Na kwa kuwa wafuasi wengi wa Yesu wanangoja kurejea Kwake, Atashuka miongoni mwa watu wapi? Iwapo ninyi ni wa kwanza kati ya wale ambao Yesu Atawashukia, Je, wengine hawataona jambo hili kama lisilo la haki sana? Najua kuwa nyinyi mna ukweli mkubwa na utiifu kwa Yesu, lakini mmewahi kukutana na Yesu? Mnajua tabia Yake? Mmewahi kuishi na Yeye? Mnaelewa kiasi gani kumhusu kwa kweli? Wengine watasema kuwa maneno haya yanawaweka katika tatizo gumu. Watasema, “Nimesoma Biblia kuanzia mwanzo hadi mwisho mara nyingi sana. Nitakosaje kumwelewa Yesu? Usijali kuhusu tabia ya Yesu—najua hata rangi ya nguo Alizopenda kuvaa. Je, haushushi hadhi yangu ukisema simwelewi?” Napendekeza kuwa usiyapinge masuala haya; ni heri utulie na kufanya ushirika juu ya maswali yafuatayo: Kwanza, unajua uhalisi ni nini, na nadharia ni nini? Pili, unajua dhana ni nini, na ukweli ni nini? Tatu, unajua kile kinachowazwa na kile kilicho halisi?

Jumanne, 15 Oktoba 2019

1. Kumjua Mungu ni nini hasa? Kuwa kwa ufahamu wa Biblia na nadharia ya teolojia unaweza kuchukuliwa kama kumjua Mungu?

X. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Jinsi ya Kumjua Mungu

1. Kumjua Mungu ni nini hasa? Kuwa kwa ufahamu wa Biblia na nadharia ya teolojia unaweza kuchukuliwa kama kumjua Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kumjua Mungu kunamaanisha nini? Kunamaanisha kwamba mwanadamu anajua shangwe, hasira, huzuni na furaha ya Mungu; huku ndiko kumjua Mungu. Unasema kwamba umemwona Mungu, ilhali huelewi shangwe, hasira, huzuni, na furaha ya Mungu, huelewi tabia Yake, wala huelewi haki Yake. Huna ufahamu wa rehema Zake, na hujui Anachokipenda ama Anachokichukia.Huu si ufahamu wa Mungu. Ikiwa unamjua, unamwelewa, na unaweza kuelewa mapenzi Yake kiasi, basi unaweza kumwamini kwa kweli, kumtii kwa kweli, kumpenda kwa kweli, na kumwabudu Yeye kwa kweli. Ikiwa huelewi mambo haya, basi unafuata tu, mtu fulani anayefuata tu na kufuata umati. Hiyo haiwezi kuitwa kutii kwa kweli au ibada ya kweli. Je! Ibada ya kweli inafanyika vipi? Hakuna wowote wanaomjua Mungu na kumwona Mungu kwa kweli ambao hawamwabudu Yeye, ambao hawamheshimu. Wote lazima wasujudu na kumwabudu Yeye. Kwa sasa, wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, kadri watu wanavyokuwa na ufahamu zaidi wa asili ya uungu wa Mungu, wa tabia Yake na kile Anacho na alicho, ndivyo wanavyovithamini zaidi na kumcha Yeye. Kwa kawaida, ufahamu mdogo unamaanisha kutokuwa makini zaidi, na kwamba Mungu anachukuliwa kama mwanadamu. Ikiwa watu wanamjua Mungu na kumwona kweli, watatetemeka kwa hofu. Kwa nini Yohana alisema, “Yeye anayekuja baada ya mimi ni mwenye nguvu kuniliko, ambaye mimi si wa kufaa kubeba viatu vyake”? Ijapokuwa ufahamu wa ndani ya moyo wake haukuwa wa kina kirefu sana, lakini alijua kwamba Mungu ni wa ajabu. Ni watu wangapi wanaoweza kumcha Mungu sasa? Bila kuijua tabia Yake, mtu anawezaje kumheshimu? Ikiwa watu hawajui kiini cha Kristo na hawaelewi tabia ya Mungu, hawawezi kumwabudu Mungu wa vitendo kwa kweli. Ikiwa watu wanaona tu kuonekana kwa nje kwa kawaida kwa Kristo na hawajui asili Yake, ni rahisi kwa wao kumchukulia Kristo kama mtu wa kawaida. Huenda wakachukua mtazamo usio wa heshima Kwake, wanaweza kumdanganya, kumkataa, kutomtii, na kutoa hukumu Kwake. Wanaweza kujiona kuwa sahihi na kuchukulia neno Lake na kazi Yake kama yasiyo na maana, wahodhi mawazo kumhusu Mungu, na kumshutumu na kumkufuru. Ili kutatua masuala haya mtu lazima ajue kiini cha Kristo, uungu wa Kristo. Hiki ndicho kipengele kikuu cha kumjua Mungu; ni kile waumini wote wanapaswa kutimiza.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani.

Alhamisi, 10 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu



Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani, kisha Akaondoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, Mungu amefanya kazi nyingi, lakini ulijua kwamba kazi anayoifanya Mungu leo ni nyingi kuliko awali na kipimo ni kikubwa zaidi? Hii ndiyo maana Nasema Mungu amefanya jambo kubwa miongoni mwa wanadamu.

Jumatatu, 7 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kazi ya Mungu,Neno la Mungu,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu|Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushikiriane kuhusu mada ya kumfuata Mungu. Lakini, lazima Niwakumbushe wote wanaoyasoma maneno haya kwamba neno la Mungu huelekezwa kwa wale wanaomtambua na wale wanaomfuata Mungu, na sio kwa watu wote wa ulimwengu, wakiwemo wale wasiomtambua Mungu.

Jumapili, 6 Oktoba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo


Neno la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi.

Alhamisi, 3 Oktoba 2019

Matamshi ya Kristo | Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. 

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

kazi ya Mungu,Neno la Mungu,ukweli

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)

Punde tu Shetani anaposhindwa, hivyo ni kusema, punde tu mwanadamu anaposhindwa kabisa, mwanadamu ataelewa kwamba kazi yake yote ni kwa ajili ya wokovu, na kuwa mbinu ya wokovu huu ni kurejesha kutoka kwa mikono ya Shetani. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani.

Jumanne, 1 Oktoba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza)

Neno la Mungu,kazi ya Mungu,Kumjua Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu(Sehemu ya Kwanza)

Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo, na mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kufanya mipango yako mwenyewe, na huna uwezo wa kujitawala mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinadhibitiwa na mikono Yake. 

Jumatatu, 30 Septemba 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Kupata Mwili,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

    Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe.

Jumapili, 29 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo| Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili)

Wakati kazi ya Mungu inafikia hatua fulani, na usimamizi Wake kufikia hatua fulani, wale wanaoutafuta moyo Wake wote huwa na uwezo wa kutimiza matakwa yake. Mungu humwekea mwanadamu matakwa kulingana na viwango Vyake mwenyewe, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Akiwa anazungumzia usimamizi Wake, Yeye humwonyesha njia mwanadamu , na kumpa mwanadamu namna ya kudumu. Usimamizi wa Mungu na vitendo vya mwanadamu vipo katika hatua sawia kikazi, na yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mungu yanagusia mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, na yanazungumzia kuhusu yale yafaayo kufanywa na mwanadamu, na mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, hugusia kazi ya Mungu; hakuna wakati ambao haya mawili yanaweza kutenganishwa.