Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu.
Jumamosi, 31 Agosti 2019
Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili)
Ijumaa, 30 Agosti 2019
Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza)
Alhamisi, 29 Agosti 2019
Neno la Mwenyezi Mungu | Je, Utatu Mtakatifu Upo?
Jumatano, 28 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili)
Jumanne, 27 Agosti 2019
Sauti ya Mungu|Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili
Jumatatu, 26 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza)
Jumapili, 25 Agosti 2019
Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu)
Jumamosi, 24 Agosti 2019
Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili)
11. Mungu mwenye mwili Anajidhihirisha mwenyewe kwa watu kadhaa wanaomfuata Anapofanya kazi Yeye binafsi, na sio kwa viumbe wote. Alijifanya mwili ili Akamilishe hatua ya kazi Yake, na sio ili amwonyeshe mwanadamu mfano Wake. Hata hivyo, kazi Yake lazima ifanywe na Yeye binafsi, kwa hivyo inalazimu Afanye kazi hiyo katika mwili. Kazi hii inapokamilika, Ataondoka duniani; Hawezi kusalia duniani kwa muda mrefu kwa hofu ya kuzuia kazi inayokuja. Anachokionyesha kwa halaiki ni tabia Yake ya haki na matendo Yake yote, na sio umbo la mwili Wake wakati Amejifanya mwili mara mbili, kwa maana mfano wa Mungu unaweza tu kuonyeshwa kupitia kwa tabia Yake, na si kubadilishwa na mfano wa mwili Wake wa nyama.
Ijumaa, 23 Agosti 2019
Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza)
1. Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, "Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa." Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu. Haijalishi jinsi imani Yake ilivyokuwa kabla ya hii—labda wakati mwingine ilikuwa dhaifu, au wakati mwingine ilikuwa na nguvu—hayo ndiyo yalikuwa maisha Yake ya kawaida ya binadamu kabla Afanye huduma Yake.
Alhamisi, 22 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili)
Jumatano, 21 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza)
Jumanne, 20 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu” (Sehemu ya Pili)
Jumatatu, 19 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza)
1. Yohana alianza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni miaka saba kabla ya ubatizo wa Yesu. Kwa watu, kazi aliyoifanya ilionekana kuwa juu zaidi ya kazi ya baadaye ya Yesu, ilhali yeye alikuwa, hata hivyo, nabii tu. Hakufanya kazi au kuzungumza ndani ya hekalu, lakini katika miji na vijiji nje yake. Hii alifanya, bila shaka, miongoni mwa taifa la Wayahudi, hasa wale waliokuwa maskini. Ni mara chache ambapo Yohana alitangamana na watu kutoka ngazi za juu za jamii, na alieneza injili miongoni mwa watu wa kawaida wa Yudea tu ili kuandaa watu wema kwa Bwana Yesu, na kuandaa maeneo yafaayo Kwake kufanya kazi. Kwa sababu ya kuwa na nabii kama Yohana wa kuandaa njia, Bwana Yesu Alikuwa na uwezo wa kuanzisha njia Yake ya msalaba mara moja punde tu Alipowasili.
Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne)
Jumapili, 18 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu)
Jumamosi, 17 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili)
13. Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kweli kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yangechipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa cha watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, wasijue waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani. "Wanajificha tu katika unyenyekevu." Ukweli ni kwamba, wachache miongoni mwenu wanajua makusudi ya Mungu kuhusu siku za mwisho.
Ijumaa, 16 Agosti 2019
Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza)
Alhamisi, 15 Agosti 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu
Kufahamu kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mtu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu. Siku itakapofika utakapomtazama Mungu kwa kweli na kutambua hekima ya Mungu; utakapotazama matendo yote ya Mungu na kutambua kile Mungu Alicho na kile Alicho nacho; utakapotazama wingi Wake, hekima, ajabu Yake, na kazi Yake yote kwa mwanadamu, basi hapo ndipo utakuwa umefikia imani ya mafanikio kwa Mungu.
Jumanne, 13 Agosti 2019
Mwenyezi Mungu anasema | Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu
Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti.
Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Je, Umekuwa Hai Tena?
Jumatatu, 12 Agosti 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Jumapili, 11 Agosti 2019
Neno la Mwenyezi Mungu | Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu
Kwenye kipindi kile ambacho Petro alikuwa na Yesu, aliona sifa nyingi za kupendeza ndani ya Yesu, hali nyingi zenye za kustahili kuigwa, na nyingi ambazo zilizomkimu. Ingawa Petro aliona nafsi ya Mungu ndani ya Yesu katika njia nyingi, na kuona sifa nyingi za kupendeza, mara ya kwanza hakumjua Yesu. Petro alianza kumfuata Yesu alipokuwa na umri wa miaka 20, na akaendelea kufanya hivyo kwa miaka sita. Kwenye kipindi hiki cha muda, hakuwahi kupata kumjua Yesu, lakini alikuwa radhi kumfuata Yeye kutokana tu na kuvutiwa na Yeye.
Jumamosi, 10 Agosti 2019
Sauti ya Mungu|Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu
Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu. Ingawa ni uamuzi wa watu kama hawa kumfuata Mungu, hawafaidi chochote.
Ijumaa, 9 Agosti 2019
Matamshi ya Kristo | Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”
Mnayaonaje maono ya Ufalme wa Milenia? Baadhi ya watu hutafakari sana kuuhusu na kusema kuwa Ufalme wa Milenia utadumu duniani kwa miaka elfu moja, hivyo basi ikiwa waumini wazee katika kanisa hawajaoa, je, wanapaswa kuoa? Familia yangu haina pesa, je napaswa nianze kutafuta pesa? … Ufalme wa Milenia ni nini? Je, mnajua? Watu ni nusu vipofu na wanapitia mateso mengi. Kwa hakika, Ufalme wa Milenia bado haujafika rasmi. Katika hatua ya kuwafanya wanadamu wakamilike, Ufalme wa Milenia ni mfano mdogo tu; katika kipindi cha Ufalme wa Milenia uliozungumziwa na Mungu, mwanadamu atakuwa amefanywa mkamilifu.
Alhamisi, 8 Agosti 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli
Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote.
Jumatano, 7 Agosti 2019
Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu
Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria, ama kurudia kazi ya awali, ama kuhisi hali ya kumbukumbu kwa vitu vilivyopita; ni Mungu ambaye ni mpya kila wakati na hazeeki, na kila siku anazungumza maneno mapya. Lazima uyafuate yale ambayo lazima yafuatwe leo; haya ni majukumu na kazi ya mwanadamu. Ni muhimu kwamba utendaji uwekwe katika nuru iliyopo na maneno ya Mungu katika siku ya leo. Mungu hafuati masharti, na Anaweza kuzungumza kutoka kwa mitazamo mingi tofauti ili kufanya wazi hekima Yake na uwezo.
Jumanne, 6 Agosti 2019
Matamshi ya Kristo | Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno
Jumatatu, 5 Agosti 2019
Matamshi ya Mungu | Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu
Jumapili, 4 Agosti 2019
Matamshi ya Mungu|Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu
Ili uwe na ushuhuda kwa Mungu na kuliaibisha joka jekundu ni sharti uwe na kanuni, na sharti: Katika moyo wako ni lazima umpende Mungu na uingie katika maneno ya Mungu. Kama huingii katika maneno ya Mungu, basi hutakuwa na njia ya kumuaibisha Shetani. Katika ukuaji wa maisha yako, unalikataa joka kuu jekundu na kuliletea aibu kamili, na ni hapo tu ndipo hili joka jekundu kweli linaaibika. Kadiri unavyohiyari kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo, ndivyo unavyothibitisha kwamba unampenda Mungu na kulichukia joka kuu jekundu; kadiri unavyotii maneno ya Mungu, ndivyo unavyothibitisha kwamba unautamani ukweli.
Ijumaa, 2 Agosti 2019
Matamshi ya Mungu | Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini
Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha.