Smiley face

Jumanne, 31 Oktoba 2017

Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu



Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni:
1. Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria, ama kurudia kazi ya awali, ama kuhisi hali ya kumbukumbu kwa vitu vilivyopita; ni Mungu ambaye ni mpya kila wakati na hazeeki, na kila siku anazungumza maneno mapya. Lazima uyafuate yale ambayo lazima yafuatwe leo; haya ni majukumu na kazi ya mwanadamu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Dibaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Dibaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Dibaji



Mwenyezi Mungu alisema: Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, sembuse kujua kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, kwamba wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa uzito kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao.

Jumatatu, 30 Oktoba 2017

Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika Ndio Wanaoingia Katika Uhalisi wa Ukweli



Mwenyezi Mungu alisema: Njia ambayo Roho Mtakatifu huchukua ndani ya watu ni kuvuta kwanza mioyo yao kutoka kwa watu, matukio, na vitu vyote, na kuingiza ndani ya maneno ya Mungu ili ndani ya mioyo yao wote waamini kwamba maneno ya Mungu hayana shaka kabisa na ni kweli kabisa. Kwa vile unaamini katika Mungu lazima uamini katika maneno Yake; ikiwa umeamini katika Mungu kwa miaka mingi lakini hujui njia ambayo Roho Mtakatifu hufuata, wewe kweli ni muumini? Ili kutimiza maisha ya mtu wa kawaida na maisha yanayofaa ya mtu na Mungu, lazima kwanza uamini maneno Yake.

Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu



Mwenyezi Mungu alisema: Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza kwa urasimu kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinayotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu.

Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari



Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii. Watu walikuwa wakisema kwamba hawakustahili kuuona uso wa Mungu au kusikia maneno Yake.

Jumapili, 29 Oktoba 2017

Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Ili uwe na ushuhuda kwa Mungu na kuliaibisha joka jekundu ni sharti uwe na kanuni, na sharti: Katika moyo wako ni lazima umpende Mungu na uingie katika maneno ya Mungu. Kama huingii katika maneno ya Mungu, basi hutakuwa na njia ya kumuaibisha Shetani. Katika ukuaji wa maisha yako, unalikataa joka kuu jekundu na kuliletea aibu kamili, na ni hapo tu ndipo hili joka jekundu kweli linaaibika. Kadiri unavyohiyari kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo, ndivyo unavyothibitisha kwamba unampenda Mungu na kulichukia joka kuu jekundu; kadiri unavyotii maneno ya Mungu, ndivyo unavyothibitisha kwamba unautamani ukweli.

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini


Mwenyezi Mungu alisema: Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, haya ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu.

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu



Mwenyezi Mungu alisema: Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo.

Jumamosi, 28 Oktoba 2017

Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi



Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kiwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi. Mambo si rahisi kama ulivyofikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hapo ndipo unapoumiliki uhalisi, hapo ndipo umeupata uelewa na kimo cha kweli. Lazima uwe na uwezo wa kuhimili uchunguzi kwa muda mrefu, lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kuidhihirisha sura ambayo inahitajika kwako na Mungu.

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli


Mwenyezi Mungu alisema: Katika matendo, amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri. Kutenda ukweli na kuzishika amri sio vitendo vinavyopingana, lakini badala yake vinahusiana.

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje


Mwenyezi Mungu alisema: Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

Ijumaa, 27 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Uzoefu


Mwenyezi Mungu alisema: Katika uzoefu wote wa Petro, alikumbana na mamia ya majaribio. Ingawa watu wa leo wanafahamu neno “jaribio,” wao huchanganyikiwa kuhusiana na maana yake ya kweli na hali. Mungu hutuliza azimio la watu, husafisha imani yao, na hukamilisha kila sehemu yao—na hii hufanikishwa kimsingi kupitia majaribio, ambayo pia ni kazi ya Roho Mtakatifu iliyofichwa. Inaonekana kama kwamba Mungu amewaacha watu, na kwa hivyo wasipokuwa waangalifu, watayaona majaribio haya kama majaribu ya Shetani. Kwa kweli, majaribio mengi yanaweza kufikiriwa kuwa majaribu, na hii ni kanuni na sheria ambazo Mungu hufanya kazi kupitia kwazo. Watu wakiishi mbele ya Mungu kwa kweli, wataona vitu vile kama majaribio kutoka kwa Mungu, na hawataviruhusu viponyoke. Mtu akisema kwamba kwa sababu Mungu yu pamoja naye Shetani hakika hatamwendea, hii siyo sahihi kabisa; je, basi inaweza kuelezwa vipi kwamba Yesu alikabiliwa na majaribu baada ya Yeye kufunga jangwani kwa siku arobaini?

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake


Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. Kwa sasa hakuna hata mmoja wenu aliye mkamilifu. Wakati mwingine mnaweza kutekeleza aina moja ya kazi na wakati mwingine mnaweza kutekeleza mbili; mradi tu mnampa Mungu nguvu zenu zote na kujitoa kwa ajili Yake, hatimaye mtafanywa wakamilifu na Mungu. 

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho


Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili. Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo.

Alhamisi, 26 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuingia Ndani ya Hali ya Kawaida


Watu wanapozidi kuwa wapokelevu wa maneno ya Mungu, ndivyo wanavyozidi kupata nuru na wanaendelea zaidi kufuatilia maarifa ya Mungu kwa njaa na kiu ya hali ya kuwa mwenye haki. Ni wale tu ambao wanapokea maneno ya Mungu wanaweza kuwa na matukio ya undani zaidi na yenye utajiri zaidi; ni wale tu ambao maisha yao yanakuwa ya kupendeza zaidi na zaidi. Kila mtu ambaye anafuatilia uzima lazima ashughulikie haya kana kwamba ni kazi yake, na ni sharti awe na hisia kuwa hawezi kuishi bila Mungu, na hakuna mafanikio yoyote bila Mungu, na kila kitu ni ubatili bila Mungu. Wanapaswa kuwa na azimio la kutofanya lolote bila uwepo wa Roho Mtakatifu, na kutotaka kutenda lolote zaidi kama matendo yao hayazai matunda.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi


Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu inayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi zaidi hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi zaidi bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa. Bado hawajui chochote kuhusu umuhimu mahususi wa kumwamini Mungu, na aidha hawana ufahamu wowote wa kazi muhimu kabisa ya Mungu katika mpango Wake wa usimamizi.

Umeme wa Mashariki | Sitisha Huduma ya Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Sitisha Huduma ya Kidini


Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. 

Jumatano, 25 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini


Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu.

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Matukio Aliyopitia Petro Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu


Mwenyezi Mungu alisema: Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, "Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika. Iwapo hukumu Yako itaonyesha tabia Yako, na kuruhusu tabia Yako ya haki kuonekana na viumbe wote, na iwapo inaweza kufanya upendo wangu Kwako uwe safi zaidi, ili niweze kufikia mfano wa mwenye haki, basi hukumu Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo. 

Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?


Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndinyi mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu.

Jumanne, 24 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Amri za Enzi Mpya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Amri za Enzi Mpya

Mwenyezi Mungu alisema: Mmeambiwa kuwa mjiandae kwa maneno ya Mungu, ya kuwa pasipo kujali kilichoandaliwa juu yenu, yote yamepangwa kwa mkono wa Mungu, na kwamba hakuna haja ya kuomba kwa bidii au kusali kwenu—haina maana. Ilhali kulingana na hali ya sasa, shida za kiutendaji mnazokumbana nazo hazitafakariki kwenu. Kama mnasubiri mipango ya Mungu tu, basi hatua zenu zitakaa zaidi, na kwa wale wasiojua kupitia kutakuwa na kulaza damu kwingi. Kwa hivyo, ikiwa umeshindwa kabisa kuyalewa mambo haya, basi umechanganyikiwa na kuwa mpumbavu katika uzoefu wako. Kama huna ukweli lakini maneno tu, je, si hii ni ishara ya makosa?

Umeme wa Mashariki | Waovu Lazima Waadhibiwe


Mwenyezi Mungu alisema: Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Utaitwa mwenye haki kwa sababu una uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu umekubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. 

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Kazi ya Mungu katika mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na kumsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, si mwanadamu ni adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa amehitimu kumshuhudia Mungu? Kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu—je, huu si udanganyifu?

Jumatatu, 23 Oktoba 2017

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Mwenyezi Mungu

alisema: 
Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii hasa kwamba mwili wa mwanadamu umepotoshwa ndiyo maana Mungu amemfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mlengwa wa upotovu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa pekee wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu.

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kiini cha Mwili Ulio na Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi. 

Jumapili, 22 Oktoba 2017

Nitampenda Mungu Maisha Yangu Yote | "Mpendwa Wangu, Tafadhali Nisubiri" (Video Rasmi ya Muziki)



Mpendwa Wangu, Tafadhali Nisubiri

Juu ya miti, nikiukwea mwezi wa amani. Kama mpendwa wangu, wa haki na mzuri.
Ee mpendwa wangu, Uko wapi? Sasa mimi nina machozi. Je, Wanisikia nikilia?
Wewe Ndiwe hunipa upendo. Wewe Ndiwe Unayenitunza.
Wewe Ndiwe unayeniwaza daima, Wewe Ndiwe unayeyatunza maisha yangu.

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu



Mwenyezi Mungu alisema: Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. 

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni


Mwenyezi Mungu alisema: Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. 

Jumamosi, 21 Oktoba 2017

Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja


Mwenyezi Mungu alisema: Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu.

Ijumaa, 20 Oktoba 2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli


Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu,  ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu


Mwenyezi Mungu alisema: Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti.

Umeme wa Mashariki | Maonyo Matatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Maonyo Matatu


Mwenyezi Mungu alisema: Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla ya kuuamua mwisho wenu, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu. Kabla Sijaendelea, mnafaa kwanza kuelewa yafuatayo: Maneno Ninayoongea ni ukweli unaoelekezwa kwa wanadamu wote, na wala hayajaelekezwa kwa mtu mahususi au aina fulani ya mtu. Kwa hiyo, mnapaswa kumakinikia kupokea maneno Yangu kutoka katika mtazamo wa ukweli, na vile vile mdumishe mtazamo wa uzingativu na uaminifu kamili. Msipuuze hata neno moja au ukweli Ninaoongea, na wala usichukulie maneno Yangu kwa dharau. Katika maisha yenu, Naona mengi ambayo mnafanya ambayo hayana uhusiano na ukweli, kwa hivyo Nawaambia moja kwa moja muwe watumishi wa ukweli na wala si kutawaliwa na maovu na ubaya. Msikanyage ukweli na kuchafua sehemu yoyote ya nyumba ya Mungu. Hili ndilo onyo Langu kwenu. Sasa Nitaanza kuzungumza kuhusu mada ya sasa:

Kwanza, kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu mnatambua kwamba nyinyi mmehesabiwa miongoni mwa wale walio katika nyumba ya Mungu, basi mnastahili kumletea Mungu utulivu wa akili katika mambo yote na kumtosheleza katika kila jambo. Kwa maneno mengine, lazima muwe wenye maadili katika matendo yenu na kutii ukweli katika mambo kama hayo. Kama hali hii inazidi uwezo wako, basi utachukiwa na kukataliwa na Mungu na vilevile kukataliwa kwa dharau na kila mwanadamu. Punde utakapokuwa katika hali mbaya kama hii, basi hauwezi kuhesabiwa miongoni mwa wale walio kwenye nyumba ya Mungu. Hii ndiyo maana ya kutoidhinishwa na Mungu.

Pili, mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. Kile Ninachoongea ni rahisi sana lakini ni kigumu maradufu kwenu. Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu. Si ajabu kwamba Nina matendo mengine kwa wale ambao si waaminifu. Bila shaka, Ninaelewa ugumu mkuu mnaokumbana nao kwa kuwa binadamu waaminifu. Nyinyi wote ni werevu sana na stadi katika kupima uungwana wa mtu kwa kipimio chenu wenyewe; kwa hiy kazi Yangu inakuwa rahisi zaidi. Na kwa sababu nyinyi mnaficha siri katika mioyo yenu, basi, Nitawatumeni, mmoja baada ya mwingine,, katika janga kupitia “jaribio” la moto, ili baadaye mtajitolea kabisa katika kuamini maneno Yangu. Hatimaye, Nitapokonya maneno “Mungu ni Mungu wa uaminifu,” kutoka kwa vinywa vyenu na kisha ndipo mtakapojigamba na kujitanua kifua na kulalama kwamba “ujanja ndio moyo wa binadamu.” Hali za akili zenu zitakuwa zipi wakati huu? Ninafikiri hamtajisahau sana na majivuno kama mlivyo sasa. Na sembuse hamtakuwa “wa maana sana kiasi cha kutoeleweka” kama mlivyo sasa. Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme. Unafaa kujua kama kunayo imani ya kweli na uaminifu wa kweli ndani yako, kama una rekodi ya kuteseka kwa ajili ya Mungu, na kama umemtii Mungu kikamilifu. Kama unakosa hivi Nilivyotaja, basi ndani yako kunabaki kutotii, udanganyifu, ulafi, na kutotosheka. Kwa vile moyo wako si mwaminifu, hujawahi kupokea utambuzi mzuri kutoka kwa Mungu na hujawahi kuishi katika mwangaza. Kile ambacho jaala ya mtu kitakuwa hutegemea kama anao moyo wa uaminifu na wa kweli, na kama anayo nafsi isiyo na doa. Kama wewe ni mtu asiye mwaminifu sana, mtu mwenye moyo wa kijicho na nafsi isiyo safi, basi rekodi ya majaliwa yako bila shaka ipo pale ambapo binadamu huadhibiwa. Kama unadai kwamba wewe ni mwaminifu sana, na bado kamwe hutendi kulingana na ukweli au kuongea neno la ukweli, basi bado unatarajia Mungu kukutuza? Bado unatumai Mungu akuchukue kama kipenzi Chake? Je, kufikiria huku si kwa upuzi? Unamdanganya Mungu katika mambo yote, hivyo nyumba ya Bwana inawezaje kumpa nafasi mtu kama wewe, ambaye mikono yake si safi?

Jambo la tatu Ninalotaka kuwaambia ni hili: Kila mwanadamu, katika kuishi maisha yake ya imani katika Mungu, amemkataa na kumdanganya Mungu wakati fulani. Baadhi ya matendo mabaya hayahitaji kurekodiwa kama kosa, lakini mengine hayasameheki; kwani mengi ni yale yanayokiuka amri za utawala, yaani, yanaikosea tabia ya Mungu. Wengi ambao wanajali majaliwa yao binafsi wanaweza kuuliza matendo haya ni yapi. Lazima mjue kwamba nyinyi mna kiburi na wenye majivuno kiasili, na hamko radhi kutii ukweli. Kwa sababu hii, Nitawaambia kidogo kidogo baada ya nyinyi kutafakari kujihusu. Ninawashawishi kuwa na ufahamu bora zaidi wa yaliyomo katika amri za utawala na kujua tabia ya Mungu. Vinginevyo, mtapata ugumu sana kuendelea kufunga vinywa vyenu na kufyata ndimi zenu dhidi ya kuropokwa bila kizuizi kwa mazungumzo ya mbwembwe, na bila kujua mtaikosea tabia ya Mungu na kujipata kwenye giza, mkipoteza uwepo wa Roho Mtakatifu na mwangaza. Kwa sababu nyinyi hamna maadili katika matendo yenu. Ukifanya au kusema kile ambacho hufai kufanya hivyo, basi utapokea adhabu inayokufaa. Lazima ujue kwamba ingawa wewe ni mpotovu katika maneno yako na matendo yako, Mungu ni mwenye maadili sana katika hali hizi zote. Sababu ya wewe kupokea adhabu ni kwa sababu umemkosea Mungu na wala si binadamu. Kama, katika maisha yako, wewe hutenda makosa mengi dhidi ya tabia ya Mungu, basi huna budi ila kuwa mtoto wa kuzimu. Kwa binadamu inaweza kuonekana kwamba umetenda matendo machache tu yasiyolingana na ukweli na si chochote zaidi. Je, una habari, hata hivyo, kwamba katika macho ya Mungu, tayari wewe ni mmoja ambaye kwake hakuna tena sadaka ya dhambi? Kwani umevunja amri za utawala za Mungu zaidi ya mara moja na hujaonyesha ishara yoyote ya kutubu, kwa hivyo huna chaguo lolote ila kutumbukia kuzimu pale ambapo Mungu anamwadhibu mwanadamu. Katika wakati wao wa kufuata Mungu, idadi ndogo ya watu ilitenda matendo yaliyoenda kinyume na kanuni, lakini baada ya kushughulikiwa na kuongozwa, waligundua polepole upotovu wao, na kisha wakachukua njia iliyo sawa ya uhalisi, na leo wanabaki wenye msingi imara katika njia ya Bwana. Binadamu kama hawa ndio watakaobakia mwisho. Ni wale walio waaminifu ndio Ninaowatafuta; kama wewe ni mtu mwaminifu na unayetenda kwa maadili, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu. Kama katika matendo yako huikosei tabia ya Mungu, na unatafuta mapenzi ya Mungu na unao moyo wa kumcha Mungu, basi imani yako ni ya kiwango kilichowekwa. Yeyote asiyemcha Mungu na asiye na moyo unaotetema kwa woga atakiuka amri za utawala za Mungu kwa urahisi. Wengi humhudumia Mungu kwa misingi ya hisia kali, na hawajui katu amri za utawala za Mungu, sembuse kuelewa athari za neno Lake. Na kwa hivyo, na nia zao nzuri, mara nyingi wanaishia kufanya vitu vinavyokatiza usimamizi wa Mungu. Kwa hali za uzito sana, wanatupwa nje na kunyanganywa fursa yoyote zaidi ya kumfuata, na wanatupwa kuzimu bila ya kuwa na uhusiano wowote mwingine na nyumba Yake unakoma. Watu hawa hufanya kazi katika nyumba ya Mungu wakiwa na nia nzuri zisizojua na wanaishia kuikasirisha tabia ya Mungu. Watu huleta njia zao za kuwahudumia wakuu na mabwana katika nyumba ya Mungu na kujaribu kufanya yatumike, wakidhania kwa kiburi kwamba njia kama hizo zinaweza kutumika hapa bila jitihada. Hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu hana ile tabia ya mwanakondoo bali ile ya simba. Kwa hiyo, wanaojihusisha na Mungu kwa mara ya kwanza wanashindwa kuwasiliana na Yeye, kwani moyo wa Mungu ni tofauti na ule wa binadamu. Ni baada tu ya kuelewa ukweli mwingi ndipo unapoweza kujua siku zote kumhusu Mungu. Maarifa haya si mafungu wala mafundisho, lakini yanaweza kutumika kama hazina ya kuingia katika matumaini ya karibu na Mungu, na ithibati kwamba Anafurahishwa na wewe. Kama unakosa uhalisi wa maarifa na hujajiandaa ukweli, basi huduma yako ya shauku itakuletea tu hali ya chuki ya kupindukia na kuchukizwa sana kwa Mungu. Sasa unafaa kuelewa kwamba imani katika Mungu si masomo tu ya teolojia.

Ingawa maneno Ninayotumia kuwaonya ni mafupi, vyote Nilivyovifafanua hapa ndivyo vinavyokosekana zaidi ndani yenu. Lazima mjue kwamba kile Ninachozungumzia sasa ni kwa minajili ya kazi Yangu ya mwisho miongoni mwa binadamu, kwa ajili ya kuamua hatima ya binadamu. Sipendelei kufanya kazi nyingi zaidi isiyo na maana, na wala Sipendelei kuendelea kuwaongoza wale binadamu wasio na matumaini kama mti uliooza, sembuse wale walio na nia mbaya kisiri. Pengine siku moja mtaelewa nia za dhati zinazoyasukuma maneno Yangu na michango ambayo Nimemfanyia mwanadamu. Pengine siku moja mtafahamu kanuni inayowawezesha kuamua hatima yenu binafsi.
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Alhamisi, 19 Oktoba 2017

Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli


Mwenyezi Mungu alisema: Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote.

Umeme wa Mashariki | Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (katika siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu?

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)




Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa

I
Nilitaka kulia lakini hakuna mahali palihisi sawa.
Nilitaka kuimba lakini hakuna wimbo ulipatikana.
Nilitaka kuonyesha upendo wa kiumbe aliyeumbwa.
Nikitafuta juu na chini, lakini hakuna maneno yangeweza kusema,
yangeweza kusema jinsi hasa ninavyohisi.

Jumatano, 18 Oktoba 2017

Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu



Mwenyezi Mungu alisema, Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo.

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu


Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako. Ukifika mahali hapo utafurahia kujua imani katika Mungu ni nini, namna ya kumwamini Mungu vizuri, na kile unachopaswa kufanya ili kutenda mambo kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu.

Jumanne, 17 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Je, Umekuwa Hai Tena?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Je, Umekuwa Hai Tena 


Baada ya kutimiza kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, na umefanywa mkamilifu, ingawa utakuwa huwezi kunena unabii, wala siri zozote, utakuwa unaishi kulingana na kufichua taswira ya mwanadamu. Mungu alimuumba mwanadamu, baada ya hapo mwanadamu akaharibiwa na Shetani, na uharibifu huu umewafanya watu wawe maiti—na hivyo, baada ya kuwa umebadilika, utakuwa tofauti na maiti hizi. Ni maneno ya Mungu ndiyo yanatoa uzima kwa roho za watu na kuwasababisha kuzaliwa upya, na roho za watu zinapozaliwa upya, watakuwa hai tena.Neno "wafu" linarejelea maiti ambazo hazina roho, kwa watu ambao roho zao zimekufa. 

Jumatatu, 16 Oktoba 2017

Umeme wa Mashariki | Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki  Maana ya “Mwanaadamu Halisi”


Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu huenda hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho na pia huenda hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda wale walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini, adui Yangu alipoungana katika vita na Mimi, Nilikuwa Nimeshamwambia kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kufanywa watoto wake na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake.

Jumapili, 15 Oktoba 2017

Neno la Mungu Humwongoza Mtu Kuishi Maisha Mapya | Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana



Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana
I
Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaimba nyimbo za sifa kubwa Kwako.
Wewe hutuleta katika maisha ya ufalme.
Sisi watu wa ufalme tu katika karamu yako ya fahari,
tukifurahia maneno Yako, tukitakaswa upotovu wetu.
Neno Lako hutuongoza na sisi kukufuata kwa karibu.

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kanisa, Umeme wa Mashariki,
Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu


Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mnamwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka.Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? 

Jumamosi, 14 Oktoba 2017

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili



Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho

Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo.